Mashindano ya Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula yametambulishwa rasmi kwa wakazi wa jiji la Mwanza katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa..
Waandaaji wa mashindano hayo wakiambatana na Balozi wa kampeni ya Grow
Jacob Stephen maarufu kama JB pamoja na Jack Monroe ambaye ni Mwanawavuti kutoka nchini Uingereza walifika viwanjani hapo na kulakiwa na
umati wa watu waliokuja viwanjani hapo ili kufahamu zaidi kuhusu Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula.
Angalia picha za matukio yaliyojiri.........
|
Jack Monroe na JB |
|
"Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu, tusikate tamaa", alisema JB. |
|
Huyu ni Khadija Liganga kutoka shirika lisilo la kiserikali la Kivulini la jijini Mwanza. Khadija amefanya kazi nzuri sana kama mshereheshaji wa shughuli hizi. |
|
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa. |
|
Kikundi cha Ngoma na michezo ya nyoka wakitumbuiza katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula jijini Mwanza. |
|
Eluka Kibona ambaye ni Meneja wa kampeni, ushawishi na utetezi kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hizo. |
|
Sharon Mariwa kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hiyo |
|
Teresa Yates, Mratibu wa kitengo cha Haki Jinsia kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hizo. |
|
Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwataka vijana kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuchangamkia fomu za Maisha Plus.. Milioni 25 itatolewa kwa mshindi.. |
|
Baadhi ya wakina mama waliojitokeza kushiriki shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakipokea fomu kutoka kwa Balozi wa Grow JB. |
|
Baadhi ya vijana wakipokea fomu za ushiriki wa shindano la Maisha Plus kutoka kwa mwanawavuti Jack Monroe. |
|
Kutana na Francis Bonda, mojawapo wa waandaaji na wasimamizi wa Mashindano ya Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula. |
|
Kutana na Jack Monroe, mwanawavuti wa masuala yanayohusu chakula wa www.agirlcalledjack.comkutoka nchini Uingereza. Jack ambaye yuko nchini kwa mwaliko kutoka Oxfam in Tanzania atapata fursa ya kutembelea pamoja na kuandika kuhusu mafanikio pamoja na changamoto wanazokutana nazo wakulima kutoka Tanzania. Akiwa nchini, Jack atakutana na wanachama wa kikundi cha wakulima wa mpunga Ngaya mkoani Shinyanga pamoja na kukutana na washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula waliopita. |
|
Kutana na Mkamiti Mgawe, Afisa wa utetezi na ushawishi kutoka Oxfam. Mkamiti ametoa wito kwa wakina mama wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakazi wa Tanzania, kuchukua fomu na kushiriki mashindano haya. Fomu za ushiriki zinaweza kujazwa moja kwa moja kupitia link hii --> http://maishaplus.tv/MamaShujaaFomu2014.html
|
No comments:
Post a Comment