Sunday, February 16, 2014

FUNDI SAMWELI ATHIBITISHA KUACHANA NA MKEWE MWANAMUZIKI SARAHA










Producer wa wimbo mpya wa Ben Pol, ‘Unanichora’, Fundi Samwel ambaye ni raia wa Sweden, amethibitisha kuachana na mke wake, Saraha.

Mtayarishaji huyo amesema sababu kubwa ya kuachana ni ubusy waliokuwa nao uliosababishwa na muziki na hivyo kuwafanya wasiwe karibu kwa kipindi kirefu.

“Mimi na Saraha tuliachana, kilikuwa kitu kibaya kwangu na kwake pia ndio maana nilikuwa kimya kidogo mwaka huu sababu unajua moyo ulivunjika sana na mood lazima ipotee,” Fundi Samwel amemuambia Sam Misago kwenye kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio.

“Unajua kukaa na kufanya muziki lazima utumie muda sana na unatumia akili sana, na hata yeye alifanya kazi nzuri hapa, alikuwa busy sana, namimi nilikuwa busy ya studio. Unajua anakuta foleni kila siku halafu wewe unapiga kazi kama masaa 15 hivi and then unachoka sasa huwezo kuongea vizuri. Hata Saraha alichoka, unajua tulishindwa kuongea vizuri na kitu kiliendelea. And then tulipofika Sweden, unajua upendo uliisha tu, uliisha kabisa,” aliongeza.

Samwel ambaye tayari amerejea kwao nchini Sweden amesema yupo Tanzania kwa wiki mbili kutengeneza nyimbo kadhaa

No comments:

Post a Comment