Friday, January 10, 2014

MUDA WA KUKAMILIKA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI

MUDA WA KUKAMILIKA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI WAONGEZWA


darajapx 048f2
Ujenzi wa Daraja la Kigamboni unatarajia kukamilika Julai mwakani badala ya Januari mwakani. 
Awali ilielezwa kuwa kazi hiyo ingekamilika Januari mwakani lakini changamoto walizokutana nazo wahandisi chini ya bahari zimesababisha ujenzi kuchelewa kukamilika.
Hayo yalibainika juzi wakati katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Mussa Iyombe, alipotembele ujenzi wa Daraja la Kigamboni lenye urefu wa wa mita 600 ili kujionea maendeleo yaliyofikiwa.
Katika eneo hilo, Mhandisi Iyombe aliwakemea wananchi watatu walikuwa wakipinga kuondoka katika eneo hilo ili kupisha mradi huo kwa madai kuwa hawakufanyiwa tathmini ya uhakika kuhusu mali zao.
Akizungumzia tatizo hilo, alisema kwa sasa watu hao wameshafanyiwa tathimini na kwamba kilichobaki ni ripoti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,kukabidhiwa kwa kwa watu hao ili hatimaye, waweze kuondoka kwa hiyari.
Mhandisi Iyombe aliwaonya watu hao wasijaribu tena kutaka kuchelewesha mradi huo na kwamba vinginevyo Serikali itatumia nguvu kuwaondoa.
Alisema mbali na changamoto hizo, bado wakandarasi wamekuwa wakiendelea vizuri na kwamba kazi iliyofanyika inatoa matumaini kwa Watanzania.

No comments:

Post a Comment