Wednesday, February 26, 2014

HUYU NDIE MZUNGU ALIYEKAMATWA NA KILO 5 ZA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR-ES-SALAAM




Raia wa Henellic, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.

Habari zinasema mzungu huyo alikamatwa wakati wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air kueleke jijini Zurich, Uswisi. Madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa yaupekuzi, kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.

Habari zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo akisubiri taratibu za kisheria ili afungukliwe mashtaka.

SUGU ASEMA "NIMEITULIZA MBEYA"

sugu_ea66c.png
Mbeya. Jimbo la Uchaguzi Mbeya Mjini linafahamika kwa rekodi yake ya kipekee.
Kwa muda mrefu lina rekodi ya kubadili wabunge kila baada ya miaka mitano. Hiyo imetokea kwa wabunge kama Polisya Mwaiseje (NCCR- Mageuzi), Benson Mpesya (CCM), miongoni mwa wengi.
Kwa sasa linashikiliwa na Joseph Mbilinyi 'Mr ll' au Sugu kutoka Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema )
.
Mr ll au Sugu ambaye kiumri ana miaka 42 aliupata ubunge huo kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2010.
Mbunge huyo ambaye pia ni msanii anaeleza mbinu alizofanya kulipata jimbo hilo, alichoahidi wakati wa uchaguzi, alivyotekelekeza na vikwazo anavyopata akiwa mbunge wa Mbeya Mjini, halmashauri ambayo inaongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, Chadema kupitia mimi katika Jimbo la Mbeya tuliahidi kurudisha madaraka kwa wananchi.
Uhuru wa biashara
Tulitaka wananchi wawe na uhuru wa kufanya biashara bila bughudha, vijana wafanye kazi kwa uhuru na mama lishe waheshimiwe,'' anasema Sugu jina ambalo amelipata kutokana na sanaa ya muziki wa kufokafoka.
Mbunge huyo anasema alilazimika kutoa ahadi hiyo kwa sababu wananchi kipindi hicho walikuwa wakikamatwa ovyo na polisi au mgambo na kusingiziwa kesi za uongo.
Anasema vijana wanaofanya biashara ndogondogo na mamalishe mitaani na wale wanaouza matunda walikuwa wakisumbuliwa na askari wa jiji na kwamba kipindi hicho wakazi wa Mbeya walikuwa na maisha ya wasiwasi.
''Hivyo mimi niliingia na hoja ya kuwatetea wanyonge, wakiwamo waosha magari, Wamachinga na wenye bajaj ambao walikuwa wakizuiwa wasiendeshe vyombo vyao mitaa ya mjini na Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Zambia,'' anasema.
Katika kutekeleza hilo, Mr ll anasema baada ya kupata ubunge, amesimama kidete kuwatetea wafanyabiashara, mamalishe na wauzaji matunda katika mitaa mbalimbali ili mradi hawavunji sheria za usafi wa mazingira
Sugu anasema pia aliwaahidi wananchi wa Mbeya kwamba akiwa mbunge atatetea kujengwa barabara za kisasa zinazoonyesha kwamba Mbeya ni jiji kweli na kwamba zisipopatikana atapigania Mbeya irudi kwenye manispaa ili kupunguza kero.
Anasema aliwaahidi wakazi wa Mbeya kwamba katika kipindi chake watamwita ''Bwana barabara'' kwa sababu barabara za mitaa, vitongozji na jiji zitaboreshwa.
Katika kutekeleza ahadi hiyo, Sugu anasema kitendo cha yeye kuwa mbunge kimechangia kwa kiasi kikubwa kutekelezwa kwa umakini wa ujenzi wa barabara kupitia mradi uliofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Anasema barabara za lami zenye urafu wa karibu kilometa 30 zimejengwa kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya wakati nazo barabara za mitaa, vitongoji vingi zimeboreshwa.
Pia, anasema mwaka 2010 aliahidi kupambana na rushwa kwa udi na uvumba kuboresha utendaji wa sekta za afya, ulinzi, elimu, umeme, na jiji lenyewe.
