Wednesday, January 29, 2014

JENGO LA JMC LILIVYONUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO


Jengo la JMC likiwaka moto.
Wananchi wakishuhudia moto huo.
Magari ya zimamoto yakiwasili eneo la tukio kutoa msaada.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakipambana na moto huo.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Askari wakidumisha ulinzi eneo la tukio.
Askari akiwasili eneo hilo eneo hilo akiwa na mbwa.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vinywaji ya Bavaria wakishuhudia jengo lililo jirani nao la JMC likiungua.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kulia) akipata maelezo ya awali kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi.
Wafanyakazi kutoka Kampuni ya Ultimate Security wakiwa eneo hilo kuongeza nguvu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akiongea na wananchi eneo la tukio.
Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi wakiwa eneo la tukio.

JENGO la JMC linalomilikiwa na Zhihir Shivji lililopo eneo la Kamata mtaa wa Kasanga, Kiriakoo jijini Dar es Salaam leo majira ya saa nane mchana lilinusurika kuteketea kwa moto ulioanzia ghorofa ya saba.

Chanzo cha moto huo na mali zilizoteketea mpaka sasa bado havijafahamika.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alifika eneo la tukio na kuagiza wamiliki wa majengo kuweka vyombo vya kutambua hitilafu mbalimbali kwenye majengo yao.

WAZIRI MKUU WA FINLAND APOKEWA RASMI NA KUFANYA MAZUNGUMZO IKULU NA RAIS KIKWETE


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu waFinland Jyrki Katainen wakipokea heshima katika jukwaa wakati wa mapokezi rasmi yaliyofanyika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen akiikwetkagua gwaride la heshima liliandaliwa na jeshi la wananchi wa Tanzania wakati wa mapokezi rasmi yaliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimuongoza mgeni wake Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen kukagua ngoma za utamaduni katika viwanja vya ikulu.  
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen wakikutana kwa faragha ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na mgeni wake Waziri mkuu wa Finland Jyrki Katainen ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen mara baada ya kufanya mazungumzo rasmi ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Waziri Mkuu huyo yupo nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili(picha na Freddy Maro)

WAZIRI ANUSURIKA KIFO


Mh. Juma Ngasongwa amenusurika kifo katika ajali iliyo tokea jana jioni Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani.   Pichani anaonekana Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Dr. Loti Kiwelu akimjulia hali katika Hospitali ya Tumbi Kibaha alipo fikishwa kwa ajili ya huduma ya kwanza ambapo alihamishiwa katika Hosipitali ya Muhimbili MOI kwa ajili ya matibabu zaidi. (picha na Chris Mfinanga).   Ajali hiyo ilihusisha gari  aina ya Rav 4 mali ya Mh. Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam kuelekea morogoro ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Tanesco. ..

Monday, January 27, 2014

RAIS KIKWETE AALIKWA NIGERIA NA RAIS JONATHAN


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako  walikuwa wakihudhuria  Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, DKT. ASHA- ROSE MIGIRO ATEMBELEA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) akipokea nakala za ripoti za Tume
ya Mabadiliko ya Katiba ikiwemo Rasimu ya Katiba kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji
Joseph Warioba wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Tume
hiyo aliyoifanya mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Saalam.Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) akimpokea Waziri wa

Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) wakati alipowasili katika Ofisi za Tume hiyo

kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Ofisi hiyo katika ziara yake aliyoifanya mwishoni

Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) wakati alipowasili katika Ofisi za Tume hiyo
kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Ofisi hiyo katika ziara yake aliyoifanya mwishoni

Waziri anusurika ajali ya ndege


Ndege ya Shirika la Ndege la ZanAir iliyopata ajali jana Mkoa wa Kusini Pemba. Na Mpigapicha Wetu.Zanzibar. Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakari Khamis Bakar, abiria na marubani wawili wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata ajali.Waziri Bakar pamoja na abiria wapatao 17 walipata ajali hiyo kisiwani Pemba jana baada ya breki za ndege hiyo ya Shirika la Ndege la ‘ZANZ AIR’ kushindwa kufanya kazi, muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, nje kidogo ya Mji wa Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Thursday, January 23, 2014

HATIMAYE ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE AFIKISHWA KIJIJINI KWAO.


Sasa tunaingia kijijini kwao Chiwanda 


Ads by Video PlayerAd Options
Tupo kijijini kwao Chiwanda na kupokelewa na mamia ya wakazi wa hapo.

