Friday, March 21, 2014

TAZAMA PICHA ZINGINE 8 JINSI AJALI YA LORI LILILOGONGA MAGARI 5 UBUNGO MCHANA LEO


 Basi la UDA likiwa limebebwa kwa juu katika eneo la tukio
 
 
 
 
 
Ajari mbaya iliyo husisha magari takribani 5 imetokea maeneo ya ubungo mkabala na stendi ya mabasi ya mikoani ikihusisha magari ya abiria uda na gari zingine ndogo mpaka sasa haijajulikana idadi sahihi ya watu walio poteza maisha

AJALI MBAYA YATOKEA KITUO CHA MABASI UBUNGO LEO









Ajali mbaya imetokea muda mfupi uliopita kituo cha Ubungo lango kuu la kuingilia mabasi yatokayo mikoani. Ajali imehusisha magari 6 likiwemo UDA. Lori lafeli break na kusababisha uharibifu Mkubwa wa Magari na watu kuumia vibaya sana kituo cha Mabasi Ubungo. Magari kibao yafinyangwa. Mpaka sasa haijajulikana idadi ya watu waliopoteza maisha.

Kuhusu kuonekana Australia kwa vipande vya ndege ya Malaysia iliyopotea.


Screen Shot 2014-03-21 at 3.36.25 PM
March 20 2014 Waziri mkuu wa Australia alitangaza bungeni kwamba nchi yake kupitia picha za satellite imeona vipande kwenye bahari ya hindi ambavyo vinaaminika kuwa mabaki ya ndege ya Malaysia iliyopotea ikiwa na abiria 239 March 8 2014.
Saa kadhaa baada ya
hizo taarifa kutoka, ilitangazwa kwamba vikosi vya uokoaji vimeshindwa kufika kwenye eneo hilo la tukio baharini kutokana na hali mbaya ya hewa iliyochangiwa na mvua.
Leo March 21 2014, taarifa kutoka vyombo vikubwa mbalimbali vya habari duniani, imefahamika hakuna kilichoonekana eneo la tukio kwenye bahari ya hindi ambako ‘ilisemekana’ vipande vya ndege hiyo iliyopotea vimeonekana hivyo vikosi vya uokoaji vimeondoka eneo hilo.

PICHA ZA MOTO ULIOTEKETEZA SEHEMU YA HOTELI YA PICOLO BEACH

Pichani juu ni taswira za sehemu ya Hoteli ya Pecolo Beach iliyopo Kawe jijini Dar iliyoteketea kwa moto leo mchana. Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyoanzia kwenye nguzo iliyopo jirani na hoteli hiyo

PISTORIUS KUUZA NYUMBA YAKE YA KIFAHAR

Nyumba ya kifahari ya Oscar Pistorius
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorious atauza nyumba yake ili aweze kumudu gharama ya kesi ya mauaji inayomkabili.
Hii ni kwa mujibu wa wakili wake Brian Webber ambaye amenukuliwa na Shirika la Wanahabari La Afrika Kusini (SAPA) akisema kesi hiyo itaendelea kwa zaidi ya wiki tatu zilizotarajiwa kwa kesi hiyo kukamilika.
Oscar hajaweza kurejea katika nyumba yake hata baada ya maafisa wa uslama kumruhusu arejee huko zaidi ya mwaka mmoja uliopita huku uamuzi ukitolewa wa nyumba ile kusalia ikiwa imefungwa hadi pale kesi hiyo itakapo kamilka.
Kwa Mujibu wa SAPA, hati za kortini zilizoandikishwa mwaka jana wakati mwanariadha huyo alipokuwa akiwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana zaonyesha kuwa nyumba hiyo iliyo katika mtaa wa Silverwoods ina thamani ya Randi millioni 5 ambazo ni sawia na dola za marekani 457 000.
Oscar anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake mnamo tarehe 14 mwezi wa Februari mwaka jana huku akisema kuwa alimpiga risasi kimakosa.
Kesi ya mauaji dhidi yake ambayo kwa sasa iko katika wiki ya tatu, imehairishwa hadi siku ya jumatatu ambapo mashahidi wengine watano wa upande wa mashitaka wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kabla ya yeye kupewa fursa ya kujitetea.
Upande wa mashitaka unadai kuwa Pistorious alimpiga risasi Bi Steenkamp, aliyekuwa mwana mitindo, mtangazaji maarufu wa runinga na mwana sheria baada ya kinachodahniwa kuwa ugomvi wa nyumbani.
Huku kwa upande wake, Pistorious akisema kuwa aliamini kuwa mpenzi wake alikuwa amelala na akidhani kuwa palikuwa na mwizi nyumbani kwake alifyatua risasi kuelekea chooni asubuhi mapema mnamo tarehe 14 februari mwaka 2013.
Iwapo mwanariadha huyu mwenye umri wa miaka 27 atapatikana na hatia , huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha

