Tuesday, February 4, 2014

IRANI YAGUNDUA NDEGE MPYA YA KIVITA YENYE UWEZO WA AINA YAKE


Iran kuzalisha ndege mpya za kivita 'Saiqe'


Naibu Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran imeanza kuzalisha kizazi kipya cha ndege za kivita aina ya Saiqe. Brigedia Jenerali Alireza Barkhor amesema kuwa utengenezaji na uzalishaji wa ndege hiyo ya kisasa ya kivita umo katika awamu zake za mwisho. Ameongeza kuwa ndege hiyo ya kivita itazinduliwa katika miezi michache ijayo. Miongoni mwa sifa za ndege hiyo ya kisasa ni uwezo wake wa kubeba na kufyatua maroketi, mabomu na makombora ya aina mbalimbali na ina rada ya kisasa. Uwezo mkubwa wa ndege hiyo ya Saiqe na kasi yake kubwa vinaipa sifa makhsusi kati ya ndege za kisasa za kivita. Ndege nyingine za kivita zinazotengenezwa hapa nchini ni pamoja na Azarakhsh na Qaher-313








No comments:

Post a Comment