Katika kutekeleza hilo anasema alianza kazi kwenye Hospitali ya Rufaa Mbeya ambako baadhi ya wafanyakazi walikithiri kwa rushwa.
Anasema alishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuwakamata baadhi ya wafanyakazi wapenda rushwa kwenye hospitali hiyo.
Pia, anasema ametetea hospitali hiyo ipate magari ya kubeba wagonjwa, tayari gari limefika na lingine linakuja.
Anaongeza kuwa amekuwa akifuatilia kwa karibu polisi wapenda rushwa na hata wafanyakazi wa mahakama, Tanesco, na jiji anapopata malalamiko kutoka kwa wananchi wa Mbeya.
''Niliahidi kushirikiana na wananchi kuwasaidia wajane na watoto yatima, na nimewasaidia wajane kwa kuweka mazingira mazuri ya wao kuendelea kufanya biashara bila bughudha,'' anaeleza.
Hata hivyo, kwa upande wa yatima anasema amewasaidia kupitia Mfuko wa elimu aliouanzisha ambao unawasomesha watoto 200 katika shule mbalimbali za msingi na sekondari.
Watoto hao wanapata msaada wa sare za shule, wengine wanalipiwa ada na kupewa vifaa vya shule.
Pia, anashauri watoto yatima katika shule mbalimbai za Serikali wanaosoma kwa misaada wasamehewe michango mbalimbali ikiwamo ya ulinzi.
Mwakilishi huyo wa wapigakura wa Mbeya anasema pia kwamba aliahidi kujenga mabwawa ya samaki katika kila kata ili kuongeza vipato vya wananchi, lakini suala hilo limekwama kutokana na migogoro ya kisiasa.
Anaongeza kuwa katika kampeni zake za ubunge aliahidi kuizindua michezo kwa kuhakikisha wakazi wa Jiji la Mbeya wanapata burudani.
Anasema 'mizuka imezinduka' na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Jumaa Idd aliamua kuinunua timu mkoani Arusha na kuipa jina la Mbeya City.
''Nasisitiza timu ni ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya, siyo ya Sugu, Chadema wala CCM , lakini ukiona vinaelea ujue vimeundwa,'' anasema na kuongeza kuwa wananchi wa Mbeya ndiyo wamiliki wa timu.
Kuhusu wasanii anasema hajawapatia fedha, lakini amewasaidia katika kupigania haki za stika na kuzishauri redio zilizopo jijini Mbeya zipende kutumia nyimbo za wasanii wa Mbeya ili kuwatangaza.
Changamoto
Changamoto anazopata akiwa Mbunge wa Chadema kwenye Serikali ya CCM, Sugu anasema siasa siyo mchezo mchafu kama wahusika wote wanakuwa na nia moja ya kuongeza kasi ya maendeleo.
Hata hivyo anasema wapo wanasiasa wachache wanaoichafua siasa kwa kukwamisha miradi ya maendeleo ya wananchi kutokana na kwamba miradi hiyo inasimamiwa na upinzani.
Anaeleza kuwa Chadema ilibuni mradi wa kuhamasisha wananchi wa Jiji la Mbeya wawe na mabwawa ya samaki jambo ambalo pia linasisitizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, lakini madiwani wa CCM wamemkwamisha.
Anatoa mfano kwamba Kata ya Nsalaga ilichimba bwawa ambalo lingekuwa na samaki wenye thamani ya Sh14 milioni kila baada ya miezi mitatu, lakini madiwani wa CCM wamekwamisha.
Pia, anasema Serikali iliyopo madarakani haipendi kutekeleza miradi ya manufaa kwa wananchi na taifa kwenye majimbo ya upinzani.
Anatoa mfano wa Serikali kutojali kufufua viwanda vya nyama, mbolea, maziwa, sabuni, pembejeo vilivyokuwapo Mbeya.
Anashauri tabia hiyo ikome, la sivyo itaondolewa kwa nguvu za umma.
Anasema kwamba uchaguzi wa mwakani, 2015 ana uhakika kuchukua jimbo hilo tena na hatimaye madiwani wote kuwa wa Chadema na kuiongaza halmashauri ya jiji na kwamba hapo kasiya maendeleo ndipo itakapoonekana wazi.
Hadi sasa Jimbo la Mbeya lina kata 36 ambapo Chadema inashikilia kata 17 kati ya hizo()

