Wednesday, January 22, 2014

TUHUMA ZA KUJIUZA ZAMTOKEA PUANI BABY MADAHA,ANYANG'ANYWA GARI,MKATABA WASITISHWA



Madaha katika pozi
Stori: Mwandishi Wetu
Jambo limezua jambo! Ile skandali ya kunaswa baada ya kuingia mkenge kwenye mtego wa kujiuza imemtokea puani staa wa sinema na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ambaye amekiri kuumbuka.
Habari hiyo iliruka hewani kwenye gazeti dada la hili, Ijumaa wiki iliyopita toleo namba 862 la Januari 17 hadi 23 likiwa na kichwa cha habari ‘BABY MADAHA ANASA MTEGO WA KUJIUZA.
SAFARINI 
Ilielezwa kuwa wakati skendo hiyo ikiingia mitaani, mwanadada huyo alikuwa safarini kuelekea Nairobi, Kenya ambako ndiko yaliko Makao Makuu ya Kampuni ya Candy n Candy iliyompa mkataba mnono wa takribani Sh. milioni 200 ili wasambaze na kuuza kazi za Baby Madaha.
MAPOKEZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini nchini humo, imezoeleka kuwa kila Baby Madaha anapotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi kwa ajili ya kazi za kampuni hupokelewa na timu maalum kisha kuchukuliwa na lile gari la bei mbaya aina ya Audi TT.

Ilielezwa kuwa baada ya habari ya kunaswa kwake kusambaa, alipotua uwanjani hapo hakukuwa na mtu aliyekwenda kumpokea kwa kile kilichoelezwa kuwa viongozi wa kampuni hiyo walichukizwa na jambo hilo.

Baby Madaha akiwa na meneja wake Joe Kariuki. 
“Unajua tatizo ni simu ambazo viongozi wa Candy n Candy wanapigiwa na vyombo vya habari kutaka kujua undani wa skendo hiyo,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
MITANDAO
 
“Pia mitandao nayo imechangia kuwashtua viongozi hao maana kila ‘blogi’ imekopi kutoka kwenye mtandao baba lao wa www.globalpublishers.info na kupesti kwao.”
NYUMBANI
 
Baada ya kugundua kuwa alitelekezwa uwanjani, Baby Madaha alifanya mpango wa kwenda kwenye nyumba ya kampuni hiyo ambayo huwa anaishi lakini huko nako alikutana na ‘mbwa mkali’. Aliambiwa uongozi umekataza yeye kutia maguu ndani ya nyumba hiyo.
Kiliendelea kutiririka kuwa wakati huo, tayari Mkurugenzi wa Candy n Candy, Joe Kairuki alishawasiliana na Baby Madaha ambaye alimwambia kuwa skendo hiyo haikuwa ya kweli bali ‘promo’ ya filamu yake mpya ya The Gal Bladder.
OFISINI
 
“Hata angejitetea vipi, wale jamaa walikuwa hawamwelewi kwani alikwenda hadi ofisini kwao lakini hawakutaka kumsikiliza hadi hapo baadaye.
“Wanacholalamikia ni kwamba Baby Madaha amechafua sura ya kampuni na wanaonekana wanafanya kazi na msanii anayejihusisha na ufuska,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
GARI
“Hata hilo gari la Audi TT atakuwa analisikia kwenye bomba. Alizoea kukatiza nalo mitaa hapa Nairobi lakini sasa matatuu (daladala) zinamhusu.”
MSIKIE
 
Baada ya kujazwa data hizo, gazeti hili lilimtafuta Baby Madaha ambaye mwanzoni alikataa kutoa ushirikiano kwa kigezo kwamba ameharibiwa maisha.
Risasi: Baby lakini ni vizuri ukawa muwazi kuliko kuwa mkali. Je, ni kweli Candy n Candy wamevunja mkataba na wewe?
Baby: (kilio) Nasema niacheni kwanza mimi siyo msemaji wa Candy n Candy, mtafuteni mkurugenzi.
Alipomaliza kusema kwa hasira, Baby alikata simu.
MKURUGENZI
 
Hata hivyo, alipotafutwa mkurugenzi huyo, Joe alikuwa na haya ya kusema:
“Yaa tumeingia kwenye matatizo kwa sababu ya hiyo habari.”
Risasi: Matatizo gani?
Joe: Tumepigiwa sana simu na vyombo vya habari kuthibitisha hiyo skendo. Tunaonekana tunafanya kazi na mtu ambaye siyo. Anatuharibia image (sura) ya kampuni.
Risasi: Kwa yeye (Baby Madaha) amewaambiaje?
Joe: Anasema ni mambo yake ya filamu, kimsingi hatujamuelewa ndiyo maana hatujampa muda wa kumsikiliza kiundani.
Risasi: Kwa hiyo mtavunja mkataba wake na ninyi?
Joe: Ndiyo lengo letu lakini siyo jambo la haraka kwani kuna masuala ya kisheria.
Risasi: Vipi kuhusu gari na nyumba mlivyomkabidhi?
Joe: Kwa sasa kila kitu kipo chini ya kampuni.
Risasi: Nini hatima yake (Baby Madaha) sasa?
Joe: Yeye ndiye mumuulize nini hatima yake.
BABY MADAHA TENA
 
Baada ya mazungumzo hayo, gazeti hili lilimrudia Baby Madaha ambapo safari hii alikuwa mpole: “(kilio cha kwikwi) jamani nimeumbuka. Yaani huku wameichukulia kuwa ishu kubwa sana.”
Risasi: Sasa nini hatima yako?
Baby Madaha: Mi nipo Nairobi najaribu kuweka mambo sawa. Namwamini Mungu, najua atanijalia haja ya moyo wangu.
AMEFIKAJE HAPA?
 
Baby Madaha aliingia mkataba na kampuni hiyo mwaka jana ambapo mpaka sasa amesharekodi nyimbo mbili za Squeeze na Summer Holiday huku akirekodi filamu moja ya The Gal Bladder iliyozinduliwa hivi karibuni, jijini Dar.

No comments:

Post a Comment