Msanii kutoka Sudan, K Denk ambaye amejijengea jina Kubwa Afrika Mashariki akiwa mshiriki wa mashindano ya Tusker Project Fame, amewashtusha wengi kwa hatua yake ya kuamua kuingia vitani katika mapambano yanayoendelea sasa huko Sudan Kusini akiwa kama muasi.
Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Kuonck Deng ameweka picha zake katika ukurasa wake wa facebook akiwa ameshikilia silaha kali (Bunduki aina ya AK47) tayari kwa mapambano katika kile alichokiita kama kupigania uhuru wake.
Kufuatia kuweka picha hii mtandaoni, K Denk amepata maoni mbalimbali yanayokosoa hatua yake hii hususan kutoka kwa mastaa/washiriki wenzake kutoka Tusker Project Fame akiwepo Ngangalito na Juvenalis kutokana na ukweli kuwa vita sio suluhisho la matatizo yaliyopo huko Sudan kwa sasa.
No comments:
Post a Comment