Tuesday, April 29, 2014

INASEMEKANA DANCE WA DIAMOND AMEKAMATWA CHINA NA MADAWA YA KULEVYA












STAA  wa  muziki  wa  bongo  fleva  nchini, Abdul  Nassib  "Diamond"  ametakiwa  kutokanyaga  kabisa  nchini  China  na  kwamba  akitokeza  pua  yake  nchini  humo  asahau  kabisa  kurudi  uraiani...

Hiyo  inafuatia  kijana  mmoja  mtanzania  kukamatwa  wiki  iliyopita  uwanja  wa  ndege  wa   Macau   China  na  kudai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

Habari  kutoka  Macau  China  zinadai  kuwa  kijana  huyo  aliyejulikana  kwa  jina  moja  la  Manyota  alikamatwa  akiwa  kwenye  harakati  za  kuingiza   mzigo  huo  wa  dawa  za  kulevya  kwa  kupitia  uwanja  wa  ndege  wa  Macau....

Kwa  mujibu  wa  vyanzo  vyetu  vya  habari, inaarifiwa  kuwa  Manyota  alikamatwa  Alhamisi  ya  wiki  iliyopita  katika  uwanja  uleule  aliokamatwa  mtanzania  mwingine  Jackline  Patrick, anayesotea  rumande  mpaka  hii  leo  huko  huko  Macau  China.....

Kijana  mmoja  wa  kitanzania  anayefanya  shughuli  zake  huko  China  amedai  kuwa  Manyota  alikamatwa  na  maofisa  wa  usalama  wa  uwanja  wa  ndege  na  katika  utetezi  wake  alidai  kuwa  yeye  ni  mwanamuziki  toka  Afrika  Mashariki...

Mtanzania  huyo  aliendelea  kudai  kuwa, Manyota  baada  ya  kukamatwa  alianza  kubabaika  kwa  kujifanya  mwanamuziki  na  baadae  akadai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

"Alijifanya  yeye  ni  mwanamuziki, baadae  akabadilika  na  kudai  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania  na  kwamba  ndani  ya  ule  mzigo  alikuwa  hajui  kuna nini  zaidi  ya  kuombwa  na  jamaa  zake  wa  Dar  awapelekee  nchini  China"...Alisema  mtanzania  huyo

Inasemekana  kuwa, ili  kujiridhisha, maofisa  hao  wa  usalama  wa  uwanja wa  ndege    walimtaka  kijana  huyo  aoneshe  moja  ya  kazi  zake  na  yeye  akaishia  kuwaonesha  moja  ya  video  za  Diamond  kupitia  mtandaoni  na  kumuonesha  mmoja  wa  wacheza  shoo  wa  mwanamuziki  huyo  kuwa  ndo  yeye  Manyota...

Inasemekana  kuwa, pamoja  na  utetezi  wake  huo  ambao  unaweza  kumuingiza  matatani  Diamond,maofisa  hao  wa  usalama  walishndwa  kumuelewa  na  kumtupa  ndani.....

Mtanzania  huyo  alihitimisha  kwa  kudai  kuwa, kutokana  na  mazingira  yalivyo,ni  vyema  mwanamuzi  Diamond  akawa  makini   sana  kama  atakuwa  na  safari  za  kwenda  China  kwani  kwa  namna  moja  ama  nyingine  jina  lake  limewekwa  kwenye  orodha  ya  majina  machafu   na  wanaweza  kumkamata  kwa  lengo  la  kuujua  ukweli.

