WAKATI Saluti5 ilipofanya ziara ya kwenda Masaki kijijini kwa mwimbaji Muhidin Maalim Gurumo aliyefriki Jumapili, ilipata mambo mengi mahsusi kutoka mwa gwiji huyo.
Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.
Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.
Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.
“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.
“Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.
“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akisimulia namna alivyopoteza jicho lake.
No comments:
Post a Comment