OLYMPIACOS YAIBANA MANCHESTER UNITED

moyes_c04c7.jpg
Manchester united iliambulia kichapo cha mabao mawili kwa nunge dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki katika mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na ghamu na mashabiki wa ligi kuu ya Mabingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo iliyokuwa ikipigiwa upatu kuwa itakayosisimua muamko mpya wa vijana wa David Moyes ilikosa makali kabisa.
Manchester united ilikamilisha shambulizi moja pekee kunako dakika ya 89 ya kipindi cha pili Robin van Persie alipoishambulia lango la wenyeji wao huko Ugiriki.
Alejandro Dominguez alifunga bao la kwanza kunako dakika ya 38.
Kiungo wa Arsenal aliyeko Ugiriki kwa mkopo Joel Campbell akikamilisha kichapo hicho kunako dakika ya 54 ya kipindi cha pili.
Kutokana na ushindi huo mkubwa ,Mabingwa hao wa Ugiriki Olympiakos waliendeleza msururu wao mkubwa wa matokeo mazuri.
Olympiakos wameshinda mechi 24 kati ya 26 walizocheza hivi karibuni na kufikia sasa wanaongoza kwa zaidi ya pointi 20.
Manchester sasa inakabiliwa na mlima wa kupanda katika raundi ya pili sawa na timu zengine mbili za Uingereza , Manchester City na Arsenal ambazo pia zililazwa mabao mawili kwa nunge juma lililopita wapinzani wao.

Tuesday, February 25, 2014

Soma Tamko Lote la Mh:Nyalandu akiwatimua Vigogo Kadhaa Wizara ya Maliasili,Akiwemo Mkurugenzi wa Wanyama Pori


Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo: 
Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.  Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.  Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.
 
Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa.
 
Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.
 
Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori.
 
Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti.
 
Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) nakukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo.  Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1)  Malengo ya wizara, 2)  Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.  Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu.
 
Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara.  Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.  Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.
Mungu ibariki Tanzania.
Asante.

Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014

mastaa wa bongo wachambana mtandao wa Instagram




Mwigulu Nchemba alipuka,Anayeona Posho haitoshi afungashe Virago

‘Anayeona posho haimtoshi afungashe virago’

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.PICHA|MAKTABA 
Kwa ufupi
Hoja ya kutaka nyongeza ya posho iliibuliwa na wajumbe wawili ambao pia ni wabunge wa CCM, Richard Ndasa (Sumve) na Suleiman Nchambi (Kishapu).
Dodoma. Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.
Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi.
Madai ya wajumbe kutaka waongezewe posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho.
Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje.
Alisema kwa msingi huo, Serikali ilitarajia kuwaona watu hao wakitanguliza uzalendo zaidi badala ya kudai malipo manono.
“Katika kutengeneza Katiba hii, hatujakodi consultants (wataalamu washauri) kutoka Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda wala nchi nyingine yoyote… Hawa ni Watanzania na kazi wanayoifanya ni yao,” alisema.
“Wangekuwa wataalamu wa kukodi wangeweza kudai malipo hayo, lakini hapa ni tofauti... wanafanya kazi yao na kila mtu anafanya kazi yake na anapaswa kujivunia kushiriki katika tendo hili la kihistoria kwa kutanguliza uzalendo,” alisema.
Nchemba alisema anazielewa hoja za baadhi ya wajumbe walioibua suala la posho, lakini kwa mtazamo wake, hoja hiyo hata kama ingekuwa na mashiko kiasi gani, imewasilishwa wakati usiokuwa mwafaka. Alisema wapo makandarasi na wazabuni waliotoa huduma kwenye taasisi mbalimbali za umma lakini hawajalipwa.
Alisema kwa kawaida, Februari ni mwezi mbaya kwa kuwa baadhi ya wilaya zina historia ya kukumbwa na uhaba wa chakula hivyo kuhitaji fedha nyingi za Serikali ili kuokoa maisha ya watu katika maeneo hayo.
Pia alisema si wakati mwafaka wa kudai nyongeza hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kuna walimu wapya 30,000 nchini kote ambao hawajapangiwa vituo kutokana na kukosekana kwa fedha za kulipa stahiki zao.
Nchemba alisema mbali na walimu hao wapya kutokupangiwa vituo, walimu wengine wanadai malimbikizo ya fedha zao na kwamba hawajalipwa kutokana na ufinyu wa bajeti serikalini.
“Siku zote ukweli unauma. Nasema kama kuna mjumbe ambaye anaona huko alikokuwa kabla ya kuteuliwa alikuwa anapata pesa zaidi kuliko hii, basi kwa heshima afungashe virago na kuondoka,” alisema

