Jana ndio ilikua siku ya Kalapina kupigana ulingoni, unajua nini kilitokea?
Yaweza kuwa ni nafasi ya wasanii wa Tanzania kujaribu upande wa pili wa maisha yao kwenye utafutaji pesa manake msanii Kalapina toka block41 Kinondoni Kikosi cha Mizinga ameamua kuangalia upande wa pili ambao ni masumbwi a.k.a ngumi za kulipwa.
December 31 mkesha wa kuukaribisha mwaka 2014 umeingia kwenye headlines upande wa Kalapina baada ya mpinzani aliyekuwa apigane nae usiku huo kutotokea kwenye pambano hilo na kufanya millardayo.com kufanya interview na Kalapina baada ya kushuka jukwaani ili kujua imekuaje.
Kalapina anasema ‘mpinzani wangu alikuwepo na alipima siku ile lakini nafikiri jina limemtisha na historia yangu ya mtaa imemtisha ameogopa na kweli leo ningefanya mambo makubwa kwenye ulimwengu wa ngumi, ningeacha historia nilijiandaa huyu mtu aondoke na machela’
‘kama nilivyotangaza pale mapromota mi nipo tayari sasa hivi nipo tayari kufa nipo tayari kupambana mi nimeingia kwenye ngumi rasmi sasa hivi, kupigana ni sehemu ya maisha yangu na bondia atakayejitokeza kupigana na mimi nitampigia saluti’ – Kalapina
‘Taarifa ya kutokuwepo mpinzani wangu kwenye mpambano sikuwa nayo mapema hadi napanda pale jukwaani nilikuwa na uhakika mpinzani wangu yupo na tunapigana, mimi sibipiwi ukinibipu nakupigia…… taarifa hii imfikie’ – Kalapina
‘Kwa sasa hivi namtaka Japhet Kaseba namtaka na Mchumia Tumbo maana wanaongeaongea sana hawa, kama Mchumia Tumbo anajifanya hana. mpinzani wakati wapinzani tupo’.
Kwenye hili pambano la Kalapina alitakiwa kuzichapa na Bahati Mwafiyale ambae aliitwa mara kumi na hakutokea jukwaani hivyo Kalapina akapewa ushindi aisee.
No comments:
Post a Comment