USHIRIKIANO HUU WA ‘UKAWA’ UWE ENDELEVU

mboye_a034a.jpg
Bila shaka kila mwananchi anayeitakia mema nchi yetu amevutiwa na habari zilizochapishwa katika gazeti hili jana kwamba vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeamua kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
Viongozi wakuu wa vyama hivyo tayari wamekubaliana kuanza mchakato huo na wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.
Sisi tunaona kitendo hicho cha vyama vinavyounda Ukawa kuwa ni hatua muhimu ya kuongeza nguvu ili kuongeza ushindani ambao ni muhimu katika mustakabali wa nchi yetu kisiasa na hivyo kusaidia nyanja nyingine za kiuchumi na kijamii.
Tangu kuruhusiwa tena kwa siasa huru karibu miaka 22 sasa, bado nchi haijashuhudia ushindani wa kweli unaoweza kuwafanya watawala kuwajibika kwa wananchi kutokana na kuona hatari ya kuondolewa madarakani na vyama pinzani.
Hii imetokana na vyama shindani katika siasa kukumbwa na mifarakano ya kisiasa ambayo imekuwa ikiwagawa na hivyo kuingia kwenye chaguzi vikiwa dhaifu na hivyo kushindwa vibaya na chama tawala na matokeo yake yamekuwa ni wananchi wengi kukata tamaa na hivyo kusababisha idadi ya wanaoshiriki kupiga kura kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na kutoona faida ya siasa za ushindani.
Pengine hiyo ndiyo sababu iliyofanya wananchi wapendekeze kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba vyama viruhusiwe kuunganisha nguvu wakati wa chaguzi kwa kuwa wameona bila ya nguvu ya vyama shindani, watawala wawataendelea kuongoza kwa mazoea na matokeo yake ni wananchi kuendelea na umaskini wao na kuona uhuru wa vyama vya kisiasa hausaidii kuwa kuboresha maisha yao.
Si nia yetu kuona chama tawala kikiondolewa madarakani na vyama shindani, lakini tunachotaka kuona na ushindani wa dhati, makini na wa kweli ambao, kwa taifa lolote lile, ni afya kwa ustawi wa wa taifa kwa kuwa huongeza uwajibikaji kwa watawala.
Hakuna ubishi kwamba upinzani wenye nguvu huisukuma serikali ichape kazi na kuwatumikia wananchi kwa kutambua kwamba ikiboronga itaondolewa madarakani na serikali kivuli ambayo ni vyama vya upinzani.
Vyama legelege vya upinzani huogopa kivuli cha serikali na kufifisha maendeleo na kuzima matumaini ya wananchi wanaotaka kuona uwajibikaji serikalini, kwani huwa chachu ya kuendeleza tawala za kiimla zisizothamini demokrasia na zisizowajibika kwa wananchi.
Ndiyo maana tunawapongeza viongozi wa Ukawa kwa kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu na kuwa wamoja ili kuweka ushindani wa kweli katika mazingira ya kisiasa tuliyomo.
Tunachoweza kuwashauri viongozi wa Ukawa ni kuwa makini na kuondoa tofauti zinazowatenganisha. Ukawa isitarajie kwamba kila kitu kitakuwa mteremko, kwani bado sheria kandamizi ambazo zimekuwa zikikwaza shughuli za upinzani bado hazijafutwa.
Ni matarajio yetu kwamba serikali na chama tawala kitachukulia hatua hiyo ya Ukawa kuwa changamoto ya kuongeza ufanisi katika kuwatumikia wananchi na si kuanza kujenga chuki na kutafuta mbinu za kuikwamisha
Serikali haina budi kuhakikisha kuwa vyama vyote vinapewa nafasi sawa ya ushindani na kujengewa mazingira ya kukua ili kukifanya chama chochote kinachopewa madaraka kiwajibike kwa wananchi na kuwaletea maendeleo

SUAREZ NDIYE MCHEZAJI BORA KATIKA LIGI KUU ENGLAND (EPL)

140123090409_luiz_suarez_512x288_z_nocredit_0abe5.jpg
Mshambulizi wa Liiverpool Luis Suarez, ametajwa kuwa mchezaji mwenye tajriba na maarifa ya hali ya juu mwaka huu.
Suarez mwenye umri wa miaka 27 alisafiri kuelekea katika sherehe hizo baada ya wao kushindwa na timu ya Chelsea.
Akizungumuza katika sherehe hiyo Suarez alisema kuwa ‘Ligi ya Primia ina wachezaji wengi ambao ni wazuri zaidi na ni jambo la heshima sana wachezaji hawa wakiona mchango wako uwanjani’"
Suarez kufikia sasa amefunga mabao 30 na ndiye anayeongoza matumaini Liverpool kukatisha ukame wa miaka 24 tangu watwae taji la ligi kuu ya Uingereza.
Suarez atakumbukwa zaidi kwa kisa kilichogonga vichwa vya habari duniani baada ya kumng"ata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic.
Suarez alipigwa marufuku ya mechi Kumi baada ya kupatikana na hatia .
Wengine walioteuliwa ni Eden Hazzard wa Chelsea aliyetajwa kama mchezaji mchanga wa mwaka huu.
Daniel Sturridge na naodha wa Liverpool Steven Gerrard walijiunga na Suarez kutokana ushirikiano wao iliyopelekea Liverpool kutajwa kama klabu bora ya mwaka huu.
Waliokuwemo ni pamoja na Kipa wa Chelsea Peter Czech na mlinzi Gary Cahil.
Hata hivyo msururu huo haingekamilika pasipo kuwataja Yaya Toure na Vincent Kompany wote wa Manchester City.
Luke Shaw na Adam Lallan wa Southampton pia wakitajwa katika orodha hiyo naye Seamus Coleman wa Everton akifunga ukurasa huo

BASI LA HOOD LILIVYOUNGUA MOTO NA KUTEKETEA KABISA MKOANI PWANI

Zaidi ya Abiria 55 waliokuwa ndani ya Basi la kampuni ya Hood, wakisafiri kutoka Mbeya kwenda Arusha walinusurika kufa baada ya Basi hilo kushika moto na kuteketea kabisa katika kijiji cha Kilolele-Chalinze Mkoani Pwani