Wednesday, March 12, 2014

Picha nne za tukio la Ajali ya Basi la Hood

Basi la Kampuni ya Hood likiwa limepinduka na watu kuumia vibaya Same,Kilimanjaro chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.


Kuhusu kesi ya Mramba na Yona,hiki ndicho kilichoamuliwa na Mahakama leo.


BASIL YONA
Leo March 11 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi  Mawaziri Waandamizi wa zamani ambao ni Basil Mramba na Daniel Yona wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
Matumizi hayo mabaya ya madaraka yanadaiwa  kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7  kwa kutoa msamaha wa kodi.
Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji John Utamwa baada ya washtakiwa hao kuwasilisha maombi ya kwenda kutibiwa nje ya nchi ambapo Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na maombi hayo.
Baada ya kusikiliza ombi hilo Jaji Utamwa alisema
mahakama inawaruhusu washtakiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kutibiwa na kwamba pamoja na ruhusa hiyo amewataka Mramba na Yona kuwepo mahakamani siku ya kusikiliza kesi hiyo Aprili 22 mwaka huu.
Katika kesi hiyo inayowakabili Mramba na Yona piamshtakiwa mwingine ni Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha Gray Mgonja,Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Aprili 22 hadi 25, mwaka huu.
Katika kesi ya msingi washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.
Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation  waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
YONA+CHRGE+2
YONA+CHRGE

Matokeo ya UEFA Usiku wa leo Jumanne na Waliofunga hawa hapa

Mapya na Mazito kuhusu Kesi ya Babu Seya na Wanaye haya hapa,Duhhh hatari

WAKILI maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando amesema mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake watatu walimbambikiwa kesi.


