Monday, December 29, 2014

TIMU MASHABIKIIIII NI MSEMO SAHIHI KABISA

Shabiki huyu alikuwa kivutio kikubwa kwenye mechi baina ya Mbeya city na Ndanda fc
Shabiki huyu katoka Mtwara kuishabikia timu yake ya Ndanda.

NYALANDU ATAKA KUWANIA URAIS 2015

Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM",

Sunday, December 7, 2014

IDRISS SULTAN ASHINDA SHINDANO LA BIGBROTHER....

1_7ebc0.jpg
IMG-20141207-WA0091_f9182.jpg
Idriss Sultan Mtanzania aliyetikisa Bigbrother leo ameibuka mshindi wa shindano hilo na kuwabwaga washiriki kutoka mataifa mbalimbali yaliyoshiriki katika shindano hilo akiibuka na kitita cha shilingi milioni 500 za Kitanzania katika shindano hilo lililokuwa likiendelea kwa miezi mitatu nchini Afrika Kusini Idriss ni Mtanzania wa tatu kushinda shindano hilo akitanguliwa na Mwisho Mwampamba na Richard wote wakiwakilisha vizuri taifa la Tanzania katika shindano hilo, Mabantanyau blog inampa hongera sana Idriss kwa ushindi huo na inamtakia kila mafanikio katika maisha yake

Saturday, September 13, 2014

MAYWEATHER ASHINDA PAMBANO LAKE DHIDI YA MADINA LEO ALFAJILI



Mayweather v/s Maidana

Mayweathet ashinda pambano lake la ubingwa wa WBC/WBA welterweight championship ambao umemalizika Alfajili ya kuamkia jumapili Sept 14 2014 leo.Mayweather ameshinda pambano lake hilo kwa point dhidi ya mpinzane wake Maidina japo pambano lilikuwa kali sana na kusisimua.Lilikuwa na laundi kumi na na mbili na zimeisha zote bila matatizo ingiwa katika raundi kama ya tisa hivi Madina alikatwa point  baada ya kumpiga kwa kiwiko na kumsukuma mayweather na kudondoka chini na refa wa mchezo huo kuamuru Madina kukatwa point kwa kosa hilo.
MWANDISHI:MABANTANYAU FAMILY

Wednesday, September 10, 2014

MIFUPA YA DINOSARIA YAPATIKANA HUKO MKOANI RUKWA TANZANIA

mifupa db4e2
Aina mpya ya dinosaria imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania. Mabaki hayo ya dinosaria yaliyopewa jina la - Rukwatitan Bisepultus - yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi mwa nchi hiyo. Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka mia moja iliyopita, na alikuwa na uzito sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita mbili. Mnyama huyo ni aina ya titanosaurus -- ambao ni wakubwa, na wanaokula nyasi. Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chaki iliumbika) takriban miaka milioni mia moja na arobaini iliyopita

NYANGUMI ALIYEKUFA AIBUKIA PWANI YA MTWARA

Mzoga wa samaki aina ya nyangumi ukiwa katika pwani ya Bahari ya Hindi mkoani Mtwara baada ya kuvutwa ukielea majini na wavuvi wa Kata ya Msangamkuu. Mzoga huo una urefu wa futi 48 na uzito unaokadiriwa kuwa zaidi ya tani 30.
Wananchi kutoka katika Kata ya Msangamkuu, Mtwara wakishuhudia mzoga huo.GPL(P.T)
Wakazi wa Mtwara wakiukata mzoga huo

PROFESA JAY (NIGGA J) KUZINDUA VIDEO ZA KIPI SIJASIKIA NA 3 CHAFU J'MOSI HII

Wednesday, September 3, 2014

CONTINHO NA JAJA KUONYESHA VITU VYAO UWANJA WA TAIFA LEO JIONI DAR

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgDGb-LS-MhaBAUcuGu2GZshDaGa5ays7COLjD15RfAOBp4T-nlnUsdwm65R5GaUPQ2zlYi2PqF_7M1zbHG7bXmFti_-HyjDD2cVdm4TPOfwkPx_7QK8H-94-jbqD2yZ4BGgaP1V3XZ8gz8/s1600/COUTINHO+NA+JAJA.jpg

