TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Paul Mhangilwa Masanja kuwa Kamishna wa Madini nchini. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue mjini Dar Es salaam leo, Ijumaa, Januari 17, 2014, imesema kuwa uteuzi huo wa Bwana Masanja ulianza jana, Januari 16, 2014. Taarifa hiyo imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Masanja alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Januari, 2014
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Januari, 2014
No comments:
Post a Comment