Monday, December 29, 2014

NYALANDU ATAKA KUWANIA URAIS 2015

Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM",

No comments:

Post a Comment