Monday, February 24, 2014

ROONEY: FEDHA ANAYOINGIZA KWA WIKI INAZIDI MSHAHARA WA MWAKA MZIMA WA BARACK OBAMA

rooney 1ae1b
£160,000 - Hii ndio fedha ambayo itabaki kwenye akaunti ya Rooney kwa wiki - baada ya kulipia kila kitu, kodi na bima.
£30,000 - Wastani wa mshahara wa wiki kwa mchezaji wa ligi kuu ya England, hii ni kwa mujibu wa Deloitte's sports business group.
£517 - Huu ni wastani wa mshahara wa wiki wa mtu anayefanya kazi ndani ya UK. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anapata £2,740 kila wiki.
65 - Itamchukua wiki 65 kwa Barack Obama, raisi wa taifa kubwa duniani Marekani, kuweza kutengeneza kiasi anacholipwa Rooney ndani ya siku saba tu - Obama analipwa £240,000 kwa mwaka.
1885 - Huu ulikuwa mwaka wa kwanza kwa mwanasoka kuweza kulipwa kutokana na kucheza soka.
£4 - Hiki ndio kilikuwa kiwango cha juu kabisa cha malipo katika Football League mwaka 1901.
60 - Namba ya miaka iliyotumika mpaka kufikia mwisho wa sheria ya kulipwa kiasi kisichozidi paundi 4 kwa mwanasoka. Sheria hii ilikufa mwaka 1961. Muda mfupi baada ya kufutwa kwa sheria hii, mchezaji wa Fulham na Engand Johnny Haynes alikuwa mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi cha £100 kwa wiki.
£1,200 - Kiasi ambacho golikipa Peter Shilton alitengeneza kila wiki mwaka 1979 wakati alipoweka rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi Uingereza kwa kusaini mkataba mpya na Nottingham Forest.
£10,000 - Mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi cha tarakimu 5 alikuwa Chris Sutton, wakati mshambuliaji huyo alipojiunga na Blackburn Rovers akitokea Norwich City mnamo 1994.
£100,000 - Sol Campbell aliondoka Tottenham na kujiunga na Arsenal mnamo mwaka 2001, akasaini mkataba ambao ulimfanya kuwa muingereza wa kwanza kulipwa mshahara wenye tarakimu 6 kila wiki

Hatimaye Hati yatolewa Rais wa Ukraine anatafutwa Akamatwe


Rais wa Ukraine aliyeondolewa madarakani Victor Yanukovych amefunguliwa mashtaka
Ukraine imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani, Victor Yanukovych, Waziri wa mambo ya ndani wa mpito ametangaza hatua hiyo.
Arsen Avakov amesema katika ukurasa wa Facebook amesema kesi dhidi yake imefunguliwa dhidi ya Yanukovych na maafisa wengine kuhusu mauaji ya makubwa ya watu.
Wabunge walipiga kura kumuondoa Yanukovych siku ya jumamosi baada ya maandamano ya miezi kadhaa yaliyojitokeza baada ya kupinga kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Machafuko yaliyotokana na maandamano hayo yalisababisha watu kadhaa kupoteza maisha juma lililopita.
Avakov amesema Yanukovych alionekana mjini Balaklava siku ya jumapili, lakini mpaka sasa hajulikani mahali alipo.

Breaking Newz,Milipuko Miwili Zanzibar Tukio Zima hili hapa


Mji wa Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamethibitisha kutokea milipuko mitatu ya mabomu kati ya Jumapili na Jumatatu leo mchana visiwani humo.
Akizungumza na 
mwandishi wetu Erick David Nampesya, mkuu wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame amesema milipuko miwili imetokea leo katika eneo la mgahawa wa Mercury huku mlipuko mwingine ukiwa umetokea katika eneo la Mkunazini, ikifuatia mlipuko uliotokea jana Jumapili katika eneo la Pangawe.
Mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa hakuna vifo wala majeruhi katika matukio yote matatu wala mali iliyoharibiwa, isipokuwa madhara ya kisaikolojia kutokana na hofu na taharuki kutokana na matukio hayo.
Aidha mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa upelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika matukio hayo ingawa hadi wakati huu hakuna mtu au mshukiwa yeyote aliyekwishamatwa kuhusiana na matukio hayo.
Kuhusu hatua za tahadhari kufuatia matukio hayo Kamanda Makame amesema Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi katika sehemu mbali mbali visiwani humo ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika maeneo kadhaa na amewaondoa hofu wananchi wa visiwa hivyo kuhusu usalama wao.