Mama wanne akishuka katika gari kijijini kwao

Baba mzazi wa watoto mapacha wanne akiwa amefurahi kumpokea mkewe huku akiwa amembeba moja ya mapacha na kusema huyu ataitwa Joseph wa Mbeya yetu

Ads by Video PlayerAd Options
Ni furaha ilioje kijijini hapo tulipokwewa vizuri sana

Mtoto Claud akimpokea mama yake mzazi kwa furaha ya kupata wadogo zake wanne yaani wee acha tu


Ads by Video PlayerAd Options
Yaani kila mwana kijiji alitamani kuwashika watoto hao angalau apate baraka maana wakazi wa hapo wanasema neema imeingia kijijini kwao



Ads by Video PlayerAd Options

Hii ndiyo nyumba ya wazazi wa watoto mapacha wanne 

Ndani ya nyumba hiyo na ndiyo chakula chetu kitamu kinapikwa humu tulikula msosi wa nguvu wali wa kuku na zawadi ya maembe tukapewa mungu awabariki sana wanakijiji cha Chiwanda

Ads by Video PlayerAd Options

Hii ni nyumba mpya ambayo imejengwa kwa siku chache tu kwa ajaani wamezindua nyumba yao mpyaili ya mapokezi ya watoto mapacha wanne pesa kiasi walichotoa wasamaria wema baba mzazi wa watoto mapacha akaamua kununua bati na kuezeka nyumba hiyo yao na ndimo walipofikia mapacha hao 

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwanda, Ignas Sinkara mwenye shati la kitenge aliwapongeza waandishi hao kwa moyo walioonesha na kuwaomba kuendelea kujitolea hivyo hivyo katika majukumu mengine.

Joseph Mwaisango ambaye ni mmoja wa wakurugenzi  wa mtandao wa kijamii wa Mbeya yetu Blog







Picha ya pamoja kabla ya kuondoka kijijini hapo



Mwanamke Aida Nakawala(25) aliyejifungua watoto wanne kwa mkupuo  usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Wazazi ya Meta kwa ajili ya hifadhi ya chumba cha joto kwa watoto na huduma muhimu kwa mzazi amewasili kijijini kwao Chiwanda na kupokelewa na mamia ya wakazi wa hapo.
Mapokezi hayo yaliyofanyika jana, mara baada ya kuwasili nyumbani kwake kijijini hapo akitokea katika Hospitali ya Wazazi ya Meta alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo Wakazi hao walionekana kushangazwa na kitendo cha mama huyo kujifungua watoto wanne kwa mkupuo tena kwa njia ya kawaida.
Baadhi ya majirani waliokuwepo Nyumbani kwa Mwanamke huyo wakiongozwa na Serikali ya Kijiji, walisema wapo tayari kumpa msaada mama huyo shujaa wa hali na mali.
Hata hivyo wakati Wananchi wakionesha furaha na mishangao Serikali ya Kijiji pia imejipanga kuhakikisha inaisaidia Familia hiyo  ambayo haina uwezo kimaisha kutokana na baba wa Familia Webson Simkanga(28) kutegemea kilimo cha Mahindi huku akiwa na jumla ya  watoto Sita, kutunza watoto hao kwa kupanga mikakati mbali mbali ya muda mfupi na muda mrefu.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofanikisha Safari ya Mama huyo kutoka Hospitali ya Wazazi Meta hadi kijijini kwao umbali wa Kilomita zaidi ya 130, Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwanda, Ignas Sinkara aliwapongeza waandishi hao kwa moyo walioonesha na kuwaomba kuendelea kujitolea hivyo hivyo katika majukumu mengine.
Alisema moja ya michango iliyopatikana imesaidia huduma za mama alipokuwa Hospitali, kukarabati Nyumba atakayoishi baada ya kujifungua pamoja na kusaidia shughuli za Shamba kutokana na wazazi wote wawili kutakiwa kusaidiana katika kuwahudumia watoto hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mpumpi anapotokea Mama huyo, Winstoni Mtali, alisema mbali na juhudi zilizopangwa na serikali ya kijiji pamoja na wasamaria wema walionesha kuguswa na mama huyo tangu alipojifungua bado misaada zaidi inahitajika kutokana na mzigo huo kuwa mkubwa kwa Wanakijiji.
Alisema bado mazingira ya nyumbani kwa mwanamke huyo na kijiji kwa ujumla siyo rafiki kwa malezi ya watoto hao kutokana na nyumba yao kutokuwa katika mazingira mazuri hivyo kuhitajika michango ya hali na mali kwa ajili ya ukarabati wa nyumba hiyo ambayo inahitaji kusakafiwa, kupigwa dali, madirisha na kusakafia kuta ili watoto wasidhurike na vumbi la ndani
Waandishi waliojitolea kufanikisha safari ya Mwanamke huyo hadi kijijini kwao ni pamoja na Venance Matinya(JamboLeo), Ezekiel Kamanga(Bomba Fm Redio), Joseph Mwaisango ambaye ni mmoja wa wakurugenzi  wa mtandao wa kijamii wa Mbeya yetu