Kiongozi wa zamani wa waasi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Bosco Ntagandaa amefikishwa katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC huko The Hague.
Mwendesha mkuu wa mashitaka ICC,Fatou Bensouda amesema kuwa Ntaganda aliamuru watu kuwaua na kuwabaka waathiriwa wa vita.
Bensouda pia alisema kuwa Bosco alihusika pakubwa katika kupanga mashambulizi dhidi ya raia. Kadhalika aliongeza kuwa Ntaganda aliwahukumu watu kwa msingi ya kabila lao kwa kuwafukuza, kuwaua, kuamuru wabakwe na kuwatumia kama watumwa wa ngono.
Hata hivyo Generali Ntanganda amekanusha kuhusika na makosa ya kivita katika maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo miaka kumi iliyopita.
Bosco Ntaganda -- anayefahamika sana Nchini Congo kwa jina Terminator yuko mahakamani kama mshukiwa wa kwanza kuwahi kujisalimisha mwenyewe.
Alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani Nchini Rwanda mwaka jana.
Bwana Ntaganda ambaye ni mshukiwa aliyekuwa akisakwa zaidi na ICC anatuhumiwa kutekeleza makosa 18 ikiwemo kuwatumia wasichana kama wafungwa wa ngono.
Majaji katika kesi hiyo wataamua kama Ntaganda ana kesi ya kujibu au la.
No comments:
Post a Comment