Monday, January 27, 2014

Waziri anusurika ajali ya ndege


Ndege ya Shirika la Ndege la ZanAir iliyopata ajali jana Mkoa wa Kusini Pemba. Na Mpigapicha Wetu.Zanzibar. Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakari Khamis Bakar, abiria na marubani wawili wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata ajali.Waziri Bakar pamoja na abiria wapatao 17 walipata ajali hiyo kisiwani Pemba jana baada ya breki za ndege hiyo ya Shirika la Ndege la ‘ZANZ AIR’ kushindwa kufanya kazi, muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, nje kidogo ya Mji wa Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

No comments:

Post a Comment