Friday, February 7, 2014

Kikwete awaonya wanasiasa

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto), akizungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa baada ya kuhutubia mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa CUF,  Maalim Seif Sharrif Hamad na kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Mziray. Picha na Salim Shao

Dar es SalaamRais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao.Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.Aliwaonya pia wanasiasa kutokazania suala la muundo wa Muungano peke yake, bali waangalie na masuala mengine yaliyomo kwenye rasimu hiyo ambayo ni muhimu kwa Taifa.

No comments:

Post a Comment