Wednesday, January 15, 2014

KANISA LA WALA NYASI LAIBUKA NCHINI!



KUNA mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi mbalimbali wa kiroho, moja wapo ni hili la kuanzishwa kanisa la wala nyasi nchini.
 Uchunguzi wa mabantanyau  umebaini kuwa kanisa hilo lipo maeneo ya Upanga jijini Dar na huduma yao inafanywa kwa kutumia jina la Rabboni Centre Ministries yenye makao yake makuu jijini Pretoria, Afrika Kusini.

mabantanyau tulifika Upanga, kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ndilo kanisa hilo lakini hakuna mtu aliyekutwa hapo.
Hata hivyo, baadhi ya majirani walisema huwa wanawaona watu wakiingia katika nyumba hiyo lakini ajabu kunakuwa hakuna kelele zozote.

No comments:

Post a Comment