Siku chache baada mashabiki kupeleka ombi rasmi la kumzuia mchezaji Tom Cleverley kuitwa kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki kwenye michuano ya kombe la dunia 2014 huko Brazil, leo hii kocha wa timu hiyo Roy Hodgson amemtetea mchezaji huyo.
Zaidi ya mashabiki 10,000 walitia saini kwenye ombi hilo la kumzuia Cleverley kuichezea England. Baadhi ya watu mashabiki wamekuwa wakitoa maoni ya lugha chafu kabisa kwenye mtandao unaokusanya saini hizo – jambo ambalo limemkera Hodgson.
“Ombi la mashabiki halijanifurahisha hata kidogo, lazima niseme ukweli,’ kocha huyo alisema huku akionekana kukerwa.
“Nimehuzunishwa kwamba Tom, kijana mdogo, amebebeshwa huu mzigo, lakini najua jambo moja kwa hakika, atapitia hali hii ngumu na atakapofanikiwa na timu yake Manchester United itakapoanza kushinda tena, ataanza kusifiwa tena na hao hao mashabiki.”
Kurudi kwenye kiwango kwa kiungo wa Liverpool Jordan Henderson kufanya nafasi ya Cleverley kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa England kitakachoenda Brazil. Lakini Hodgson amekataa kutompa nafasi kiungo huyo wa Manchester United, ambaye alicheza mechi 9 za hatua ya kufuzu kombe la dunia..
No comments:
Post a Comment