Rais Yoweri Kaguta Mseveni ala Sahani Moja na Mashoga,Leo amesain Muswada na Kuwa Sheria


Moses mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja atafuta hifadhi nchini Marekani
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na wandishi wa habari. 
Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya 
kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza, 
Adhabu ya maisha jela itatolea kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.
Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi. 
Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.

Thursday, February 20, 2014

Facebook yasema itainunua WhatsApp

Facebook na WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana.
Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.

BAADA YA KUANDAMWA NA MENGI IKIWEMO KUNASWA AKIJIUZA ...BABY MADAHA ATANGAZA KUACHA MUZIKI NA FILAMU




IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego wa kujiuza na makachero wa OFM ya Global Publishers, staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na maisha ya presha. Akistorisha na paparazi wetu juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.

Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.
“Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.

Hivi karibuni Madaha aliingia kwenye kumi na nane za Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ambapo alipatana bei ya kutoa uroda kwa ‘mfanyabiasha’ wa madini kutoka jijini Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Mike – kumbe ulikuwa mtego.

Wednesday, February 19, 2014

TMA Yatoa Tahadhari ya Mvua Kubwa Kunyesha

Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya mitaa ilivyo jaa maji kutokana mvua kubwa kunyesha juzi jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya mitaa ilivyo jaa maji kutokana mvua kubwa kunyesha juzi jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya nchi ambayo huwenda ikaleta madhara. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Ofisa Uhusiano wa TMA, Monica Mutoni maeneo ambayo yanaweza kuathiriwa na mvua hizo ni pamoja na mikoa ya Singida na Dodoma, Iringa, Mbeya na Njombe na Mikoa ya Ruvuma na Morogoro.
Alisema kwa mujibu wa vipimo, mvua hizo za zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24 zinatarajia kunyesha kuanzia Februari 19 hadi 21, 2014 hivyo TMA imewataka wananchi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari juu ya madhara yoyote yanayoweza kusababishwa na mvua hizo kwa maeneo tajwa.
Taarifa imefafanua kuwa hali hiyo imesababishwa na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika rasi ya Msumbiji, kitendo kitakachosababisha kuvuta upepo kutoka misitu ya Congo kupitia maeneo tajwa hivyo kukubwa na mvua hizo.
“…Idara zinazohusika na hali ya tahadhari pamoja na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari. Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi,” ilisema taarifa hiyo ya TMA.

CCM Yawaadhibu Lowassa, Sumaye, Membe na Wassira…!

Walioadhibiwa ni waliokuwa mawaziri wakuu, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye,  mawaziri Benard Membe, Stephen Wassira na Naibu Waziri, January Makamba pamoja na aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Walioadhibiwa ni waliokuwa mawaziri wakuu, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, mawaziri Benard Membe, Stephen Wassira na Naibu Waziri, January Makamba pamoja na aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Na Joachim Mushi
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) hatimaye kimeanza kuchukua hatua kwa wanachama wake 6 nguli walioonekana kuanza kampeni za kugombea urais ndani ya chama hicho mapema kabla ya muda kutangazwa. Walioadhibiwa ni pamoja na waliokuwa mawaziri wakuu, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, mawaziri Benard Membe, Stephen Wassira na Naibu Waziri, January Makamba pamoja na aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari toka CCM na kusainiwa na Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi NEC Taifa, Nape Nnauye alisema makada wote 6 wa CCM waliohojiwa wamekutwa na makosa hivyo kupewa adhabu ya onyo na chama. Alisema makada hao 6 wa CCM pia watakuwa chini ya uchunguzi wa mwaka mmoja wakiangaliwa mwenendo wao ili kujirekebisha.
Vigogo hao wa CCM, Edward Lowasa, Frederick Sumaye, Bernard Membe, Stephen Wassira, January Makamba na William Ngeleja walihojiwa na sekretarieti ya CCM mjini Dodoma kabla ya kubainika na makosa, kabla ya Tume ya Udhibiti na Nidhamu kuwajadili na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu hiyo kwa wahusika.
Nape alisema baada ya kuhojiwa wote walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati jambo ambalo ni kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
“…Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii. Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo,” alisema Nnauye.
“Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya onyo kali na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi. Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni; “Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.” Ilieleza taarifa ya Nnauye.
Aidha alifafanua kuwa Kamati Kuu imeitaka Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuwa mawakala na wapambe walioshirikiana na makada hao walioadhibiwa nao kuchukuliwa hatua.
“…Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu za Chama.”