Mabere Nyaucho Marando akiongea na waandishi 
Akizungumza na waandishi wa habari wa Global Publishers katika ofisi zao zilizopo Mwenge Bamaga mwishoni mwa wiki iliyopita, Marando alisema alipitia jalada la kesi hiyo lenye kurasa 1,362 na kugundua kuwa hakuna hata sehemu moja inayomhusisha kigogo mmoja wa nchi, lakini kesi walikuwa wamebambikiwa.
Hakutaja waliombambikia. Baadhi ya mahojiano ya Marando na waandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Wewe uliwatetea Babu Seya na watoto wake, unaweza kutueleza ilikuwaje ukatafutwa wewe kuwatetea?
Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
Marando: Kuna rafiki yangu alikuja kuniomba nifanye kazi ile, nilikataa hasa kwa kuwa nami nina watoto wa kike. Baadaye nilikubali kwanza kusoma jalada la kesi lenye kurasa 1,362 nikaona hawakufanya makosa waliyoshitakiwa, walibambikiwa nikaamua kuwatetea katika ngazi ya rufaa, niliwatetea bure kabisa.
Mwandishi: Kama hivyo ndivyo, ina maana makosa walibambikiwa?
Marando: Ndiyo, naamini makosa yale walibambikiwa lakini siyo na kigogo yeyote wa serikali katika nchi hii. Lakini Mahakama ya Rufaa haina makosa, Babu Seya na wanawe walikuwa wamehukumiwa na magazeti. Nyinyi waandishi mlimhukumu kwa hii fabricated case (kesi ya kutunga) na sababu zipo.
Mwandishi: Je, kuna njia yoyote iliyobaki ya kumtoa Babu Seya na mwanaye?
Marando: Mimi kama wakili, hapo ndiyo mwisho wangu, nimenyoosha mikono. Nimeshindwa nusu, nimeshinda nusu (Kwa kuwatoa jela Mbangu na mdogo wake Francis Nguza na kubaki jela Nguza na Papii.)
Mwandishi: Umekuwa Chadema na kuna habari kuwa uliondolewa kuwa mwanasheria wa chama akapewa Tundu Lissu,pia kuna habari kuwa umekosana na mwenyekiti wako, Freeman Mbowe, Je,  kuna ukweli wowote juu ya hayo?
Marando: Sijawahi kuwa mwanasheria wa Chadema isipokuwa wanapokuwa na tatizo la kisheria huwa nawapa ushauri wakihitaji. Mheshimiwa Mbowe sijakosana naye isipokuwa katika vikao tunaweza kutofautiana na hivyo ndivyo chama makini kilivyo. Wote hamuwezi kuwa na wazo moja katika hoja, baadaye inapigwa kura, upande unaoshinda na unaoshindwa huwa kitu kimoja. Hakuna ugomvi hapo, mimi ni Makamu  Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu.
Mwandishi: Lipo suala kuwa wewe ni usalama wa taifa na ulihusika na mauaji ya Komandoo Tamim, Je, hilo unaweza kulifafanua?
Marando: Mimi nilijiunga na usalama wa taifa na nilikuwa kitengo cha mambo ya nje hasa kuhusu vyama vya ukombozi enzi hizo. Niliacha kazi hiyo kwa kukabidhi barua kwa aliyekuwa mkurugenzi wake, Dk. Hansy Kitime baada ya kulazimishwa kujiunga na TANU kwani sikuwa mwanachama. Kuhusu Tamim aliuawa mwaka 1983 wakati huo mimi nilikuwa nimeshaacha kazi.
Hili la kuua walikuwa wakinipakazia watu wa usalama wa taifa bila shaka kwa sababu niliacha kazi kijeuri nikawa jobless (sina kazi).
Baadaye nikaajiriwa Shirika la Sheria Tanzania kabla ya kuanzisha kampuni yangu ya uwakili mwaka 1984. Nimefafanua hili mara nyingi sana, nadhani leo mmenielewa na Watanzania watanielewa

Breaking news ya Radio One kuhusu waliokamatwa kituo cha mabasi Ubungo.


Screen Shot 2014-03-12 at 1.51.39 AM
Screen Shot 2014-03-11 at 11.35.01 PM

Huu ndio Mkoko Wa Samwel Etto ambao Kwa Wachezaji yeye Pekee anamiliki,Ni Balaa


Screen Shot 2014-03-12 at 2.55.30 AM 
Hili ni moja ya magari ambayo tumezoea kuyaona kwenye video za muziki za gharama kubwa lakini pia hata kwenye baadhi ya movie za Hollywood.
Unaambiwa hili ni moja ya magari ya kifahari anayomiliki staa wa soka Samuel Eto’o ambae anaichezea Chelsea sasa hivi huku akitajwa kuwa staa wa soka anaeshika namba 3 kwa utajiri duniani akiwa nyuma ya Ronaldo anaeshika namba 1, na Lionel Messi anaeshika namba 2.
Hizi ni baadhi tu ya pichaz kutoka kwenye video yenyewe hapojuu ambayo ndio unaweza kulitazama hili gari vizuri hata kumuona yeye mwenyewe akiliendesha.
Screen Shot 2014-03-12 at 2.55.44 AM
Screen Shot 2014-03-12 at 2.56.15 AM
Screen Shot 2014-03-12 at 2.57.03 AM