WANAFUNZI WAPOTEZA MAISHA WAKIOGELEA KWENYE ‘SWIMMING POOL DAR ES SALAAM

landmark-hotel-pool
Bwawa la kuogelea la kisasa (Swimming Pool) la Hoteli ya Landmark ambapo pamepelekea vifo vya watoto watu na wengine saba kujeruhiwa
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Kinondoni, linamshikilia mfanyabiashara jijini Dar es Salaam, Mboka David (44) mkazi wa Kijitonyama kwa kosa la kusababisha vifo vya watoto watatu wa shule ya msingi na wengine saba kujeruhiwa walipokuwa wakiongelea katika bwawa la kuogelea 'Swimming pool' ya Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach jijini humo FikraPevu imebaini. (J M)
Aidha, taarifa za awali kuhusu tukio hilo ambalo lilitokea jana Jumapili Aprili 27, mwaka huu saa 11 jioni katika hoteli hiyo zilidai mwanamke huyo ambaye sasa anahojiwa, aliwachukua watoto wake wakiwa na watoto wengine (wakiwemo waliokufa) kutoka majumbani mwao eneo la Kijitonyama karibu na Polisi – Mabatini bila ruhusa ya wazazi na kuelekea katika eneo hilo.
Awali, FikraPevu ilidokezwa kuwa, wakati wa tukio mama huyo akiwa na familia yake na watu wengine walikuwa wakijipatia kinywaji (pombe) ndipo watoto hao walipokuwa wakiogelea walizidiwa na maji na kupiga kelele ili kuomba msaada bila kupata mwitikio wowote na hata hapakuwa na mhudumu wa hoteli katika bwawa hilo huku wengine wakifanikiwa kujiokoa wenyewe.
Uchunguzi wa Kipoli
FikraPevu ilifuatilia tukio hili kwa karibu ambapo Inspekta katika kanda hiyo lilithibitisha tukio hilo kupitia kwa Mkaguzi msaidizi wa Polisi katika kanda hiyo, na kuelezea mazingira ya tukio hilo.
Alisema siku ya tukio mwanamke huyo ambaye hadi sasa anahojiwa, walienda katika hoteli hiyo kwa lengo la kufanya sherehe 'birthday' ya kuzaliwa kwa mtoto Eberick Mboka (1), wakiwa na ndugu jamaa na marafiki.
Hata hivyo alisema watoto hao walifariki katika Hospitali ya Entry-Mbezi walipokuwa wamepelekwa na wahudumu wa hoteli hiyo baada ya kupata taarifa hizo kwa ajili ya matibabu.
Aliwataja marehemu kuwa ni, Ndimuni Bahati (9), Eva Nikolas (6) na Janeth Zakaria (10) na wote ni wa jinsia ya kike. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo huku Jeshi hilo likikanusha kuchelewa kufika katika tukio hilo kama ambavyo vyanzo vya FikraPevu vilidokezwa na mashuhuda kuwa utoaji taarifa wa tukio hilo uligubikwa na hali ya usiri/utata.

Monday, April 21, 2014

Kietyongyuth ampiga Miyeyusho

Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka nchini Thailand imempiga Bondia Francis Miyeyusho Chichi Mawe kwa Knock Out katika daidika za awali za mzunguko wa kwanza kati ya mizunguko kumi waliyotakiwa kucheza

Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka Thailand (kulia) baada ya kumpiga Fransic Miyeyusho, katika raundi ya kwanza ya pambano na kumaliza pambano hilo kwa KO.
Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka nchini Thailand imempiga Bondia Francis Miyeyusho Chichi Mawe kwa Knockout (KO) katika daidika za awali za mzunguko wa kwanza kati ya mizunguko kumi waliyotakiwa kucheza katika pambano lisilo la ubingwa,pambano lililopigwa katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam
Akiongea mara baada ya Pambano hilo mwamuzi wa Pambano,Emmanuel Mlundwa anasema wamelazimika kumaliza pambano kufutia Francis Miyeyusho kuanguka mara mbili na kuonekana hawezi kuendelea kufuatia kuzilai baada ya kupigwa masumbwi mazito ya kichwa na Bondia huyo kutoka Thailand.
Pambano hilo la kimataifa la masumbwi litatanguliwa na pambano kati ya Bondia Gavad Zohrehvand kutoka nchini Iran aliyepambana na Francis Cheka ambapo walitoka suluhu baada ya kumaliza mizunguko nane ya mchezo huo pasipo kuambulia mshindi.

Friday, April 18, 2014

SABABU YA MAALIM GURUMO KUPOTEZA JICHO LAKE MOJA UNAIFAHAMU?

WAKATI Saluti5 ilipofanya ziara ya kwenda Masaki kijijini kwa mwimbaji Muhidin Maalim Gurumo aliyefriki Jumapili, ilipata mambo mengi mahsusi kutoka mwa gwiji huyo.

Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau  au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.
Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.
Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.
“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.
“Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.
“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akisimulia namna alivyopoteza jicho lake.

Breaking-news-meli-yazama-ziwa-victoria

Meli ya mizigo ya Kampuni ya FB Matara iliyokuwa inatoka Bukoba kwenda Mwanza ikiwa na wafanyakazi kumi na shehena ya sukari imezama ziwa victoria katikati ya visiwa vya Kerebe na Bumbile. Taarifa kamili itakujia baadaye...









..

Hili ndilo Daraja refu kuliko yote duniani linalopita juu ya bahari

Chukua hiyo: Daraja refu kuliko yote duniani linalopita juu ya bahari

Daraja la Akashi- Kaiyo lililopo Japan ndilo daraja refu na pana kuliko madara yote duniani yanayopita juu ya maji.
Daraja hilo lina urefu wa mita 1,991 juu na lilijengwa kwa muda wa miaka 10, ambapo lilimalizika mwaka 1998.
Daraja hilo linaunganisha jiji la Kobe liliko bara na Iwaya iliyoko katika kisiwa cha Awaji. Daraja hili linajulikana pia kama ‘Pearl Bridge

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD.


MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument. 
2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station. 
3. Barabara ya Kivukoni Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).

4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.

5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .

