Sunday, January 5, 2014

VILIO MAJONZI MSIBA WA WAZIRI MGIMWA

Mwili wa William Mgimwa, ukipokelewa uwanja wa ndege DarVILIO, majonzi na simanzi jana vilitawala katika Uwanja wa Ndege wa Kimaitafa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam wakati mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa, ukipokelewa kutoka nchini Afrika Kusini.
Mgimwa alifariki dunia Januari Mosi, mwaka huu, nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa kwa muda usiopungua miezi mitatu.
Mwili huo uliwasili nchini majira ya saa saba mchana na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini, ukiwa na familia yake ikiongozwa na mkewe Jane Mgimwa pamoja na baadhi ya maofisa wa serikali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi; Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba; Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi wa Tanzania, nchini Afrika Kusini, Monica Mwamunyange pamoja na wanafamilia watatu ndio waliwaongoza mawaziri, manaibu mawaziri, maofisa wa serikali, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge na wananchi kupokea mwili huo.
Viongozi, maofisa na wananchi waliokuwepo uwanjani hapo walionyesha sura ya huzuni hata wengine kububujikwa machozi mara baada ya kuona jeneza lenye mwili wa Waziri Mgimwa likitolewa katika ndege na baadae kupelekwa katika gari maalumu la kubebea maiti na kuanza msafara kuelekea nyumbani kwake, Mikocheni B.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa nyakati tofauti uwanjani hapo namna walivyomfahamu Mgimwa, alivyoongoza wizara nyeti ya Fedha na Uchumi, viongozi kadhaa walisema alikuwa mchapakazi na mnyenyekevu katika kazi yake hasa pale alipotakiwa kujibu hoja na maswali mbalimbali kwa wabunge.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alisema Mgimwa alikuwa akikaa karibu naye bungeni na pia atamkumbuka kwa uchapakazi wake.
“Nitamkumbuka, lakini tutamkosa sana marehemu Waziri Mgimwa kwani alikuwa mchapakazi wakati wote akiwa wizarani kwake, bungeni na hata katika jimbo lake,” alisema Chikawe.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli alisema atamkumbuka Mgimwa kwa uchapakazi wake, unyenyekevu, upendo wake kwa watu wote hasa mawaziri wenzake, wafanyakazi na wananchi wote aliouonyesha katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu alipokuwa waziri.
“Siku si nyingi niliongea naye kuhusu kuwalipa makandarasi wangu… aliniahidi mara atakapopona atawalipa, lakini Mungu amempenda zaidi, tumwombee,” alisema.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema alijifunza unyeyekevu na hekima kutoka kwa marehemu ambaye hakujali cheo cha mtu katika kuwahudumia.
“Waziri Mgimwa alikuwa na sifa nyingi sana, uaminifu na kujituma nazo zilikuwa zake… kwa kweli ameacha pengo kubwa,” alisema.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, alisema marehemu Mgimwa alikuwa mtu makini na muwazi, kwamba kutokana na sifa hizo aliweza kuongoza sekta ngumu yenye lawama, lakini alijitahidi kuieleza kwa uwazi.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema ameguswa na msiba huo kwa kuwa alifanya kazi na marehemu Mgimwa, bila ya kukwaruzana naye akiwa Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi.
“Mimi kama waziri kivuli wa wizara kama yake, niliweza kuwasiliana naye mara kwa mara, alinipokea kwa unyenyekevu, alipokea ushauri wangu na kuufanyia kazi… hata siku moja sijawahi kujibishana na marehemu Mgimwa,” alisema Zitto.
Zitto aliwataka viongozi wote wa siasa na serikali kuiga uongozi wa marehemu Mgimwa aliouonyesha mara alipoteuliwa na rais kuwa Waziri wa Fedha na hasa unyenyekevu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema atamkumbuka marehemu Mgimwa kama mtu wa watu, kiongozi asiye mbinafsi kwa kuwa alichokipata kilikuwa cha wote.

Msafara wake.