Na MABANTANYAU FAMILY
Timu ya soka ya Yanga siku ya leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Thika United ya nchini Kenya,kwenye mchezo wa kujipima ubavu.
Mchezo huo ni maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara, ambayo inatarajia kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu. Maandalizi ya mchezo huo tayari yamekwisha kamilika,huku timu hizo zikitarajiwa kutoa burudani kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania.
Kumekuwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili,zikijinasibu kushinda mchezo huo.Huu ni mchezo wa nne wa kocha Marcio Maximo tangu achukuwe mikoba ililoachwa wazi na kocha Hans Der Plujim ambae alifungashiwa virago.Kwenye michezo mitatu ya mwanzo timu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi kwenye michezo yote .
Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.Continho,jaja kuonyesha vitu uwanja wa taifa leo
Timu ya soka ya Yanga siku ya leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Thika United ya nchini Kenya,kwenye mchezo wa kujipima ubavu.
Mchezo huo ni maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara, ambayo inatarajia kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu. Maandalizi ya mchezo huo tayari yamekwisha kamilika,huku timu hizo zikitarajiwa kutoa burudani kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania.
Kumekuwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili,zikijinasibu kushinda mchezo huo.Huu ni mchezo wa nne wa kocha Marcio Maximo tangu achukuwe mikoba ililoachwa wazi na kocha Hans Der Plujim ambae alifungashiwa virago.Kwenye michezo mitatu ya mwanzo timu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi kwenye michezo yote .
Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.Continho,jaja kuonyesha vitu uwanja wa taifa leo
Timu ya soka ya Yanga siku ya leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Thika United ya nchini Kenya,kwenye mchezo wa kujipima ubavu.
Mchezo huo ni maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara, ambayo inatarajia kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu. Maandalizi ya mchezo huo tayari yamekwisha kamilika,huku timu hizo zikitarajiwa kutoa burudani kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania.
Kumekuwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili,zikijinasibu kushinda mchezo huo.Huu ni mchezo wa nne wa kocha Marcio Maximo tangu achukuwe mikoba ililoachwa wazi na kocha Hans Der Plujim ambae alifungashiwa virago.Kwenye michezo mitatu ya mwanzo timu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi kwenye michezo yote .
Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.

GARI LA RAIS WA KENYA LAPATIKANA UGANDA BAADA YA KUIBIWA



Msemaji wa Rais alikana kuwa gari hilo lilikuwa limeibwa
Maafisa wakuu kutoka shirika la polisi wa kimataifa, Interpol amethibitisha kuwa gari la ulinzi wa rais Uhuru Kenyatta lililoibwa mjini Nairobi wiki jana limepatikana nchini Uganda.
Kwa sasa gari hilo limepelekwa mjini Kampala.
Gari hilo aina ya BMW liliibwa siku ya Jumatano usiku mjini Nairobi. Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na wizi huo.
Mkurugenzi wa polisi wa kimataifa Interpol nchini Uganda Assab Kasingye aliambia BBC kuwa gari hilo litarudishwa Nairobi.
Gari hilo liliibwa na watu waliokuwa wamejihami Jumatano wiki jana.
Hata hivyo msemaji wa serikali Manoah Esipisu alikanusha habari hizo akisema kuwa gari lililoibwa halikuwa na ulinzi wa Rais Kenyatta bali lilikuwa gari kuu kuu la polisi.
Lakini lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi aliyeripoti kuwa gari hilo ni mmoja ya magari ya ulinzi wa Rais.Afisa huyo wa polisi pia alisemekana kuwa mmoja wa maafisa wa polisi wa ulinzi wa Rais.
Tukio la wizi wa gari hilo, lilisababisha taharuki miongoni mwa maafisa wa ulinzi kwa sababu magari ya ulinzi wa Rais yenyewe yanapaswa kuwa na ulinzi mkali.
Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa visa vitatu vya wizi wa magari huripotiwa mjini Nairobi kila siku.
Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi vya wizi wa magari ambapo mtu yeyote anaweza kuathirika.

