MWENYEKITI Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, ameshangazwa na hatua ya moja ya kampuni kutoka nje ya nchi, kuuza sehemu ya vitalu vya gesi walivyopewa. Kutokana na hali hiyo, amewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanasimamia ukweli badala ya kutawaliwa na mawazo ya mtu mmoja kuhusu hatua ya nani mwenye haki miliki ya vitalu vya gesi. Akizungumza Dar es Salaam juzi, aliwaomba viongozi hao wa dini kusikiliza maoni ya wadau wote wa Serikali, sekta binafsi na wananchi wengine kwa ujumla, ili kujua hali ya sekta ya gesi nchini na kujua nini cha kushauri.
“Mfano wa karibu ni kampuni ya nje ambayo imeuza sehemu ya vitalu walivyopewa na kupata zaidi ya dola bilioni moja. Inawezekanaje mwekezaji wa nje apewe vitalu na auze sehemu ya vitalu hivyo ili kupata fedha ya kuendeleza vitalu vinavyobaki, lakini inaonekana ni dhambi kwa wawekezaji wazawa kufanya hivyo.
“Mfano wa karibu ni kampuni ya nje ambayo imeuza sehemu ya vitalu walivyopewa na kupata zaidi ya dola bilioni moja. Inawezekanaje mwekezaji wa nje apewe vitalu na auze sehemu ya vitalu hivyo ili kupata fedha ya kuendeleza vitalu vinavyobaki, lakini inaonekana ni dhambi kwa wawekezaji wazawa kufanya hivyo.
“Nina imani viongozi wa dini zote watasikia ombi langu kwa niaba ya Watanzania wenzangu. Nina imani wataliangalia kwa undani na kwa umakini, kwa kuwa gesi asilia ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo inapaswa kuwanufaisha Watanzania wote wakubwa kwa wadogo, masikini na matajiri,” alisema.
“Ni vizuri ikaeleweka kwamba, kinachopiganiwa si TPSF kuchukua nafasi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), wala hakuna mzawa anayetaka kumiliki kitalu cha gesi peke yake. Sekta binafsi inataka Watanzania wote, mmoja mmoja au vikundi wamiliki uchumi wa gesi,” aliongeza Mengi.
“Kwa vile Wizara ya Nishati na Madini imeamua kuitisha vikao kinyume cha mapendekezo hayo, tunashauri viongozi wa dini wawasikilize, lakini pia watafute nafasi kama hiyo kuisikiliza Taasisi ya Sekta Binafsi na wadau wengine ambao hawajashirikishwa kwenye mikutano hiyo.”
Alisema viongozi wa dini ni watu wenye heshima kubwa kwenye jamii na wanaoaminiwa, hivyo wakiujua ukweli kuhusu uchumi wa gesi watashauri vema na kuwaeleza waumini hali halisi kuhusu sekta hiyo.
Mwenyekiti huyo wa IPP, alisema uhuru kamili kwa Watanzania wengi maskini utakamilika pale watakapoweza kujitawala kiuchumi na kwamba uchumi wa gesi ni mkombozi wa kufanikisha uhuru huo.
“TPSF ilifarijika na mafanikio yaliyoonekana wakati wa kikao cha Baraza la Taifa la Biashara kilichoendeshwa chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, ambacho kiliamua uwepo wa kamati ya kuchambua na kupeleka mapendekezo yake ya namna ya kuwawezesha kikamilifu Watanzania kushiriki uchumi wa gesi, lakini katika hali ya kushangaza, Wizara ya Nishati na Madini, imekuwa ikiitisha vikao na wadau mbalimbali kujadili jambo hilo,” alisema.
No comments:
Post a Comment