Key:
1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.

2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way}

3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets}

4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala

5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART

6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout}

7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}

Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.

AU.
OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA

MASOGANGE, NIKISEMA UNAJIUZA UTAKATAA?



AGNES Jerald, binti anayetumika sana kunengua na pozi katika video za nyimbo za wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, amejipatia umaarufu mkubwa sana baada ya kufanya kazi na mkali wa Morogoro, Belle 9 katika kibao chake cha Masogange.

Limegeuka kuwa jina lake na mwenyewe analitumia kikamilifu katika harakati za kimjini. Lakini aligeuka kuwa kipusa zaidi baada ya kukamatwa katika Uwanja waNdege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg mwaka jana, akiwa na shehena kubwa ambayo Tanzania ilijulikana kama madawa ya kulevya, lakini Afrika Kusini wakasema ni malighafi inayoweza kutumika kutengeneza mihadarati.


Masogange ni msichana ambaye Mwenyezi Mungu amemjaalia uzuri wa asili wa Kiafrika. Ana sura nzuri ambayo bado hajaanza kuikoboa kwa mikorogo na mwili unaoendana na umbo lake maridhawa.

Sifa moja kubwa ya uzuri wa msichana huyu, ni maumbile yake ya nyuma, amejazia kiasi ambacho ni wanaume wachache, tena walio waadilifu kwelikweli, wanaoweza kupishana naye na wasigeuke nyuma kuhakikisha walichokiona!

Baada ya kuachiwa kutoka mahabusu nchini Afrika Kusini ambako alishindwa kesi ya kukutwa na shehena ile ya madawa ya kulevya, Masogange alijikuta akiwa gumzo kubwa jijini Dar es Salaam, kiasi kwamba pamoja na kuachiliwa, bado ilimchukua muda mrefu kurudi nyumbani.

Akiwa huko kwa Madiba, binti huyu alikuwa akiweka picha zake kila mara katika mitandao ya kijamii inayopatikana katika Internet, hasa Instagram. Ni utamaduni mpya kwa wasichana wa Kibongo siku hizi, wengi wanapenda kutupia picha zao humo na watu ambao huwaona, huwasifia kama wamependeza au huwaponda kama wamechukiza.

Lakini katika hali isiyotarajiwa kabisa, wiki kadhaa zilizopita, Masogange aliweka picha yake huko, ikionyesha sehemu kubwa ya mwili wake, ikiwa imepakwa hina.

Aliipaka kwa staili ambayo mtu akiitazama haraka haraka anaweza kudhani ni Tattoo, ile michoro inayochorwa kwa sindano mwilini ambayo hapo awali tulianza kuiona kwa wasanii wa Kimarekani.

Lakini kitu kibaya katika picha hiyo ni kwamba Masogange amepiga picha mguu wake akiwa amepaka hina hiyo hadi juu kabisa pajani.

Baadaye akapiga picha nyingine akiwa amevaa kimini, lakini kikionyesha sehemu ya paja hilo lililopakwa urembo huo ambao pia hutumiwa na wanawake wa Kiislamu wakati wa ndoa!

Ni picha ambayo mwanaume yeyote mkware akiiona, anavuta hisia za mahitaji ya kimapenzi. Na nieleweke, siyo Masogange tu anayetupia picha za aina hii, wasichana wengi hufanya hivi na baadhi yao, baada ya kuziweka, huweka pia na namba zao za simu, ukiwa na shida nao uwatafute!

Sitaki kuamini moja kwa moja kwamba msichana huyu ambaye amepata umaarufu bila ya kutarajiwa anajiuza, lakini ni vigumu sana kwa picha zile kuacha kusadiki jambo hili kama mtu mmoja atajitokeza na kutoa madai kama hayo.

Inakuaje mtoto wa kike, mwenye jina, tena na uzuri wako bomba kabisa wa asili, unapiga picha za namna ile na kuziweka hadharani? Nafikiri siyo sawa, zipo picha zinazopaswa kuendelea kubakia chumbani.

Kwa jinsi mambo yanavyotokea, unapata kabisa hisia kwamba kumbe dada zetu wanatafuta umaarufu kwa nguvu kwa malengo binafsi, yasiyo ya kimaadili na yenye kuchefua.

Wakishapata majina na bahati nzuri kuanza kufuatiliwa na vyombo vya habari, vikitanguliwa na magazeti, wanaanza makeke!

Kwa kutambua kwamba sura zao zinafahamika, badala ya kujistahi, ndiyo kwanza utashangaa kuona wanavaa mavazi yenye utata, kumbe tunaanza kuelewa kuwa wanafanya hivi ili kujitangaza, kama wanavyosema mabingwa wa uchumi, biashara matangazo.

Rais Kikwete: "Ni kukosa adabu, Tuwaache walivyo, Dunia itawafundisha"

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ni ukosefu wa adabu kuwatukana waasisi wa Tanzania - JK

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu kuwa baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli Waanzilishi ma Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume. 

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa viongozi hao wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi, mambo makubwa na mambo ya kihistoria kiasi cha kwamba Watanzania wanao wajibu wa kudumisha na
kuenzi heshima yao kwa namna ya kudumu. 