RAIS YOWERI MUSEVEN ASAINI SHERIA YA KUPIGA MARUFUKU UUVAJI WA NGUO FUPI MAARUFU KAMA VIMINI.

Screen Shot 2014-02-19 at 8.27.49 AM 

Taarifa ikufikie kwamba imepigwa marufuku kwa jinsia ya kike kuvaa nguo fupi (ki-mini) nchini Uganda na tayari Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni amesaini rasmi sheria hii.


Japokua baadhi ya Wabunge walipinga kwamba marufuku hii inaingilia uhuru wa mtu kuvaa, wabunge wengi wameunga mkono uamuzi huu.


Unaambiwa marufuku hii ambayo imelenga kuepusha vitendo vya ubakaji na ngono zembe kutokana na ushawishi unaotokana na uvaaji huu, inahusisha pia nguo nyingine fupi ambazo zinaacha sehemu kubwa ya mwili wazi kama vile kifuani.


Wanawake/Wasichana wataruhusiwa kuvaa mavazi mafupi kwenye matukio maalum tu yanayohusisha uvaaji huu kama vile michezo ambapo Waziri husika 
Screen Shot 2014-02-19 at 8.03.41 AM

Screen Shot 2014-02-19 at 8.28.49 AM 
Sheria hii pia inawabana Wanamuziki wa kike ambao wamekua wakivaa nguo fupi kwenye show zao pamoja na video ambapo Waziri Lokodo amesema ‘hatutaki uhusike kufanya watu wakutamani au watamani kufanya ngono, hatutaki ushawishi chochote kwa jinsia ya kiume, kuwa na tabia njema kwa kuvaa kiheshima’

Screen Shot 2014-02-19 at 8.26.31 AMVilevile vyombo vya habari yakiwemo Magazeti na TV, vimepigwa marufuku kuonyesha picha za watu wakipigana busu au picha zozote za Wanawake wakiwa nusu uchi

MSAMALIA MWEMA KUTOKA UINGEREZA ATUMA MISAADA KWA MZAZI WA MAPACHA WA NNE MKOANI MBEYA



Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya. 
 Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza. 
 Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo. 
 Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia. 
 Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na issamichuzi@gmail.com ama j.mwaisango@tonemg.com nasi tutafikisha ubani wako. 
 Muhidin Issa Michuzi 


Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.



mbeya

TUZO ZA KILI ZAZINDULIWA RASMI

kili_bf22f.jpg
Dar es Salaam. Tuzo za Muziki, maarufu 'Kilimanjaro Music Award' zimezinduliwa rasmi jana na zitafikia kilele chake Mei 3 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zinaratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kushirikiana na TBL kupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro.
Mratibu wa Tuzo hizo kwa upande wa Basata, Kurwijira Ng'oko alisema mwaka huu wameboresha zaidi tuzo hizo, ambapo hivi sasa wanataka muziki uwe ni ajira rasmi kwa hiyo msanii ambaye atapendekezwa katika vipengele vya tuzo hizo kama hajasajiliwa Basata hataruhusiwa kushiriki.
Ng'oko alisema pia tuzo ya mtayarishaji chipukizi wa mwaka haitakuwapo kwa vile watayarishaji ni wale wale kila mwaka na hivyo kufanya tuzo kujirudia.
Naye meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wa tuzo hizo, George Kavishe alisema kuwa Watanzania ndio watakaoteua msanii atakayeingia kwenye mchakato wa kinyang'anyiro cha tuzo hizo kwa kutoa mapendekezo yao kwa njia ya simu au mitandao ya kijamii

CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA RAIS KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa kuomba radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo suala hilo litafikishwa jumuiya za kimataifa.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo Chadema wanaitafsiri kama kielelezo cha kuvuruga amani ndani ya nchi.
Kwa majibu CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamwe hawatafanya hivyo.
"Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na kutokana na vitendo vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema kuvuruga amani nchini," alisema na kuongeza kuwa dawa ya moto ni moto.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kufuta alichokizungumza ndani ya siku tatu kuanzia jana, vinginevyo watalifikisha suala hilo mbele ya jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya malalamiko yao.
Alisema kuwa Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu, na alihoji kwanini awatake WanaCCM kujibu mapigo dhidi ya wapinzani badala ya kuacha hatua za kisheria zikafuatwa kwa kutumia vyombo husika ambavyo ni polisi na majeshi na mahakama.

