Saturday, January 18, 2014

KUNA UWEZEKANO MKUBWA KESHO KUTANGAZWA MAWAZIRI


Zipo taarifa  kuwa  Ikulu kesho  imetoa  mwaliko kwa wanahabari nchini na  yawezekano wito huo ukaenda sanjari na  kutangaza  mawaziri  walioteuliwa  kuziba nafari  za  mawaziri  wanne  waliotenguliwa  nafasi  zao na ile  ya  aliyekuwa  waziri  wa  fedha  marehemu Dr Wiliam Mgimwa  ama  yawezekana  wito huo ukawa wa  tofauti na hayo  kwani  yote  yanawezekana  ila  tuombe tufike  salama kesho jumapili
............................................
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Balozi Ombeni Y. Sefue ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, kesho, Jumapili, Januari 19, 2014, saa 5 asubuhi atazungumza na waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
 DAR ES SALAAM. 
18 Januari, 2014

No comments:

Post a Comment