Akizungumza na Wahariri wa baadhi ya
vyombo vya habari usiku wa jana, Jumatano, Aprili 16 katika mahojiano maalum ya kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano, Rais Kikwete amesema: "Ni kukosa adabu na ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mtanzania yoyote kuwatukana, kuwadhihaki ama kuwakejeli waasisi wa Tata letu. Hawa ni watu ambao waliifanyia nchi yetu mambo makubwa," amesema Rais Kikwete na kuongeza: 

"Mzee Karume yule aliongoza Mapinduzi yaliyoondoa dhuluma na uonevu pale Visiwani. Waafrika walio wengi walikuwa wanaonewa sana pale Tanzania Visiwani, pengine watu wamesahau, lakini hata pale walipokuwa wanashinda uchaguzi bado walikuwa hawapewi nafasi ya kuongoza maisha yao wenyewe." 

Amesisitiza Rais Kikwete: "Ni ukosefu wa adabu kwa yoyote kumshutumu mtu aliyejitolea kiasi hicho ili kubadilisha mfumo dhalimu na kujenga maisha na mazingira ya maisha bora kwa wengi." 


"Mzee Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye umoja, lenye amani na mshikamano. Misingi ambayo aliijenga yeye ndiyo imeendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka pate hii. Viongozi wengine wale ambao wamemfuata yeye — Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa mimi mwenyewe, tumefuata na kuongozwa na misingi hii. Na siku nchi yet inaamua kuipuuza misingi hiyo, tutaingia katika matatizo makubwa." 

Rais Kikwete ametoa msimamo boo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu matusi, kejeli, dhihaki ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache ma Bunge Maalum la Katiba juu ya waasisi hao ma Tanzania na Wabunifu Wakuu wa Muungano wa Tanzania.

PISTORIUS TAABANI....! SOUTH AFRICA

Pistorius akitoa ushahidi
Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius amerejea tena mahakamani kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi februari tarehe 14 mwaka uliopita .
Bwana Nel amekuwa akimwandama Pistorius , akisema hakuwa mkweli katika toba yake na alimfokea mpenzi wake Reeva Steenkamp mara kwa mara 
Siku ya kwanza ya maswali ya mahakama dhidi yake Nel alianza kwa kuonyesha picha za kutisha za kichwa kilichochuruzika damu cha Bi Steenkamp, baada ya kupigwa risasi na Pistorius.
Mwanariadha huyo anadai hakumuua makusudi bali alidhani ni mtu alievamia nyumba yake.
Ameiambia mahakama kuwa alimpenda sana mwanadada huyo Reeva.(P.T)
Kiongozi wa mashataka amemsuta Pistorious akisema kuwa alikuwa ni mbinafsi sana kwa mpenzi wake na kuwa kile alichokijali sana ilikuwa ni sifa zake na hadhi yake katika jamii.
Pistorious alikanusha madai hayo akisema anajuta kwanini hakuwahi kumwambia Reeva kuwa anampenda kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.
Mwanariadha huyo alikuwa na wakati mgumu kuelezea mahakama kwanini Reeva alimlaumu kwa kumuonea katika moja ya ujumbe wa simu ya mkononi wa WhatsApp ambao alimwandikia Oscar''tangu turejee kutoka cape town umekuwa ukinionea sana .''
Viongozi wa mashtaka wana imani kuwa alimuuwa kimakusudi ndani ya choo chake baada ya kuzozana.
Mwanariadha huyo mlemavu mwenye umri wa miaka 27, ambaye hana miguu yake yote mawili, huenda akahukumiwa jela maisha iwapo atapatikana na kosa la kuuwa.
Kinyume ya hali ilivyokuwa Siku ya Jumanne, alipolia kizimbani alipokuwa akielezea yaliyojiri nyumbani kwake kabla na baada ya mauwaji hayo,
leo alionekana mjasirii na mtulivu akimjibu Kiongozi wa mashataka ya umma bwana Nel.
Mamake Reeva bi June Steenkamp amesema kuwa japo aliombwa msamaha na Oscar moyo wake haukumsamehe kwani hadi hapo Oscar hakukiri alimua bali alisisitiza kuwa anaomba msamaha kwa kusababisha kifo chake..
Bi Steenkamp alishangaa iwapo Pistoriuos alikuwa anaigiza au la kwani amekuwa akilia na kutapika mahakamani .
Katika tukio lingine Oscar alikataa katakata kuwa alifyatua risasi katika mkahawa mmoja alipoulizwa na kiongozi wa Mashtaka bwana Nel.
Pistorious alisema kuwa hakujua bunduki hiyo ilikuwa na risasi.
Iwapo hatapatikana na hatia ya kukusudia kuua Reeva ,basi kulingana na sheria za Afrika Kusini, Pistorious huenda akashtakiwa kwa kosa la kuua bila ya kukusudia ambayo hukumu yake ni kati ya miaka 6- 15 jela.
Mbali na shtaka la mauaji, Pistorius anakabiliwa na shtaka la kufyatua bunduki hadharani na shtaka lingine la kumiliki risasi kinyume na sheria

KIGOGO TANESCO ASHTAKIWA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA MIL. 200/-

tanescologo_e4d1c.jpg
Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Semtutu na wenzake wanne, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka mawili yakiwamo ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. milioni 200.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa Fedha, Lusekeo Kasanga, Mwanasheria Godson Ezekiel na Mkandarasi Martin Abraham.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isdore Kyando alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011.
Kyando alidai kuwa katika shitaka la kwanza, Desemba, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo jijini Dar es Salaam washtakiwa walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha Mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho.

