Saturday, January 18, 2014

CHELSEA vs MANCHESTER UNITED, REFA NI PHIL DOWD HUKO STAMFORD BRIDGE


Kocha wa Man United David Moyes amethibitisha kuwa Man United itawakosa Mastraika wake wakubwa, Wayne Rooney na Robin van Persie, ambao bado kuwa fiti baada kukabiliwa maumivu kwa Wiki kadhaa sasa.

Man United wana rekodi nzuri kwa Mechi za Ugenini wakiwa wamefungwa Mechi moja tu, ile ya Captal One Cup na Sunderland, Sare moja na kushinda zilizobaki. 
Kesho Jumapili, Manchester United wanasafiri kwenda Stamford Bridge kucheza na Chelsea na kabla Mechi hiyo kuanza, wanaweza kujikuta wako Pointi 14 nyuma ya Arsenal ambao wanacheza Jumamosi na Fulham Uwanja wa Emirates. 
Kwenye Mechi na Chelsea, Man United itawakosa Mastraika wao wakubwa, Van Persie na Wayne Rooney, ambao ni Majeruhi. 
Van Persie hajaichezea Man United tangu Desemba 10 walipocheza Mechi ya UCL na kuifunga Shakhtar Donetsk Bao 1-0.Rooney na Van Persie wakifanya mazoezi
Mchezaji wa Man United, Wayne Rooney ambaye pia ataukosa mtanange wa kesho jumapili huko Darajani Chelsea
Nae Robin van Persie nae majanga atakuwa nje!
Rooney mpaka sasa yupo nje tangu mwaka mpya alipocheza na Tottenham huko Old Trafford
Jembe!: Marouane Fellaini jana ijumaa alijifua kwenye mazoezi na kesho anatarajiwa kucheza mtanange huo wa kukata na shoka na Chelsea huko Stamford BridgeDanny Welbeck ndani..
Phil Jonesnae atakuwepo kwenye kikosi hicho cha kukwaana na Chelsea kesho saa 1:00 usiku

No comments:

Post a Comment