JK ATANGAZA KULA SAHANI MOJA NA MAJANGILI

Wawakilishi wa Chama cha Uhifadhi wa Wanyama cha Frankfurt (FZS), wakikabidhi magari zaidi ya 11 kwa Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusaidia vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori katika hifadhi na mbuga za taifa.Picha na Ikulu
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imenuia kumaliza kabisa ujangili nchini, ikiwa ni hatua ya kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.
Hakusita kusisitiza kwamba, nia ya dhati ya Serikali ni kuhakikisha mkakati huo unakamilika, japokuwa kumekuwa na changamoto zinazotokana na ukubwa wa hifadhi hizo na uhaba wa vitendea kazi pamoja na askari wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa kupokea magari 11 ya kisasa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili kutoka kwa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la Ujerumani, Kikwete alisema tatizo hilo limekuwa la muda mrefu, lakini juhudi za kulikomesha zinafanyika.
Alisema, pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna tatizo la uhaba mkubwa wa wafanyakazi wanaotakiwa kudhibiti majangili, ambapo kwa sasa kuna wafanyakazi 1,155 sawa na asilimia 24 tu ya mahitaji halisi ya wafanyakazi 4,000 wanaohitajika.
"Mwaka uliopita, Serikali ilisimamia ajira ya wafanyakazi 449 na sasa kuna ajira ya wafanyakazi 500.
Kwa maana hiyo tutafikisha wafanyakazi wapya 949 na kufanya mahitaji ya wafanyakazi wapya kuwa 4,000 zaidi ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu kwa viwango vya kimataifa," alisema.
Kwa mujibu wa viwango vilivyopo sasa, mfanyakazi mmoja anasimamia eneo la kilometa za mraba 169 ikilinganishwa na viwango vya kimataifa vya kilometa za mraba 25 kwa kila mfanyakazi mmoja.
Rais Kikwete alisema kwa sasa Serikali itaendelea kuajiri idadi hiyo ya wafanyakazi kila mwaka kwa miaka mitatu ijayo ili kuhakikisha pengo lililopo linazibwa.
Alisisitiza kuwa, kampeni dhidi ya ujangili ni suala la kimataifa na Tanzania au nchi zilizoathirika hazitaweza kulikabili bila ushirikiano wa kimataifa.
Alisema upo ulazima wa kuteketeza mitandao yote ya ujangili na kuwawajibisha ipasavyo watakaonaswa, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kulinda urithi huo wa dunia.
Ukosefu wa vifaa
Akifafanua, Rais Kikwete alisema kuongeza idadi hiyo ya wafanyakazi pekee haitakuwa na maana iwapo hawatakuwa na vifaa maalumu vya kisasa vitakavyowawezesha kukabiliana ipasavyo na tishio la ujangili.
Katika mkakati wa maboresho hayo, Kikwete alisema wanafanya jitihada za kuongeza idadi ya magari, kuongeza vifaa vya kisasa kwa ajili ya doria na vifaa vya mawasiliano, ambavyo vinahitaji uwezo mkubwa wa kifedha ambao utaweza kutekelezwa na serikali kwa kipindi kirefu iwapo haitapata msaada wa uwezeshaji kutoka kwa wadau.
Msimamo wa Wizara
Akizungumzia msimamo na mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Waziri Lazaro Nyalandu alisema kutokana na ukubwa wa tatizo, wanahitaji vifaa vya kisasa zaidi, ikiwamo helikopta na ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kufanya doria kwenye maeneo yote ya mbuga na hifadhi za taifa.
Aliwatahadharisha wafugaji wanaopenda kuingiza mifugo yao kwenye maeneo ya hifadhi, akiwataka kuondoa mifugo yao mapema kwa kuwa katika operesheni hiyo hakuna atakayeachwa.
"Katika operesheni hii, hakuna jangili wala mfugaji atakayeachwa iwapo atakutwa kwenye maeneo ya hifadhi," alisema.
Alifafanua kwamba, msaada huo wa magari utapelekwa maeneo tofauti, matano kanda nane za Selous, mengine matano Hifadhi ya Serengeti na moja Hifadhi ya Maswa.
Mwaliko wa vyombo vya habari
Nyalandu alisema Wizara yake imevialika vyombo vyote vya habari vya kimataifa kwa ajili ya kuja kupata taarifa sahihi kuhusu kampeni dhidi ya ujangili zinavyotekelezwa ili kuepuka ripoti za upande mmoja kwa ajili ya kuweka usawa.
Alisema hatua hiyo ilichukuliwa na wizara yake walipokwenda kwenye mkutano maalumu na Rais Kikwete ulioandaliwa na mtoto wa Mfalme wa Uingereza, Prince Charles kwa ajili ya kuangalia namna ya kulinda wanyama walio hatarini kutoweka duniani, wakiwemo tembo na faru