Monday, August 18, 2014

KWA MUONEKANO TU NCHI YA DUBAI IMEKATAA MTU HUYU KUINGIA NCHINI HUMO

Uso wake Rolf Bushholz ulivyo na maumbile kama pembe
Mwanaume mmoja kutoka Ujerumani anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu aliyetoboa zaidi mwili wake, Rolf Buchholz amekatazwa kuingia Dubai.
Rolf Buchholz, ametoboa mwili wake mara 453 ikiwemo usoni mwake na ana pembe mbili juu ya paja la uso wake.
Rolf Bushholz aliyenyimwa ruhusa ya kuingia Dubai.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa ameratibiwa kuandaa onyesho katika klabu moja mjini humo.
Bwana Buchholz alieleza BBC kuwa maafisa wakuu katika uwanja wa ndege walihofia huenda alikuwa ni '' mchawi'' .
Mtaalamu huyu wa tarakilishi alitambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness, kama mwanaume aliyetoboa mwili wake zaidi duniani mwaka wa 2012.
Rolf Bushholz katika moja ya maonyesho yake
Alieleza wanahabari wa Press News Agency kuwa hapo awali alikuwa amekubalika lakini baadaye akarejeshwa kabla ya kufika eneo la maafisa wa usafiri ndipo akarejeshwa katika ndege iliyokuwa ikielekea mjini Instabul Uturuki.
Onyesho lake katika mgahawa maarufu wa Irque le Soir ulioko katika hoteli ya Fairmont Hotel Dubai lilifutiliwa mbali.
Mdomo wake uso wake Rolf Bushholz ulivyotogwa
Maafisa wa mgahawa huo wa Fairmont Dubai wamesema kuwa walifanya chochote kadri ya uwezo wao kumuingiza Buchholz nchini Dubai lakini hawakufua dafu.
Bwana Rolf amesema kuwa mizigo yake bado iko Dubai na aliapa kwenye mtandao wa kijamii kuwa hatarudi tena katika milki za Kiarabu.
Polisi na Maafisa wa usafiri wa ndege nchini Dubai hawajazungumzia swala hilo.
CHANZO:MABANTANYAU FAMILY

KITUO CHA WAGONJWA WA EBOLA CHAVAMIWA NA MALI KUPORWA

Wafanyakazi wa afya wabeba maiti ya mgonjwa wa Ebola, Monrovia, Liberia Agosti 12, 2014
Waandamanaji nchini Liberia walishambulia na kupora mali kwenye kituo kimoja kilichowekewa karantini kwa wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.
Maafisa wanasema shambulizi lilitokea Jumamosi jioni kwenye kituo kilichopo katika mji jirani wa West Point. Wanasema kundi moja la wakazi wenye silaha, wengi wao wanaume waliokuwa na virungu, walivunja jengo na kuiba vifaa kutoka kituo cha afya ambavyo huenda vimeathiriwa na virusi vya Ebola.
Shirika la habari la Ufaransa-AFP, linawakariri wafanyakazi wa afya wa Liberia wakisema kwamba wagonjwa 20 ambao wote walifanyiwa uchunguzi na kugunduliwa wana virusi vya Ebola, pengine walikimbia baada ya shambulizi au walilazimishwa kuondoka na jamaa zao.
CHANZO:MABANTANYAU FAMILY

LIPUMBA AELEZA WANACHOKITAKA UKAWA

Wakati mchakato wa Katiba mpya unaendelea mjini Dodoma na suala la theluthi mbili likisumbua vichwa vya wengi, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuwa kura za wajumbe 14 kutoka Zanzibar ndizo zitauokoa au kuukwamisha mchakato huo.
Profesa Lipumba alikuwa kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kuhusu mustakabali wa mchakato wa Katiba baada ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia kuhudhuria vikao.
Kundi hilo lilisusia vikao Aprili 16 kwa madai kuwa Bunge lilipoteza mwelekeo kwa kuacha kujadili Rasimu ya Katiba, hasa katika suala la muundo wa serikali ya Muungano na kwamba chama tawala, CCM kiliingiza suala la serikali mbili ambalo halimo kwenye rasimu hiyo badala ya serikali tatu.
Kutokana na uamuzi wa Ukawa, ambayo inaundwa na wajumbe kutoka CUF, Chadema, NCCR Mageuzi na baadhi wa kundi la 201 kutoka taasisi mbalimbali za kijamii, kuna shaka kwamba mchakato huo huenda usifanikiwe kutokana na ukweli kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inataka uamuzi upitishwe na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Bara na idadi kama hiyo kutoka Zanzibar.
Kutokana na utashi huo wa kisheria, Profesa Lipumba alisema wana uhakika kuwa Katiba haitapita kwa kuwa wanao wajumbe 14 kutoka kundi la 201 ambao ndiyo tegemeo lao.
"Sisi tunao wabunge na wawakilishi kutoka Zanzibar wa vyama vyetu ambao hawakwenda hata kwenye vikao. Tukiwajumlisha, tunahitaji watu 14 kutokana na wale wajumbe 77 (wa Zanzibar) wa Kundi la 201 na kule tuna uhakika wa watu kama 21," alisema.
"Wapo baadhi waliokwenda kuhudhuria vikao, lakini tunajua misimamo yao. Tunajua kuna mbinu zinafanyika kuwarubuni, lakini tunawafuatilia kwa karibu."
Alisema kuwa Ukawa wana uhakika pia wa kuungwa mkono na wabunge na wawakilishi wa CCM kutoka Zanzibar katika kutetea mamlaka ya Zanzibar.
"Kama mnafuatilia mazungumzo ya Baraza la Wawakilishi, katika malalamiko ya suala la Muungano, mazungumzo ya CUF na CCM yalikuwa yanafanana na hata ule waraka uliopelekwa bungeni kutoka CCM Zanzibar ambao sasa wanaukana, unataka mamlaka tatu. Maana yake nini? Mamlaka ni Serikali," alisema Profesa Lipumba na kuongeza:
"Hata kura zitakapopigwa, CCM hawawezi kupata theluthi mbili za upande wa Zanzibar. Suala la Katiba ni suala la maridhiano."
Aitetea Tume ya Jaji Warioba
Huku akitetea uamuzi wa Ukawa kutoka nje ya Bunge la Katiba, Profesa Lipumba ametaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na rasimu iheshimiwe kwa kuwa imefanya kazi kubwa.
CHANZO:MABANTANYAU FAMILY