Tuesday, April 15, 2014

MAFURIKO DAR: WALIOPOTEZA MAISHA WAFIKIA 13

111222170118 tanzania floods 304x171 jamiiforums nocredit 8c4d1
Na MABANTANYAU FAMILY.
Idadi ya waliokufa kutokana na mafuriko jijini Dar es Salaam imefikia watu 13 kufikia Jumatatu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadiq Meck Sadiq amesema idadi hiyo huenda ikaongezeka baada ya kupata taarifa za matukio ya mafuriko kutoka maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa siku tatu mfululizo tangu Ijumaa iliyopita, mvua kubwa ziliendelea kunyesha na kusababisha madhara makubwa vikiwemo vifo, uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja, hivyo kukata mawasiliano na mikoa ya jirani ya Pwani na Morogoro na hata ndani ya mkoa wenyewe.
Karibu maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam yameathirika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko, huku wakaazi wa maeneo ya mabondeni wakiathirika zaidi baada ya nyumba zao kujaa maji.
Miundombinu ya barabara na madaraja mbalimbali yanayounganisha jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake pia imeharibiwa.
Mradi mwingine muhimu wa mabasi yaendayo kasi, DART unaolenga kutatua tatizo la usafiri jijini Dar es Salaam, nao umeathiriwa na mafuriko hayo ambapo magari, mashine na mifuko ya saruji imechukuliwa na maji hivyo kusitisha shughuli zake za ujenzi zilizo katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi huo.
Shughuli za urejeshaji wa miundombinu zimekuwa zikiendelea ikiwa ni pamoja na matengenezo katika daraja la Mpiji linaloiunganisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Hata hivyo Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania, TMA, yametahadharisha kuhusu kuendelea kunyesha kwa mvua na kuwataka watu wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhama ili kusalimisha maisha na mali yao

MAELFU YA ABIRIA WAKWAMA UBUNGO

mabasi_28773.jpg
Dar es Salaam. Uharibifu wa barabara uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, umeendelea kuwatesa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mbalimbali nchini hasa baada ya mabasi ya mikoani kuzuiwa kufanya safari zake jana.
Amri ya kuzuia mabasi hayo ilitolewa jana ikiagiza mabasi yote yasiondoke katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo hadi itakapotangazwa vinginevyo, kutokana na uharibifu wa Barabara za Kilwa, Morogoro na Bagamoyo ambako madaraja yamevunjika.
Dereva wa Basi la Adventure liendalo Kigoma, Joseph Luciano alisema walitangaziwa na Sumatra na trafiki kuwa wasubiri mpaka hapo watakapojulishwa kuondoka.
"Hatuwezi kuondoka mpaka Serikali itakapotangaza ili kuepuka faini ambayo wenzetu, wale wanaopakia nje, wametozwa," aliongeza huku ikielezwa kuwa baadhi ya mabasi yalitozwa faini kwa kukiuka amri hiyo.
Abiria anayesafiri kwenda Kibondo, Kigoma, Lydia Lutakinikwa alisema: "Nilikuja kuchukua mzigo wa duka langu tangu Ijumaa na nimekuwa nikilala gesti. Nimeishiwa hela hivyo nalazimika kuendelea kuwapo kwenye hili basi kwa kuwa sina tena pesa ya kwenda kulipia malazi."
Kondakta wa Basi la Taqwa liendalo Nairobi, Yahaya Maulid alisema wameruhusu kubadilishwa tiketi za abiria wao, kama walivyoelekezwa na mamlaka husika ili kutoa nafasi kwao kujipanga upya.
Mkuu wa Usalama Barabarani Ubungo, Inspekta wa Polisi, Yusuf Kamutta alisema zaidi ya mabasi 400 yameathiriwa na uamuzi huo... "Tumezuia mawakala wasitoe tiketi mpya kwa sababu abiria wa leo (jana) ndiyo wanaotarajiwa kusafiri kesho, hivyo wanaweza kuuza tiketi za kuanzia keshokutwa."
Msururu wa magari Pwani
Kutokana na kuharibika kwa baadhi ya madaraja katika Mkoa wa Pwani, magari yaliyokuwa yakisafiri kutoka maeneo mbalimbali yalikwama katika maeneo tofauti. Baadhi yalikwama Visiga na mengine Mlandizi jirani na Kituo cha Polisi katika misururu mirefu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei aliwataka wamiliki wa magari makubwa ya mizigo wanaotumia barabara hiyo kusitisha safari zao kwa kipindi hiki hadi hapo hali itakapotengamaa.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani na uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ililazimika kuweka kambi kwa siku nzima eneo la Mlandizi jirani na daraja la Ruvu kusimamia shughuli ya ukarabati wa daraja dogo lililokuwa na hitilafu.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani, Tumaini Sarakikya alisema hadi jana mchana magari yalikuwa yameanza kupita upande mmoja, lakini baadaye jioni yangeanza kupita bila wasiwasi
Waliokufa Dar wafikia 13
Mafuriko yaliyotokana na mvua hizo yamesababisha vifo vya watu 13 mkoani Dar es Salaam hadi jana, huku Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pekee ikipokea maiti tisa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema maiti mbili zilipatikana Wilaya ya Temeke na nyingine moja ilikutwa eneo la Jangwani, Ilala na miili hiyo imehifadhiwa MNH na Hospitali ya Temeke.
Alisema jitihada zinaendelea kubaini iwapo kuna miili zaidi katika mito na mabonde ambayo yalikumbwa na mafuriko hayo na ameomba mwananchi kutoa ushirikiano.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema hadi jana hospitali hiyo ilikuwa imepokea maiti tisa zote zikiwa za wanaume na kati ya hizo, mbili zimetambuliwa na ndugu zao.
Kwa upande mwingine, Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Njela alisema maiti moja ya mwanamume ilikutwa jana kwenye Mto wa Mabibo nyuma ya Kampuni ya Ami

