Wednesday, February 12, 2014

AGIZO LA KUREJESHA MAGARI YA TOYOTA

prius22_b3ff7.jpg
Kampuni ya kutengeza magari ya Toyota nchini Japan, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni 1.9 aina ya Prius katika kiwanda cha magari hayo nchini Japan.
Hii ni kutokana na hitilafu ya kimitambo ambayo inaweza kusababisha gari hilo kukwama.
Gari la Prius ni moja ya magari yenye muundo unaonyesha ubunifu wa hali ya juu wa kampuni ya Toyota.
Gari hilo linaweza kutumia petroli na betri huku likitoa kiwango kidogo sana cha moshi kuliko magari ya kaiwada.
Sasa kampuni hiyo imetambua hitilafu ya programu ya gari hilo ambayo inaweza kusababisha vifaa vya elektroniki vya gari hilo kukwama.
Magari mengi yenye hitilafu hiyo yako nchini Japan na Amerika ya Kaskazini na Toyota inasema kuwa haijapokea taarifa zozote za ajali au majeraha kutokana na hitilafu hiyo

No comments:

Post a Comment