MAUWAJI YA ALBINO YAENDELEA HUKO TABORA

kamanda-suzan-kaganda_300_179_cad4c.jpg
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, 
Suzan Kaganda
MATUKIO ya kukata viungo vya walemavu wa ngozi (albino), yameendelea mkoani hapa, ambapo juzi mlemavu wa pili katika muda usiozidi wiki mbili, amekatwa kiwiko cha mkono wake na wahusika kutoweka nacho kusikojulikana.
Suzana Mungi (35) ambaye ni mlemavu wa ngozi na mkazi wa Kijiji cha Buhelele kata ya Nsimbo wilayani Igunga, amekatwa kiwiko cha mkono wake na wahusika kutoweka nacho kusikojulikana.
Katika tukio hilo lililofanyika juzi, mume wa Suzana, Mapambo Mashili ameuawa kikatili kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kifuani na kichwani wakati akijaribu kumnusuru mkewe asikatwe mkono wake.
Hivi karibuni mtoto Upendo Sengerema (15), mkazi wa Kijiji cha Usinge, Kata ya Uganza Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, alikatwa mkono na wahalifu ambao walikimbia nao. Mpaka sasa Upendo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo mkoani hapa.
Akizungumzia tukio hilo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, alisema kitendo hicho ni cha kinyama, ambacho hakiwezi kuvumiliwa na mtu yeyote.
Alisema watu wote watakaobainika kufanya unyama huo, watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo visivyokuwa vya kistaarabu.
Aidha, aliwataka wakuu wa wilaya zote mkoani hapa, kutambua maeneo yote ambayo wanaishi walemavu wa ngozi na kuwa karibu nao kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wao kila siku katika maeneo wanayoishi.
Dau la RC Mkuu wa huyo wa Mkoa, ametangaza dau la Sh 500,000 kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa za kupatikana kwa wahalifu wanaojihusisha na matukio hayo.
Pia, Mwassa aliliagiza Jeshi la Polisi mkoani Tabora, kuhakikisha waliofanya matukio hayo, wanakamatwa na kutiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzana Kaganda, aliwataka wakazi wa Mkoa wa Tabora, kuachana na imani za kishirikina na kueleza kuwa atahakikisha wahusika wanakamatwa.
CHANZO:MABANTANYAU FAMILY