Sunday, March 9, 2014

WAANDISHI WA HABARI WAZUIWA BUNGE LA KATIBA

pandu_ameir_kificho_c76f2.jpg
Bunge Maalumu la Katiba limepitisha kanuni ya kuwazuia waandishi wa habari kuingia katika vikao vya kamati za chombo hicho, hatua ambayo inaelezwa ni kinyume na Katiba inayotoa uhuru wa wananchi kupata habari.
Kanuni hiyo ilipitishwa jana baada ya malumbano makali yaliyowagawa wajumbe wa bunge hilo, baadhi wakipinga kifungu hicho kwa sababu kinavunja Katiba ya nchi inayotoa uhuru kwa waandishi kukusanya na kusambaza habari na wengine wakiunga mkono kuwazuia.
Kanuni hiyo ilipitishwa kwa mbinde huku baadhi ya wajumbe wakiendelea kushikilia msimamo wa kuikataa, hata baada ya Mwenyekiti wa Muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kuridhia kipite. Wajumbe waliopinga kanuni hiyo ni Joshua Nasari, Moses Machali, Peter Serukamba, Ezekiah Wenje na Maria Sarungi.
Baadhi ya wajumbe akiwamo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga walisimama kutaka kuzungumza lakini hawakupata fursa hiyo.
Mjumbe aliyekuwa mwiba kwa Tasnia ya Habari ni, Dk Harrison Mwakyembe ambaye aliwashawishi wajumbe kufunga mjadala huo ili wasonge mbele kwa madai kuwa hata yeye pia ni mwanahabari. "Hakuna upande usiotambua umuhimu wa vyombo vya habari katika mchakato huu... Tunachotofautiana ni jinsi na namna
ya ushiriki wa vyombo vya habari," alisema Dk Mwakyembe. Alisema Taifa limeingia katika kipindi maalumu kama cha vita na kwa msingi huo, kanuni zinabadilika kulingana na mazingira na kwamba vyombo vya habari vinapaswa kulitambua hilo.
Hata hivyo, Kifungu cha 57 (3) katika kanuni hiyo kilipita baada ya kufanyiwa marekebisho kuondoa maneno 'mwenyekiti anaweza kutoa taarifa' badala yake, ikawa 'ni lazima kutoa taarifa.'
Kanuni hiyo inampa mamlaka mwenyekiti wa kamati au mjumbe yeyote kwa idhini yake, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mambo yaliyojitokeza kwenye kikao.
Mjadala wakwama
Mvutano juu ya kifungu hicho ulianza juzi jioni wakati baadhi ya wajumbe walipotofautiana.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti, Mjumbe George Simbachawene alisema iwapo waandishi wataruhusiwa wangeweza kutoa taarifa zisizochujwa ambazo zitawachanganya wananchi.
Hata hivyo, Mjumbe wa bunge hilo, Ezekiah Oluoch alisema kisheria kanuni hiyo ilikuwa inakwenda kinyume na Ibara ya 18 ya Katiba ya nchi ambayo kimsingi, ndiyo sheria mama. Aliisoma ibara hiyo akisema kama wajumbe wataruhusu kupitishwa kwa kifungu hicho, litakuwa kosa kubwa la kuvunja katiba ya nchi.
Ibara hiyo ya 18 ya katiba inasomeka, "Kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila kujali mipaka ya nchi... anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii."
"Hapa tuko kwa masuala muhimu kwa jamii kama waandishi wa habari wa Tanzania wana matatizo katika kuripoti habari za Bunge, hilo ni tatizo jingine, hatuwezi kutunga kanuni zinazokwenda kinyume na Katiba ambayo ndiyo sheria mama," alisema.
Akichangia hoja hiyo, Mjumbe Halima Mdee alisema: "Namshangaa Mheshimiwa Simbachawane kwani yeye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na anajua kwamba waandishi wanaruhusiwa kwenye vikao vya kamati. Iweje hapa kwenye Bunge la kutunga Katiba?
"Ninachokiona ni kwamba waandishi wa habari wanakatazwa kwa sababu ya hofu. Hii siyo Katiba ya kikundi cha watu 629 tuliopo hapa. Hii ni Katiba ya wananchi na wanayo haki ya kujua majadiliano yanayoendelea katika Kamati."
Mjumbe Machali alisisitiza kuwa kuwazuia waandishi ni kukiuka Katiba na kuhoji: "Nyie mnaosema mnataka kura za wazi ili wananchi wajue, mnaogopa nini? Katika hoja hiyo, Mjumbe Freeman Mbowe alisema Katiba ni mali ya wananchi na kwamba wana haki ya kufahamu kila kinachoendelea ndani ya Bunge.
"Kuna Watanzania kwa mamilioni ambao wanatusikiliza, kinachoonekana hapa tunaanza kuweka mkakati wa kuchuja nini kipelekwe kwa wananchi na hii ni hatari sana katika mchakato wa Katiba," alisema.
Alisema vyombo vya habari vina umuhimu wa kuripoti kila kinachoendelea ndani ya kamati na utaratibu wa kuwaruhusu waandishi wa habari kuripoti katika kamati umetumika katika nchi za Kenya na Afrika Kusini.
Baada ya hoja hizo za juzi usiku, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Costa Mahalu alisema: "Wajumbe ndiyo mnaokubali au kukataa mapendekezo yaliyotolewa na kamati yetu. Sisi mnatuagiza tunarekebisha mwafaka uliofikiwa na wajumbe na kuonyesha msimamo wao kwa pamoja, naomba hili tulirudishe kwa wajumbe wenyewe waliamue."
Hata hivyo, malumbano zaidi yaliendelea jana na Mwenyekiti Kificho alitoa taarifa ya kukubaliana na mapendekezo ya kamati yake.(P.T)

