Wednesday, January 29, 2014

WAZIRI ANUSURIKA KIFO


Mh. Juma Ngasongwa amenusurika kifo katika ajali iliyo tokea jana jioni Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani.   Pichani anaonekana Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Dr. Loti Kiwelu akimjulia hali katika Hospitali ya Tumbi Kibaha alipo fikishwa kwa ajili ya huduma ya kwanza ambapo alihamishiwa katika Hosipitali ya Muhimbili MOI kwa ajili ya matibabu zaidi. (picha na Chris Mfinanga).   Ajali hiyo ilihusisha gari  aina ya Rav 4 mali ya Mh. Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam kuelekea morogoro ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Tanesco. ..

No comments:

Post a Comment