JK AITISHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA CCM

Rais Jakaya Kikwete
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu kitakachofanyika Dodoma kesho.
Habari za uhakika zilizopatikana Dar es Salaam jana, zinasema moja ya ajenda kubwa inayoweza kutawala kikao hicho ni mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba ambalo limesusiwa na wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Kwa muda sasa Ukawa wamekuwa wakimtaka Rais Kikwete aliahirishe Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma, kwa kile wanachodai kutotendewa haki.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya CCM kililiambia MTANZANIA kuwa kikao hicho cha siku moja kitajadili masuala mbalimbali likiwamo kufuatilia mwenendo wa makada wa chama hicho ambao katika siku za hivi karibuni kwa namna moja au nyingine wanadaiwa kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"Nakwambia hakuna mjumbe hata mmoja anayejua nini kinakwenda kujadiliwa, Rais Kikwete amekwenda na siri nzito moyoni...tusubiri tuone nini kitatokea Dodoma.
"Hata hivyo, ajenda kubwa itakuwa uamuzi mpya juu ya hatima ya sasa ya Bunge Maalumu la Katiba ambalo mwenendo wake umekuwa ukilalamikiwa na wengi," kilisema chanzo hicho kutoka ndani ya CCM Makao Makuu.
Chanzo hicho kilisema kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM kilichoanza juzi mjini Dodoma kufuatilia mwenendo wa makada sita waliopewa adhabu ya mwaka mmoja kwa kuanza kampeni za kuteuliwa kuwania urais kabla ya wakati. Kikao hicho kitatoa taswira na mwelekeo mpya ndani ya CCM.
Uamuzi wa Rais Kikwete kuitisha CC unatokana na uamuzi wa Kamati Kuu iliyoketi Julai 16 mwaka huu ambayo ilipokea taarifa za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonyesha nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais.
Kutokana na hali hiyo, CC iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao.
Julai 17 mwaka huu, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema endapo Kamati ya Usalama na Maadili ya chama hicho inayotarajiwa kukutana Agosti mwaka huu ikibaini kama makada hao walikiuka mwenendo wa utekelezaji wa adhabu waliyopewa watapoteza sifa ya kugombea.
Pamoja na adhabu nyingine, makada hao walizuiwa kujihusisha na masuala ya siasa ndani ya chama hicho kwa miezi 12, huku mienendo yao ya siasa ikifuatiliwa.
Kabla ya adhabu hiyo, makada hao waliitwa na kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ambayo iliwatia hatiani kwa kutumia Kitabu cha Kanuni ya Uongozi na Maadili ya CCM, toleo la Februari 2010, Ibara 6 (7)(i).
Nape alisema CC ilipokea taarifa za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonyesha nia ya kuomba ridhaa ya chama kugombea urais.
"Baada ya kutafakari kwa kina, kamati kuu inapenda kuwakumbusha kuwa ili wasipoteze nia ya kugombea ni muhimu wakazingatia katiba, kanuni na taratibu za chama zinazosimamia masuala hayo," alisema Nape.
Alisema kama itabainika makada hao hawakutekeleza masharti ya adhabu zao kama zilivyotolewa na CC, kuna hatari ya kuongezewa adhabu kulingana na ukubwa wa uvunjaji wa masharti ya adhabu husika.
"Kila mmoja anafuatiliwa mwenendo wake; kuhusu wale waliopewa adhabu na Kamati Kuu kutokana na kukiuka baadhi ya taratibu za chama kwa suala hili, Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama itafanya mapitio ya mwenendo wao wa utekelezaji wa adhabu hiyo.
Kama watakuwa hawajatekeleza adhabu zao kamati itapeleka mapendekezo CC waweze kuongezewa adhabu kulingana na ukubwa wa makosa yao na taratibu za chama," alisema Nape.
Alisema ni muhimu kwa wanachama wote kukumbuka chama ni pamoja na katiba, kanuni na taratibu zake, hivyo kutoziheshimu na kuzifuata ni kukivuruga jambo ambalo halivumiliki.
Alisema nia ya CCM ni kusimamia na kuhakikisha chama kinakuwa na umoja na mshikamano ambao ni muhimu hasa katika kuelekea kukamilisha kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010/2015 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Hoja ya kuendelea kufuatiliwa kwa makada hao ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, PhilipMangula, aliyesema amefungua jalada kwa ajili ya makada hao.
Suala jingine alilowasilisha Mangula ni ripoti ya ziara yake aliyoifanya katika mikoa ya Tabora na Kigoma na Tanga.
Februari 18 mwaka huu, CCM kupitia Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu katika kikao chake ilipendekeza kuchukuliwa hatua za nidhamu kwa makada wake ambao wameanza kampeni ya kuwania urais wa mwaka 2015.
Uamuzi huo ulibarikiwa na Kamati Kuu iliyokutana Februari 17, mwaka huu mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.
Makada waliopewa adhabu ya mwaka mmoja kwa tuhuma za kuanza kampeni za kuwania urais kabla ya wakati ni Naibu Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
MTANZANIA lilimtafuta Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye hakupatikana kwenye simu yake ya kiganjani na muda wote ilikuwa imezimwa.
Hata hivyo, ofisa wa CCM Idara ya Uenezi alipoulizwa kuhusu kikao hicho cha CC alisema hana taarifa zozote kuhusiana na kikao hicho.
"Mimi sina lolote ninalolijua kwa sasa labla kwa kuwa nipo kwenye mapumziko acha nifuatilie taarifa zaidi. Lakini ninachojua hakuna kikao chochote kwa sasa," alisema ofisa huyo.
CHANZO:MABANTANYAU FAMILY

Wednesday, July 30, 2014

MAN U YAENDELEZA TENA WIMBI LAO LA USHINDI

article-2710210-201DD49500000578-25_634x414
Shinji Kagawa, Darren Fletcher na Tom Cleverley, wafungaji wanne wa penati za United, wakishangilia ushindi wao wa penalti 5-3 dhidi ya Inter Milan.