Wednesday, March 5, 2014

Giza nene mabilioni ya IPTL, Tanesco

 Gavana wa BoT, Profesa Benno.PICHK TABAIMA

Dar es Salaam.
 Wakati haijafahamika nani aliyelipwa mabilioni ya shilingi yaliyokuwa kwenye akaunti ya Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutokana na mvutano baina ya Tanesco na Kampuni ya IPTL, imebainika kuwa Bunge liliwahi kuagiza fedha hizo zisichukuliwe mpaka mitambo ya IPTL itakapokuwa chini ya Tanesco mwakani.
Hiyo imo katika taarifa ya iliyokuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2007.
Hata hivyo, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alithibitisha jana kuchotwa kwa Dola za Marekani 122 Milioni (Sh195.2 bilioni) katika akaunti hiyo, lakini akakataa kutaja nani hasa aliyelipwa.
Mkataba wa miaka 20 baina ya IPTL na Tanesco ulisainiwa mwaka 1995 na ulitakiwa kuisha 2015 na mitambo hiyo kuwa mali ya Tanesco.
Hata hivyo, ukiwa umebaki mwaka mmoja kumalizika, imebainika kuwa mitambo hiyo imeuzwa kwa Kampuni ya Pan African Power, ambayo inatarajiwa kuingia mkataba mwingine na Tanesco ili iwauzie umeme.
Ndulu alisema fedha zilizokuwa kwenye akaunti hiyo ni Dola za Marekani 22 milioni na Sh161 bilioni za Tanzania ambazo zote kwa pamoja ndizo zilizofikisha jumla ya Sh195.2 bilioni.
Vyanzo vingine vilitoa takwimu mbili tofauti, kimoja kikisema kiasi cha fedha hizo kilifikia Dola za Marekani 270 milioni na kingine Dola 250 milioni. Kuhusu nani mwenye mamlaka ya kutoa fedha hizo, Profesa Ndulu alisema kwa mujibu wa mkataba wa kufunguliwa kwa akaunti ya fedha hizo, ni Wizara ya Nishati na Madini pamoja na IPTL.
“Hakuna mtu mwingine anayeweza kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo zaidi ya hao, kwa hiyo hao ndiyo waliosaini kutolewa kwa hizo fedha na taratibu zote zilifuatwa,” alisema Profesa Ndulu.
Alipoulizwa ni nani aliyelipwa fedha hizo, Profesa Ndulu alisema IPTL ndiyo iliyokuwa na mamlaka ya kusema ni nani alipwe na ilifanya hivyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alipoulizwa juu ya fedha hizo alisema: “Kwa kawaida huwa nina majibu mafupi sana, lakini kwa kuwa mmeamua kuandika uongo, endeleeni, siwezi kukujibu chochote wasiliana na hao IPTL wakujibu.”
Hata hivyo, haikuwa rahisi kumpata kiongozi wa IPTL kuzungumzia suala hilo kwa kuwa tayari kampuni hiyo ni mufilisi.
Msimamo wa Bunge

