Wednesday, January 29, 2014

JENGO LA JMC LILIVYONUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO


Jengo la JMC likiwaka moto.
Wananchi wakishuhudia moto huo.
Magari ya zimamoto yakiwasili eneo la tukio kutoa msaada.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakipambana na moto huo.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Askari wakidumisha ulinzi eneo la tukio.
Askari akiwasili eneo hilo eneo hilo akiwa na mbwa.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vinywaji ya Bavaria wakishuhudia jengo lililo jirani nao la JMC likiungua.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kulia) akipata maelezo ya awali kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi.
Wafanyakazi kutoka Kampuni ya Ultimate Security wakiwa eneo hilo kuongeza nguvu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akiongea na wananchi eneo la tukio.
Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi wakiwa eneo la tukio.

JENGO la JMC linalomilikiwa na Zhihir Shivji lililopo eneo la Kamata mtaa wa Kasanga, Kiriakoo jijini Dar es Salaam leo majira ya saa nane mchana lilinusurika kuteketea kwa moto ulioanzia ghorofa ya saba.

Chanzo cha moto huo na mali zilizoteketea mpaka sasa bado havijafahamika.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alifika eneo la tukio na kuagiza wamiliki wa majengo kuweka vyombo vya kutambua hitilafu mbalimbali kwenye majengo yao.

No comments:

Post a Comment