article-2710210-201DD4F500000578-474_634x417
Fletcher akishangilia ushindi na kipa wa United David De Gea baada ya kushinda kwa penalti na kumpa Van Gaal rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika michuano hiyo. 
KOCHA Louis van Gaal ameendelea kufanya vizuri kufuatia Manchester United kuitandika kwa penalti 5-3 Inter Milan baada ya sare ya 0-0 katika mechi ya Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington, penati za Man United zilizamishwa kambani na Ashley Young, Javier Hernandez, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco Andreolli wa Inter aligongesha mwamba.  
ziara hiyo ya Marekana imekuwa ya mafanikio kwa Van Gaal kwani ameshinda mechi tatu mfululizo na wachezaji wake wamepata nafasi ya kumuonesha uwezo, hivyo lawama hazitegemewi.

Kocha huyo mpya wa United anaendelea kutafuta njia ya kuutekeleza mfumo wake anaoupenda wa 3-5-2.

Kwa mfano jana usiku, Man United walianza mchezo na washambuliaji wawili,  Wayne Rooney na Danny Welbeck. Walimaliza mchezo na Nani na Wilfried Zaha katika nafasi hizo.

TETESI ZA SOKA LA ULAYA NA USAJILI

Beki was Aston Villa Ron Vlaar, 29, atakuwa na mazungumzo na meneja wake Paul Lambert kuhusiana na hatma yake licha ya Southampton kumwania (Daily Mirror), QPR wanafikiria kumchukua kiungo wa Colombia Carlos Sanchez, 28, kwa pauni milioni 4 kutoka Elche (Daily Mirror),
West Ham na QPR wamepanda dau kwa Marseille kumchukua Matheiu Valbuena baada ya kiungo huyo Mfaransa kukataa kuhamia Dynamo Moscow (L'Equipe), Manchester United na Barcelona bado wanamfuatilia Juan Cuadrado, 26, wa Fiorentina lakini huenda wakatishwa na bei ya pauni milioni, 32, ya kiungo huyo kutoka Colombia (Marca),
Manchester United wamefikia makubaliano "ya mdomo" na kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, ya uhamisho wa pauni milioni 47 (Tuttosport), matumaini ya Manchester City kumsajili beki kutoka Morocco Mehdi Benatia, 27, yamefifia baada ya Roma kusema hakuna dalili za mchezaji huyo kuondoka (Le Figaro),
Meneja mpya wa Manchester United amewaonya mashabiki wake kuwa timu hiyo huenda ikasuasua katika miezi mitatu ya mwanzo wa msimu wakati wachezaji wakianza kuzoea mbinu zake (Times), Van Gaal amesema iwapo watashinda Ligi Kuu msimu ujao na kuwapiku majirani zao Manchester City, utakuwa ushindi "mtamu" zaidi (Manchester Evening News),
Kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 31, amesema huenda akasalia katika timu hiyo hadi atakapoacha kucheza soka (Guardian), mshambuliaji mpya wa Barcelona Luis Suarez, 27, ambaye anatumikia adhabu ya miezi minne, amehamia katika mji wa Pyrenees kuanza mazoezi ya msimu mpya akiwa na mwalimu binafsi (Daily Mail), Didier Drogba, 36, amesema Diego Costa, 25, atakuwa mchezaji "mkali" katika Ligi Kuu ya England (Sun), AC Milan wanafanya mazungumzo wa mshambuliaji kutoka Brazil Robinho, 30 (Le Figaro),
Kiungo wa Arsenal Santi Cazorla,29, bado anasakwa na Atlètico Madrid. Atlètico pia wanamfuatilia Fernando Torres, 30, na winga wa PSV Eindhoven Zakaria Bakkali, 18 (AS.com), kiungo anayefuatiliwa na Liverpool, Xeridan Shaqiri, 22, huenda akaamua kubakia na klabu yake ya Bayern Munich (Tuttosport), Borussia Dortmund na Schalke wanamtaka mshambuliaji kutoka Serbia, Aden Ljajic, 22, kutoka AS Roma (Bild),
Barcelona wametangaza kumsajili kiungo kutoka Brazil, Alex Varoneze Dione anayejulikana kama "Betri" kwa miaka mitatu (Mundodeportivo), Manchester United wameanza tena kumfuatilia beki wa kati wa Atletico Madrid Miranda, baada ya Atlètico kusema wapo tayari kupokea dau la pauni milioni 23 (Metro), AC Milan wanamtaka winga wa Newcastle Hatem Ben Arfa na huenda akauzwa kwa pauni milioni 12 (Daily Star),
Bayern Munich wapo tayari kusubiri hadi Oktoba kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdez ambaye anauguza jeraha la goti, ingawa anaweza kusita kwenda kugombea namba na Manuel Neuer (Mundo Deportivo),
QPR wanataka kumchukua Ronaldinho ambaye amemaliza mkataba wake na Atletico Mineiro (Globoesporte) na Chelsea wanakataa kutengeneza jezi zenye jina la kipa Thibaut Courtois, 22 na Romelu Lukaku, 22, kwa sababu wachezaji hao bado hawajapewa namba (Daily Star). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share hizi na wapenda soka wote. Cheers!!