SERIKALI YAJITETEA UBOVU MIUNDOMBINU

Wananchi wakipita kwa taabu katika sehemu finyu ya barabara ya Kilwa maeneo ya Mbagala, iliyoharibiwa na maji ya mvua na kusababisha magari kushindwa kupita. Picha na Venance Nestory
Dar es Salaam. Wizara ya Ujenzi imesema kuwa asilimia kubwa ya miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko haikujengwa chini ya kiwango kama inavyodaiwa, bali ni matokeo ya uharibifu wa mazingira.(MM)
Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa wizara hiyo, Martin Ntemo alisema madaraja mengi yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea nchini yameliwa katika makutano na barabara na si kumeguka.
"Mito mingi imechepuka katika mikondo yake ya zamani kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wakazi wa maeneo hayo kila kukicha.," alisema na kuongeza:
"Pia asilimia kubwa ya madaraja hayo yameshuka katika urefu wake wa awali kutokana na mchanga unaosababishwa na mmonyoko wa udongo, hivyo kupunguza sehemu iliyokuwa imekadiriwa kwa maji kupita."
Aliongeza kuwa madaraja na barabara hizo nyingi zilikuwa zimeshakabidhiwa muda mrefu kwa Serikali na kwamba Wizara inaendelea kutafuta suluhu ya kuyarudisha katika hali yake ya kawaida.
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimeendelea kuharibu miundombinu mbalimbali ya barabara ambapo mawasiliano kati ya Jiji la Dar es Salaam na mikoani yalikatika kutokana na madaraja kuharibika na kufurika maji.
"Tulikuwa na wakati mgumu katika Daraja la Mpiji kutokana na uhaba wa mawe, lakini tayari tumeshapata sehemu ambayo malori yatakuwa yakichukua na kupeleka eneo la ujenzi," alisema Ntemo.
Alisema walifanikiwa kupata mawe eneo la Wazo Hill na viunga vyake ambayo yatasaidia kukamilisha ujenzi wa daraja hilo lililopo Barabara ya Bagamoyo kufikia leo asubuhi au mchana.
Kwa mujibu msemaji huyo, tayari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Kampuni za Ujenzi za Skol Building Contractors na Estim zinaendelea na ujenzi wa maeneo mbalimbali yaliyoathirika.
Alipoulizwa kuhusu gharama za jumla za uharibifu huo, alisema bado Wizara inaendelea kukusanya taarifa ikizingatiwa kwamba mvua bado zinaendelea kunyesha.
Aliongeza kuwa, Waziri aliagiza madaraja yote kutengenezwa usiku kucha kuhakikisha yanaendelea kuunganisha miji na mitaa kama awali.
"Wanajeshi wanaangalia jinsi ya kuweka daraja la dharura katika Daraja la Mto Kiziga ambalo kalavati liliharibika na pale Kongowe, daraja la Mto Kozi, wanajaza kifusi ili kufungua mawasiliano yaliyokuwa yamesitishwa," alisema

LOWASSA AMKARIBISHA MKAPA MONDULI

lo_e37a9.jpg
mk_cb85d.jpg
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh Benjamin Mkapa katika shule ya msingi ya Manyara Ranchi wilayani Monduli ambayo inafadhiliwa  na shirika la kimataifa ya African Wildlife Foundation.Mzee Mkapa ni Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo duniani.