Tuesday, February 18, 2014

UNAFAHAMU KUWA WEMA SEPETU NA MANAIKI SANGA NI WAPENZI?




Mastaa wa filamu, Manaiki Sanga na Wema Sepetu wanadaiwa kuwa wapenzi. Habari ni kuwa wasanii hao walianza kama marafiki wa kawaida na baadaye Manaiki kurusha kete yake kwa Wema Sepetu...

Kwasasa wawili hao inasemekana wapo karibu sana kiasi cha kuzua minong'ono kwa wafuatiliaji wa habari za mastaa nchini.

"Manaiki Sanga amemnasa Wema katika himaya yake, wapo karibu sana siku hizi hata marafiki zao(wa Wema na Manaiki) wanajua kuwa wanatoka pamoja, si wajua Manaiki ni playboy na akiamua kumpata girl yeyote yule hashindwi??" kilisema chanzo hicho ambacho pia ni msanii wa filamu nchini

Naye Manaiki Sanga ambaye siku za hivi karibuni alikumbwa na skendo ya kutembea na kupiga picha chafu na wasichana kibao alipotafutwa na kuulizwa kuhusu kuwa katika mapenzi na Wema Sepetu alijibu kwa ufupi kwa kusema "ni wazushi".

Manaiki alipoulizwa tena kama ukaribu wake na Wema ni wa kikazi au wanashuti filamu pamoja, alijibu kwa kusema: "Nililala siku nne kwake wakajua demu wangu!!!"

Alipododoswa zaidi kwanini alale nyumbani kwa Wema wakati Wema yupo na Diamond kwasasa kama wapenzi alijibu "Diamond alikuwa anafungiwa ndani , alikuwepo"

KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII AKEMEA DAWA ZA KULEVYA, ASEMA WATANZANIA ZAIDI YA 500 WASHIKILIWA NCHI ZA NJE,WENGINE 100 WASUBIRI KUNYONGWA NCHINI CHINA

Katibu Mkuu Anna Maembe akisalimiana na akina mama wanakikundi cha kutunza Mazingira katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa jana. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMAKATIBU Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Anna Maembe ametaka vijana vijana nchini kuachana kabisa na biashara ya dawa za kulevya kwani inawasababishia matatizo makubwa katika maisha yao badala yake wajiunge na kutengeneza vikundi vya kijasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kujikwamua kimaisha na kufikia ndoto zao.
Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa, zaidi ya vijana 500 wa Kitanzania wako kizuizini katika nchini tofauti duniani walikokamatwa wakisafirisha dawa hizo, huku vijana wengine wapatao 100 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa nchini China.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii wakati wa ziara yake katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa jana, ambapo alisema biashara hiyo inachafua sana jina la Tanzania katika Jumuia ya Kimataifa kutokana na idadi kubwa ya vijana kujihusisha na biashara hiyo.
Akizungumzia sera ya Jinsia inayotekelezwa na wizara yake, Katibu Mkuu huyo alisema haina lengo la kuwafanya wanawake kuwatunishia misuli wanaume katika familia bali ni kuwawezesha wanawake kushiriki katika uzalisha na kukuza kipato cha familia na taifa  kwa ujumla ili kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimepanda sana kwa sasa.
Vilevile alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto ili kujua changamoto zinazowakabili ikiwemo unyanyasaji wa kijinsi na kisaikolojia wanazokumbana nazo na pia kuwapatia haki zao za kimsingi kama elimu, afya na kusikilizwa kama  ambavyo sera ya watoto hapa nchini inavyoelekeza.
Katika kuimarisha vikundi vya wanawake mkoani Rukwa, katibu mkuu Maembe ametoa shilingi milioni 43 kutoka katika wizara yake, ambapo vikundi kutoka katika Halmashauri za wilaya ya Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Vijijini na Manispaa vitanufaika kwa mtindo wa wanachama wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo kwa ajili ya kutekeleza shughuli zao za kiuchumi

KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII AKEMEA DAWA ZA KULEVYA, ASEMA WATANZANIA ZAIDI YA 500 WASHIKILIWA NCHI ZA NJE,WENGINE 100 WASUBIRI KUNYONGWA NCHINI CHINA

