Tuesday, April 29, 2014

WANAFUNZI WAPOTEZA MAISHA WAKIOGELEA KWENYE ‘SWIMMING POOL DAR ES SALAAM

landmark-hotel-pool
Bwawa la kuogelea la kisasa (Swimming Pool) la Hoteli ya Landmark ambapo pamepelekea vifo vya watoto watu na wengine saba kujeruhiwa
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Kinondoni, linamshikilia mfanyabiashara jijini Dar es Salaam, Mboka David (44) mkazi wa Kijitonyama kwa kosa la kusababisha vifo vya watoto watatu wa shule ya msingi na wengine saba kujeruhiwa walipokuwa wakiongelea katika bwawa la kuogelea 'Swimming pool' ya Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach jijini humo FikraPevu imebaini. (J M)
Aidha, taarifa za awali kuhusu tukio hilo ambalo lilitokea jana Jumapili Aprili 27, mwaka huu saa 11 jioni katika hoteli hiyo zilidai mwanamke huyo ambaye sasa anahojiwa, aliwachukua watoto wake wakiwa na watoto wengine (wakiwemo waliokufa) kutoka majumbani mwao eneo la Kijitonyama karibu na Polisi – Mabatini bila ruhusa ya wazazi na kuelekea katika eneo hilo.
Awali, FikraPevu ilidokezwa kuwa, wakati wa tukio mama huyo akiwa na familia yake na watu wengine walikuwa wakijipatia kinywaji (pombe) ndipo watoto hao walipokuwa wakiogelea walizidiwa na maji na kupiga kelele ili kuomba msaada bila kupata mwitikio wowote na hata hapakuwa na mhudumu wa hoteli katika bwawa hilo huku wengine wakifanikiwa kujiokoa wenyewe.
Uchunguzi wa Kipoli
FikraPevu ilifuatilia tukio hili kwa karibu ambapo Inspekta katika kanda hiyo lilithibitisha tukio hilo kupitia kwa Mkaguzi msaidizi wa Polisi katika kanda hiyo, na kuelezea mazingira ya tukio hilo.
Alisema siku ya tukio mwanamke huyo ambaye hadi sasa anahojiwa, walienda katika hoteli hiyo kwa lengo la kufanya sherehe 'birthday' ya kuzaliwa kwa mtoto Eberick Mboka (1), wakiwa na ndugu jamaa na marafiki.
Hata hivyo alisema watoto hao walifariki katika Hospitali ya Entry-Mbezi walipokuwa wamepelekwa na wahudumu wa hoteli hiyo baada ya kupata taarifa hizo kwa ajili ya matibabu.
Aliwataja marehemu kuwa ni, Ndimuni Bahati (9), Eva Nikolas (6) na Janeth Zakaria (10) na wote ni wa jinsia ya kike. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo huku Jeshi hilo likikanusha kuchelewa kufika katika tukio hilo kama ambavyo vyanzo vya FikraPevu vilidokezwa na mashuhuda kuwa utoaji taarifa wa tukio hilo uligubikwa na hali ya usiri/utata.

No comments:

Post a Comment