Monday, April 14, 2014

TUNDU LISSU ATIKISA BUNGE

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Tundu Lissu.PICHA|MAKTABA
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Tundu Lissu amesema Tanganyika ilikufa kwa amri iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere na siyo kwa makubaliano katika hati ya Muungano.
Lissu alitoa kauli hiyo jana alipopata fursa ya kukamilisha dakika 16 za hotuba yake ya ufafanuzi wa maoni ya walio wachache iliyokuwa imekatishwa baada ya matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni ya Taifa (TBC1) kukatika Jumamosi iliyopita.(MM)
Huku akinukuu maneno yaliyopo katika vitabu vilivyoandikwa na Profesa Issa Shivji na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, Lissu alisema Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bila uhalali wa kisheria kwa kuwa hayakuwapo makubaliano ya kila upande wa Muungano.
Alisema Aprili 26, 1964 (Siku ya Muungano), Mwalimu Nyerere alitoa amri ya masharti ya mpito ya mwaka 1964 ambayo pamoja na mambo mengine iliifuta Tanganyika. Akichambua kitabu cha '50 Years of Independence: A Concise Political History of Tanzania' (Miaka 50 ya Uhuru: Historia fupi ya Tanzania), kilichoandikwa na Msekwa na kuchapishwa Januari mwaka huu, Lissu alisema:
"Msekwa anasema katika kitabu hicho kuwa amri hiyo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali la siku hiyo. Kwanza, iliwabadilisha waliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano."
Alisema hata Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Tanganyika iligeuzwa kuwa nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.
Alisema tarehe hiyohiyo, Mwalimu Nyerere alitoa amri ya Katiba ya muda ya mwaka 1964 na ilitangaza kuwa Katiba ya Tanganyika ndiyo iwe Katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano.
"Kifungu cha nne cha amri hii ndicho kilichoipatia Serikali ya Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano yote na vilevile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika," alisema Lissu huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo.
Alisema Juni 15, 1964, Mwalimu Nyerere alitoa amri nyingine iliyoitwa 'Amri ya Masharti ya Mpito' ambayo ilieleza kwamba mahali popote ambako sheria zilizokuwapo zimetaja jina la 'Tanganyika' basi jina hilo lifutwe na badala yake jina la 'Jamhuri ya Muungano' liwekwe.
Huku akimnukuu Msekwa, Lissu alisema kigogo huyo wa CCM katika kitabu chake amesema, "Uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla za amri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndiyo ilikuwa Tanganyika lilitolewa uhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu hata jina la eneo la kijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwa Tanzania Bara."
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lissu aliyoitoa jana, Msekwa alisema: "Kitabu kipo na ukikisoma kwa umakini utagundua kuwa alichokisema Lissu siyo ambacho kimeandikwa. Sasa umhoji kuhusu hayo aliyoyasema, muulize ameyapata wapi?"Kuhusu Shivji

Saturday, April 12, 2014

MVUA ZAENDELEA KUHATARISHA MAISHA YA WAKAZI WA JIJINI DSM

20140411 162238 15917
Hapa ni makutano ya Barabara ya Morogoro na Lumumba ambapo ujenzi wa Barabara umekamilika lakini tatizo la kujaa kwa maji linaendelea.
20140411 162445 ba299
Upepo mkali uliangusha baadhi ya Miti.
20140411 163130 b2631
Hali ya maji katika bonde la msimbazi,  serikali imeiifunga barabara ya Morogoro kutoka magomeni hadi Faya, kutokana na maji kuvuka kima cha Daraja la Jangwani.
20140411 163133 71f43
(Picha na

NYATI, TAZAMA ALIVYOMJERUHI SIMBA

Documentaries have made us believe that lions and lionesses are invinciblehuntingdown wild animals as they wish.Perhaps that’s true to some extent, but this lioness at the Governors Camp in Maasai Mara has a story to tell.
Siena was injured badly on her left lower flank on Friday by a buffalo horn. The wound was deep with the skin sheath being fleeced but luckily no perforations to the stomach wall or any bone dislocation.
She was found by a driver on Friday morning, who immediately alerted the rangers. A vet was flown from David Sheldrick Wildlife foundation in Nairobi, and treatment started that afternoon.
The lioness was treated and stitched in an operation that took one and a half hours. She’s now doing quite well, and should be back hunting soon. Incredible

HISTORIA YA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TANZANIA...

Na Mabantanyau
Edward Moringe Sokoine alizaliwa tarehe 1 Agosti 1938 alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania tarehe 13 Februari 1977 hadi tarehe 7 Novemba 1980 tena akawa Waziri mkuu toka tarehe 24 February hadi tarehe 12 Aprili 1984.
Alikuwa ni mtu aliyepanda usawa kwa kila mtu aliamini kila mtu anaweza kuwa na maendeleo kama akijituma katika kilimo na sehemu alipo pamoja na kujitegemea akiwa ni wakala wa mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu na mwaminifu.
Alizaliwa Monduli Mkoani Arusha Tanzania, alipata elimu ya msingi na sekondari katika miji ya Monduli na Umbwe toka mwaka 1948 hadi 1958.
Mwaka 1961 alijiunga na chama cha TANU baada ya kuchukua masomo katika Uongozi nchini Ujerumani 1962 hadi mwaka 1963.
Aliporudi kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Masai.
Mwaka 1967 alikuwa naibu waziri wa mawasiliano, usafiri na kazi.
Hatua nyingine katika maisha yake alijitangaza mpaka kuwa Waziri Mkuu 1970.Mwaka 1972 aliamia kwenye Waziri wa usalama.
Mwaka 1975 alichaguliwa kwenye Bunge tena wakati huu kupitia Monduli.Miaka miwili baadae akawa mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), 1977 alianza muhula wa kwanza ofisini akiwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.
Muhula huu ulidumu hadi 1981, baada ya kutulia kwa kipindi cha mwaka alikuwa tena Waziri Mkuu tena mwaka 1983, alikaa mwaka mmoja ofisini mpaka alipofariki Aprili 1984 kwa ajali ya gari. Kuna Chuo Morogoro Tanzania kinaitwa jina lake (Sokoine University Of Agriculture (SUA) kilianza mwaka 1984 kama chuo cha kilimo kinachotoa diploma katika kilimo.
Chuo hicho kikaongezwa hadi kutoa mchepuo wa kilimo mwaka 1969 chini ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.