WENGI wamesikia historia ya wale mapacha walioungana kiwiliwili; baada ya kimya chao cha muda mrefu wengi watapenda kujua wako wapi na wanafanya nini?
Wanafunzi hao Maria Mwakikuti na Consolata Mwakikuti wanasoma shule ya sekondari ya Nyota ya Asubuhi iliyopo Kidabaga, wilayani Kilolo mkoani Iringa.
Uongozi wa shule umeweka masharti magumu kidogo ili kukutana nao, lakini mtandao huu unaendelea kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo ili watanzania waweze kujua maendeleo yao.
Kwa wasiofahamu mapacha hao, ni wenyeji wa wilaya ya Makete mkoani Njombe; wilayani humo wanaishi katika kijiji cha Ikonda, hapo ndipo walipozaliwa na kumalizia elimu yao ya msingi.
Walipokuwa wakimaliza elimu ya msingi, walikuwa na umri wa miaka 13 na katika ndoto zao kwa pamoja walisema wanataka kuwa wataalamu wa kompyuta.
Miaka mitatu sasa imepita toka wawakilishi wa mtandao huu wakutane nao katika hafla ya kuwapongeza baada ya kufaulu vizuri mitihani yao ya darasa la saba.
Wapo kidato cha nne katika shule hiyo ya Nyota ya Asubuhi; walijiunga na shule hiyo baada ya walezi wao kukataa wasijiunge na shule ya sekondari ya Jangwani walikokuwa wamepangiwa baada ya matokeo yao kutoka
Hivi sasa wana miaka 17. wanaukaribia utu uzima, kwa vyovyote watakuwa na mengi ya kuzungumza kuhusu maisha yao ya sasa, elimu yao, changamoto wanazopata na matarajio yao ya baadaye.
No comments:
Post a Comment