Friday, February 7, 2014

SAMATTA: TUZO YA MASHABIKI NI KITU KIKUBWA

Samata-Bwana580211 62199
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunguka na kusema kuwa anajivunia tuzo aliyopewa ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu yake ya TP Mazembe. Samatta alichaguliwa na mashabiki wa klabu kama mchezaji bora wa klabu kwa mwaka 2013.
Mfungaji huyo bora wa michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika amesema hayo wakati akizungumza na mtandao huu siku ya leo.
"Nafurahi tu kwa kupata tuzo hiyo, maana wapo wachezaji wengi pia ambao walistahili. Inaleta maana kubwa kama tuzo hiyo inatoka kwa mashabiki wa timu yako."
Samatta ametokea kuwa mchezaji muhimu sana wa klabu hiyo ambayo aliisaidia kufika hatua ya fainali ya michuano ya vilabu barani Afrika mwaka uliopita. Endelea kufuatia mtandao huu ambao kwa sasa upo katika jitihada za kufanya mahojiano na mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania

No comments:

Post a Comment