Huyu ndio mama mzazi wa Nicki Minaj, ameanza kuimba na yeye.. msikie hapa

Screen Shot 2014-03-05 at 10.00.02 AMKama ilivyo kwa msanii kama Dully Sykes ambae yeye na baba yake wote wanafanya muziki, ndio imetokea hivyo pia kwa rapper Nicki Minaj wa Young Money ambapo mama yake mzazi nae ameanza kuimba.
Inawezekana alianza kuimba siku nyingi ila kwa sasa ndio imetambulika rasmi kupitia vyombo vya habari kwamba mama huyu anaimba, muziki anaoimba ni wa Injili.
Unaweza kutumia sekunde 32 za hii single ya Carol Maraj iitwayo ‘God’s been Good’ alafu uniandikie chochote kama mama katisha mama huyu ambae pia ni mwandishi wa nyimbo.
Nicki Minaj ana umri wa miaka 31 sasa hivi, huyu hapa chini ni mama yake miaka kadhaa iliyopita.
Screen Shot 2014-03-05 at 10.34.12 AM


Baada ya mashabiki 10,000 kumkataa Cleverley timu ya taifa, kocha Roy Hodgson awajibu

article_a8a1a4b43f6e6a33_1347185582_9j-4aaqskSiku chache baada mashabiki kupeleka ombi rasmi la kumzuia mchezaji Tom Cleverley kuitwa kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki kwenye michuano ya kombe la dunia 2014 huko Brazil, leo hii kocha wa timu hiyo Roy Hodgson amemtetea mchezaji huyo.
Zaidi ya mashabiki 10,000 walitia saini kwenye ombi hilo la kumzuia Cleverley kuichezea England. Baadhi ya watu mashabiki wamekuwa wakitoa maoni ya lugha chafu kabisa kwenye mtandao unaokusanya saini hizo – jambo ambalo limemkera Hodgson. 
“Ombi la mashabiki halijanifurahisha hata kidogo, lazima niseme ukweli,’ kocha huyo alisema huku akionekana kukerwa.
“Nimehuzunishwa kwamba Tom, kijana mdogo, amebebeshwa huu mzigo, lakini najua jambo moja kwa hakika, atapitia hali hii ngumu na atakapofanikiwa na timu yake Manchester United itakapoanza kushinda tena, ataanza kusifiwa tena na hao hao mashabiki.”
Kurudi kwenye kiwango kwa kiungo wa Liverpool  Jordan Henderson kufanya nafasi ya Cleverley kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa England kitakachoenda Brazil. Lakini Hodgson amekataa kutompa nafasi kiungo huyo wa Manchester United, ambaye alicheza mechi 9 za hatua ya kufuzu kombe la dunia..

Haya ndio Mapya kuhusu Jack Cliff,Mateso Gerezani,Gonjwa la Ajabu alilopata,Waliomtuma wanavyokula Bata Dsm

MODO mwenye mvuto Bongo Jacqueline Patrick ‘Jack’, ambaye yuko mahabusu ya Gereza la Qincheng nchini China kwa madai ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini humo, anazidi kuteseka, safari hii akidaiwa kukabiliwa na tatizo kubwa la kiafya.

Jacqueline Patrick ‘Jack’.
 Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jack anasumbuliwa na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, hali iliyomfanya apoteze uzito wa kilo kumi huku akikabiliwa na tatizo lingine la kupungua kwa kasi ya mapigo ya moyo. 


KAMA HALI ITAENDELEA
Chanzo kimesema kuwa endapo hali ya kuzorota kwa afya hiyo kutaendelea, Jack anaweza kujikuta katika tatizo kubwa zaidi ambalo linaweza kusumbua kwenye mwenendo mzima wa kesi yake.
 “Kusema kweli kuhusu maisha ya mahabusu si mabaya sana kwake, hateswi kwa kupigwa wala hanyimwi chakula, ila hana uhuru binafsi, ni kama amefichwa, naamini matatizo hayo ya kiafya yanatokana na uzito wa kesi yake,” kilisema chanzo hicho. 