Katibu Mkuu Anna Maembe akisalimiana na akina mama wanakikundi cha kutunza Mazingira katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa jana. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMAKATIBU Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Anna Maembe ametaka vijana vijana nchini kuachana kabisa na biashara ya dawa za kulevya kwani inawasababishia matatizo makubwa katika maisha yao badala yake wajiunge na kutengeneza vikundi vya kijasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kujikwamua kimaisha na kufikia ndoto zao.
Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa, zaidi ya vijana 500 wa Kitanzania wako kizuizini katika nchini tofauti duniani walikokamatwa wakisafirisha dawa hizo, huku vijana wengine wapatao 100 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa nchini China.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii wakati wa ziara yake katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa jana, ambapo alisema biashara hiyo inachafua sana jina la Tanzania katika Jumuia ya Kimataifa kutokana na idadi kubwa ya vijana kujihusisha na biashara hiyo.
Akizungumzia sera ya Jinsia inayotekelezwa na wizara yake, Katibu Mkuu huyo alisema haina lengo la kuwafanya wanawake kuwatunishia misuli wanaume katika familia bali ni kuwawezesha wanawake kushiriki katika uzalisha na kukuza kipato cha familia na taifa  kwa ujumla ili kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimepanda sana kwa sasa.
Vilevile alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto ili kujua changamoto zinazowakabili ikiwemo unyanyasaji wa kijinsi na kisaikolojia wanazokumbana nazo na pia kuwapatia haki zao za kimsingi kama elimu, afya na kusikilizwa kama  ambavyo sera ya watoto hapa nchini inavyoelekeza.
Katika kuimarisha vikundi vya wanawake mkoani Rukwa, katibu mkuu Maembe ametoa shilingi milioni 43 kutoka katika wizara yake, ambapo vikundi kutoka katika Halmashauri za wilaya ya Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Vijijini na Manispaa vitanufaika kwa mtindo wa wanachama wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo kwa ajili ya kutekeleza shughuli zao za kiuchumi

RUBANI NDIE ALIYETEKA NDEGE YA ETHIOPIA


Ndege iliyokuwa imetekwa
Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ethiopia ndiye aliyeiteka nyara .
Maafisa mini Geneva wanasema kuwa naibu huyo wa rubani alichukua usukani wa ndege hiyo rubani wake alipokwenda msalani kwa haja.
Tukio hilo inaripotiwa kutokea ndege hiyo aina ya Boeing 767-300 ilipokuwa ikipaa katika anga ya Sudan.
Rubani huyo msaidizi alibadili mkondo wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Rome Italia ,na kuipaa hadi Uswisi alipoitua katika uwanja wa ndege wa Geneva.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari shirika hilo linasema kuwa abiria wote 200 wako salama .
Ripoti ya idara inayosimamia usafiri wa ndege ya Uswisi inasema kuwa rubani huyo msaidizi aliomba uraiya kabla ya kutua ndege hiyo na akajisalimisha kwa maafisa wa usalama waliokuwa wameizingira ndege hiyo.

Polisi walimtia mbaroni mara moja 

SHEREHE ZA JUBILEE YA MIAKA 25 YA KKKT - DMZV ZILIVYOFANA JANA JIJINI MWANZA.


Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mwanza Ziwa Victoria (DMZV) Andrew Gulle kabla ya kufunua jiwe maalum la Jubilee alikata utepe kuashiria safari ya maadhimisho hayo kuanza rasmi, ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 31 Agosti, 2014.  
Jiwe la jubilee.
Maaskofu waalikwa toka makanisa mbalimbali kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Baada ya tukio la kuzindua jiwe la Jubilee Maaskofu na mamia ya waumini walielekea kwenye jengo la Kanisa kuu la Mwanza kwaajili ya kulizindua.
Kabla ya Uzinduzi wa kanisa la Imani KKKT Mwanza historia ya ujenzi wa kanisa hadi kukamilika ilisomwa naye Bw. Serafin Kimaro. Jumla ya shilingi bilioni moja na milioni 500 zimetumika kukamilisha ujenzi huo uliotumia miaka takribani 13 hadi kukamilika.
Akishuhudiwa na mamia ya waumini na viongozi wa makanisa mbalimbali Kanda ya ziwa na mikoa mingine nchini ukafika wakati sasa wa mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa kukata utepe kuzindua kanisa la KKKT Imani Makongoro Mwanza.