RAISI BARACK OBAMA ATANGAZA VIKWAZO VIPYA DHIDI YA URUSI

Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kupanua uwigo wa vikwazo dhidi ya Urusi kufuatia mgogoro unaoendelea Ukraines.Tangazo hilo la Rais Obama linafuatia vikwazo vilivyotangazwa na Jumuiya ya Ulaya saa chache kabla ya hili la Marekani.
Vikwazo hivyo vilivyotangazwa Marekani imesema itaiwekea vikwazo Urusi katika maeneo ya nishati,silaha na uchumi.
Hata hivyo Rais Obama amekanusha madai kwamba vikwazo hivyo vyaweza kuanzisha vita baridi dhidi ya Urusi, bali amesema kuwa wanalenga kuhakikisha Ukraine inarejea katika hali yake na kufuatia machafuko yanayoendelea hivi sasa

Monday, July 21, 2014

GALI LILILO BEBA MIFUKO YA RAMBOILIYOKUWA NA MAITI ZAIDI YA MIA LA KAMATWA MAENEO YA BUNJU DAR ES SALAAM




NA MABANTANYAU FAMILY:



                  TUKIO HILO LIMETOKEA MIDA YA JIONI HUKOBUNJU DAR ES SALAAM

                                                                                           

Saturday, July 12, 2014

UKATILI WA AJABU:MTOTO AFICHWA UVUNGUNI KWA MIAKA 6 MOROGORO

mtoto_06305.jpg
Morogoro. Wakati jamii ikiwa bado haijasahau mateso aliyoyapata mtoto Nasra Mvungi na kusababisha  kifo chake, tukio lingine la aina hiyo limetokea katika Kijiji cha Matongola, Tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa, baada ya kubainika mtoto wa miaka sita akiwa amefichwa uvunguni mwa kitanda na kufanyiwa vitendo vya kikatili na mama yake mzazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa za mateso ya mtoto huyo zilifikishwa Kituo cha Polisi wilayani Kilosa za saa za mchana jana, baada ya uongozi wa  kijiji na kata kutoa taarifa na tayari mwanamke huyo amekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Mama aliyefanya ukatili huo anafahamika kwa jina la Sala Mazengo ambaye alimficha ndani mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Devota Malole na kumfanyia vitendo vya kikatili ikiwa pamoja na kutompa chakula, wala kumfanyia usafi.
Baada ya kufichuliwa kutoka alipofichwa, mtoto huyo alionekana kuwa dhaifu kiafya kutokana na kukosa lishe pamoja na mazingira aliyokuwa akiishi kutoridhisha, jambo ambalo ni kosa kisheria, pia ukiukwaji wa haki za watoto.
Inadaiwa kuwa tangu mwka 2009 Sala amekuwa akimficha mtoto wake huyo ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kupatiwa vipimo na matibabu.
Hata hivyo, mwanamke huyo alipoulizwa alidai kuwa afya ya mtoto wake ilikuwa mbaya tangu alipozaliwa kutokana na magonjwa ya mara kwa mara, pia hali ngumu ya maisha ilichangia kudhoofisha afya ya mtoto huyo.
Alidai kuwa ana watoto sita, pia alikiri kumlaza chini mtoto huyo kutokana na kuwa na kitanda kimoja, ambacho hakiwatoshi watoto hao.
Aliongeza kuwa hata chakula amekuwa akikipata kwa shida kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa kuwa ana mtoto mwingine mdogo.
Kamanda Paulo alisema kuwa  mwili wa mtoto huyo umedhoofu kutokana na kufichwa ndani kwa muda mrefu na bado mwanamke huyo hajaeleza sababu za kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto huyo.
“Siwezi kutoa taarifa ya kidaktari, lakini kutokana na afya ya mtoto yule na mazingira tuliyomkuta ni dhahiri alikuwa akipata mateso na kufanyiwa vitendo vya ukatili. Hata hivyo, uchunguzi zaidi tunaufanya na kwamba taratibu za kumfikisha mtuhumiwa huyo Kituo Kikuu cha Polisi mkoani hapa zinaendelea,” alisema Kamanda Paulo.
Alisema kuwa mpaka sasa bado haijafahamika kama mtoto Davota ni mlemavu au la na kwamba taarifa za afya ya mtoto huyo zitatolewa baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi wa kina.

