Saturday, April 12, 2014

RAIS KIKWETE APEWA TUZO WASHINGTON DC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jumatano jioni alipewa tuzo la kiongozi mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika. Tuzo hilo lilipokelewa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw. Bernard Membe.
Sherehe za kutoa tuzo hilo ziliandaliwa na jarida la African Leadership Magazine Group kwenye hoteli ya St. Regis ya Washington DC.
Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kutoka hoteli hiyo, mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya Tanzania Bw. Salva Rweyamamu alisema rais Kikwete alituzwa kutokana na huduma zake kwa jamii ya Tanzania, lakini pia ametambuliwa kwa kuwa mstari wa mbele kutatua migogoro barani Afrika.
Mahojiano na Salva Rweyemamu
 Hotuba na sherehe wakati wa hafla hiyo zilipepereshwa hewani moja kwa moja kupitia mtandao wa mawasiliano ya internet.
Tuzo hilo la heshima hutolewa kwa viongozi wa bara la Afrika wanaotoa mchango mkubwa zaidi kwa jamii zao ikiwa ni pamoja na utawala bora

No comments:

Post a Comment