Manchester united iliambulia kichapo cha mabao mawili kwa nunge dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki katika mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na ghamu na mashabiki wa ligi kuu ya Mabingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo iliyokuwa ikipigiwa upatu kuwa itakayosisimua muamko mpya wa vijana wa David Moyes ilikosa makali kabisa.
Manchester united ilikamilisha shambulizi moja pekee kunako dakika ya 89 ya kipindi cha pili Robin van Persie alipoishambulia lango la wenyeji wao huko Ugiriki.
Alejandro Dominguez alifunga bao la kwanza kunako dakika ya 38.
Kiungo wa Arsenal aliyeko Ugiriki kwa mkopo Joel Campbell akikamilisha kichapo hicho kunako dakika ya 54 ya kipindi cha pili.
Kutokana na ushindi huo mkubwa ,Mabingwa hao wa Ugiriki Olympiakos waliendeleza msururu wao mkubwa wa matokeo mazuri.
Olympiakos wameshinda mechi 24 kati ya 26 walizocheza hivi karibuni na kufikia sasa wanaongoza kwa zaidi ya pointi 20.
Manchester sasa inakabiliwa na mlima wa kupanda katika raundi ya pili sawa na timu zengine mbili za Uingereza , Manchester City na Arsenal ambazo pia zililazwa mabao mawili kwa nunge juma lililopita wapinzani wao.
No comments:
Post a Comment