REFA WA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA HUYU HAPA

Nicola Rizzoli amechaguliwa na Fifa kuwa mwamuzi katika mchezo wa fainali - Kombe la Dunia Brazil 2014 kati ya Ujerumani na Argentina.
Howard Webb kutoka England, aliyechezesha fainali ya Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, aliorodheshwa lakini hakuchaguliwa.
Ujerumani itapambana na Argentina kwenye dimba la Maracana, jijini Rio De Janeiro, siku ya Jumapili Julai 13.
Rizzoli ni msanifu majengo kutoka Bologna, na tayari amechezesha mechi tatu katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 42 alichezesha mechi kati ya Spain dhidi ya Uholanzi, Nigeria na Argentina na Argentina ilipocheza na Ubelgiji.
Rizzoli pia alichezesha mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa kati ya Atletico Madrid dhidi ya Fulham mwaka 2010, na pia mchezo wa fainali ya Uefa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2013 kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Rizzoli atasaidiwa na waamuzi wa pembeni Renato Faverani na Andrea Stefani, na mwamuzi wa nne atakuwa Carlos Vera kutoka Ecuador.
Rizzoli atakuwa mwamuzi wa tatu kutoka Italy kuchezesha fainali, baada ya Sergio Ginella mwaka 1978 na Pierluigi Collina mwaka 2002.

UINGEREZA WAANZA KUJADILI MSWADA WA KUJIUA

Bunge la mabwana nchini Uingereza
Askofu mkuu wa zamani wa Cantebury Lord Carey amesema kuwa ataunga mkono sheria ambazo zitahalalisha watu wanaougua kupitia kiasi nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujiua.
Katika taarifa yake ndani ya gazeti la Daily Mail Lord Carey ameondoa pingamizi yake dhidi ya mswada huo kufuatia hali inayowakumba watu wanaougua.
Lakini Askofu mkuu wa Cantebury anayehudumu kwa sasa Justin Welby ameutaja mswada huo kama ulio na makosa na hatari kubwa.
Wabunge wataujadili mswada huo siku ya ijumaa.
Mswada huo uliowasilishwa na mbunge wa chama cha leba Lord Falconer utawapa fursa watu wazima nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujitoa uhai.
Fursa hiyo itashirikisha wale walio na chini ya miezi sita kuishi.
Madaktari wawili watalazimika kuthibitisha iwapo mgonjwa anaugua kupitia kiasi na kwamba wameafikia uamuzi wao wenyewe wa kujitoa uhai.
Takriban wabunge 110 wameorodheshwa kuzungumza wakati bunge litakapojadili mswada wa wanachama binafsi siku ya ijumaa.
Wakati Askofu Lord Carey alipokuwa Askofu mkuu wa Cantebury, alikuwa miongoni mwa watu waliopinga mswada wa Lord Joffes wa kuwasaidia wagonjwa wanaougua kupitia kisia kujitoa uhai ambao ulipingwa katika bunge la mabwana mnamo mwaka 2006.
Anasema kuwa inawezekana kuwa mcha mungu na vilevile kuwasaidia wale wanaotaka kujitoa uhai.
lakini katika taarifa yake hii leo katika gazeti la Daily Mail Lord Carey alisema ''ukweli ni kwamba nimebadilisha uamuzi wangu''.

Thursday, July 3, 2014

LIVERPOOL KUMUACHIA SUAREZ KWENDA BARCA AMA?

Huenda Luis Suarez akaichezea Barcelona msimu ujao,
Kaimu mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre aliutumia muda wake mwingi kwa majadiliano na maafisa wa juu wa Barcelona siku ya jumatano jijini London.

Liverpool imeshikilia msimamo wake kuwa Suarez 27, hatauzwa kwa kiwango cha chini ya kile wanachokihitaji kumuachia mchezaji huyo kinachoaminiwa kuwa kati ya Pauni milioni 70 na 80.

Afisa mmoja wa Liverpool ameiambia BBC kuwa mazungumzo yalizaa matunda na kuwa pande zote zina matarajio chanya. bado hawajafikia makubaliano hata hivyo mazungumzo zaidi yataendelea.
Suarez, aliyejiunga na Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 22.7 kutoka Ajax na ambaye amebakisha miaka mine kuichezea timu hiyo kwa mujibu wa mkataba wake, anatumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi mine baada ya kumng'ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini katika mechi ya kombe la dunia