Sunday, January 19, 2014

HAYA NDIO MATOKEO YA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CHAMA MAARUFU CHA UPINZANI NCHINI JANA



Habari zilizotufikia muda si mrefu zinathibitisha kwamba Mkutano Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi umemchagua tena James Mbatia(Pichani) kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi kingine cha kuanzia Januari 2014-2019.

Katika uchaguzi huo, Mbatia alikuwa akichuana kwa mbali na aliyekuwa Kamishna wa chama hicho mkoa wa Katavi Charles Makofila na mpaka mwisho Mbatia ameshinda kwa kura 201 huku Makofila akiambulia kura 26 na kura moja ikiharibika.

Wajumbe waliohudhuria mkutano huo walikuwa  228 kati ya 289.

No comments:

Post a Comment