MLOLONGO WA MAMBO
Habari zaidi zinadai kwamba kesi ya msingi ya staa huyo kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya itaanza kusikilizwa rasmi Septemba, mwaka huu baada ya mwanasheria wake kukamilisha taratibu zote.

“Ile kesi yake sasa ni Septemba mwaka huu. Si unajua hajawahi kupandishwa kizimbani kuulizwa kama ni kweli alikamatwa na unga au la!” kilisema chanzo hicho.

Jack Patrick akiwa amefunikwa uso baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni nchini China.
 WAKILI WAKE ANATOKA HONG KONG
Taarifa zaidi zinasema kuwa wakili wa mrembo huyo anatoka jijini Hong Kong nchini humo ambako ndiko kwenye wanasheria wazuri kwa kiwango cha kesi yake ya unga. 

KUMWONA NI KWA AHADI
Ikazidi kudaiwa kwamba kuna Mtanzania mmoja tu ambaye amekuwa na fursa ya kumuona modo huyo na kabla ya kwenda lazima aombe na kupewa ‘apointimenti’ maalum. 

WALIOMTUMA WAMPIGA CHENGA, WALA ‘BATA’
Tofauti na kwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye naye aliwahi kupata msala mkubwa kama huo nchini Afrika Kusini, Julai, mwaka jana ambapo ‘mabosi’ wake walikuwa mstari wa mbele kumhangaikia, Jack anasota mwenyewe.
 Habari zinasema kuwa hakuna cheni yoyote kutoka kwa watu ambao wanatafsiriwa kuwa ni waliomtuma kwani wanaosumbuka ni watu wake wa karibu, wakiwemo ndugu zake. 

Juzi, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na mtu wa karibu sana na mtuhumiwa huyo ambapo alikiri Jack kuwa na hali ngumu katika kesi yake hiyo huku akisema kwamba watu wanaodaiwa ndiyo mabosi wake wanakula ‘bata’ tu jijini Dar es Salaam. 

“Unajua tatizo la biashara ya unga ni hapo tu! Wewe unayebeba ukinaswa ni juu yako, waliokutuma wao wanachofanya ni kuthibitisha tu kuwa ni kweli umekamatwa maana wapo wanaodaiwa wamekamatwa kumbe si kweli, wanaingia mitini na mzigo,” alisema mtu huyo.  
 SABABU ZA MOYO KUSHINDWA KUSUKUMA DAMU
Juzi, gazeti hili lilimtafuta daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza tatizo la moyo kushindwa kusukuma damu ambapo alisema: 

“Moyo kushindwa kusukuma damu kwa mwendo wa kawaida husababishwa na shinikizo la damu lisilodhibitiwa, mgonjwa kushindwa kudumisha udhibiti wa maji mwilini, chakula au dawa. 

“Sababu nyingine ni upungufu wa damu na utoaji wa kiwango cha juu cha homoni za koromeo ambazo zinaleta maumivu ya ziada kwenye misuli ya moyo, utumiaji mwingi wa vimiminika au ulaji wa chumvi uliopitiliza na utumiaji wa dawa ambazo husababisha uwekaji wa maji mwilini kama vile Hiazolidinedione.” 

KUHUSU KUKOSA HAMU YA KULA
Kwa mujibu wa daktari huyo, tatizo hilo humkumba mtu anapokuwa katika msongo mkubwa wa mawazo kutokana na jambo zito linalomkabili, ambalo halina mlango wa kutokea.
TUKUMBUKE
Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za heroin tumboni zikiwa na thamani ya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 300. 
Awali ilidaiwa kuwa kesi yake ingeanza kusikilizwa mwaka 2016 baada ya yeye kujifunza Kireno (lugha inayotumika Macau) kwa miaka miwili

Hatimaye Msanii Ally Kiba aanika Hekalu(mjengo) Wake wa Nguvu huu hapa


 
Akimalizia kuweka sama maeneo ya Chumbani. 
Ukiwa ndani ya Hekalu Jumba la Ngvu la Msanii ally KibaHili ni eneo la Nje la Hekalu la Msanii Ally Kiba
Msanii Wa Bongo Fleva hii leo Kupitia Ukurasa wake wa FB ameamua kuweka hizi Picha zenye mwonekano wa Hekalu(mjengo wa Nguvu) anaoumalizia kuufanyia-renovation