Msafara wenye magari yasiyopungua 50 uliondoka uwanja wa ndege majira ya saa 9, kuelekea nyumbani kwake, Mikocheni B, ambapo ilifanyika ibada ya misa takatifu na baadae mwili kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo.Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, Rais Jakaya Kikwete, leo anatarajia kuongoza mamia ya waombolezaji wakiwamo wanafamilia, wananchi, viongozi wa kisiasa na kiserikali kuuaga katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa 5 asubuhi.Ratiba hiyo inabainisha kuwa mara baada ya shughuli hiyo itakayoisha saa 8 mchana, mwili huo utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Teminal 1) kwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Iringa ambapo utafika saa 10 jioni ili kuwapa fursa wananchi wa mkoa huo kuuaga katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Na mara baada ya wananchi wa Iringa Mjini kuuaga, jioni hiyo hiyo mwili wa Mgimwa utapelekwa kijijini kwake Magunga kwa ajili ya mazishi kesho yake ambayo nayo yataongozwa na Rais Kikwete.

Mkwasa kocha Yanga

Mkwasa kocha msaidizi wa Yanga


















Uongozi wa Young Africans SC umepata warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi (Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali na Dr. Suphian Juma), huku wakiendelea na mchakato kumpata kocha mkuu ambaye atachukua nafasi ya mholanzi Ernie Brandts aliyesitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.
Charles Boniface Mkwasa "Master" aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting katika mzunguko wa kwanza anachukua nafasi ya aliyekua kocha msaidizi Fred Felix "Minziro" ambaye muda wake umemalizika mwishoni mwa mwaka 2013. Mkwasa ambaye aliichezea Young Africans miaka ya 80's kwa kiwango cha hali juu pia alishawahi kuwa Kocha Mkuu/Msaidizi kwa kikosi cha Jangwani kwa vipindi tofauti jambo ambalo linamfanya aiwe mgeni katika mitaa ya Twiga na Jangwani.
Kocha wa makipa wa timu ya Taifa Tanzania "Taifa Stars" Juma Pondamali "Mensah" anachukua nafasi ya aliyekua kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa ambaye pia alistishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013. Pondamali golikipa aliyeichezea Yanga miaka ya 80's kwa kwa kiwango cha hali ya juu hata kufikia kuwa katika kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano ya Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, sio mgeni katika timu ya Young Africans kwani awali alishwahi kuwa kocha msaidizi kwa vipindi tofauti.
Dr Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr Nassoro Matuzya ambaye pia alisitishiwa ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013 pamoja benchi la Ufundi. Mara baada ya kuwapata viongozi hao watatu wa Benchi la Ufundi kikosi cha Young Africans kesho kitaanza mazoezi jioni katika Uwanja wa Bora Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kimataifa huku kocha Mkwasa akiongoza benchi hilo la Ufundi mpaka atakapopatikana kocha mkuu ambaye watafanya watafanya kazi kwa pamoja.

Saturday, January 4, 2014

HII NDIYO HIFADHI YA CHURA ANAYEZAA.


HII NDIYO HIFADHI YA CHURA ANAYEZAA‏, HAPATIKANI POPOTE DUNIANI ISIPOKUWA TANZANIA. MALI ASILIZETU

Pichani ni Bomba zilizowekwa na kutoa maji ya mvuke 'Sprinkers' kule kwenye korongo la Kihansi ambako ni makazi asilia ya chura kuwavutia chura kuishi kumejengwa na daraja la mbao kwa ajili ya kuvuka mto.
 
Wengi wanapenda sana kufahamu juu ya hifadhi ambayo kuna Chura pekee wanaozaa, na ambao hawapatikani sehemu nyengine lakini Tanzania Pekee.. hifadhi hii ni pekee kabisa inayo patikana katika korongo la la kihansi .. chura huyu wa Kihansi ni kama zilivyo raslimali nyengine na ni maliasili ya muhimu sana inayopatikana Tanzania
Chura huyu ambaye aligunduliwa mnamo mwaka 1996 katika maporomoko ya maji ya yaitwayo mahalala yanayopatikana ndani ya mlima Udzungwa wilayani kilombero mkoani Morogoro .Kwa hakika Chura huyu anaishi katika mazingira ya maji yanayo tiririka na kutoka kwenye mvuke wa kutosha unaotokana na nguvu za maji.
Chura huyu ambaye kwa ufupi na kwa jina lake la kingereza anaitwa Spray Toad na kwa jina la kitaalam anaitwa Nectophynoides asperginis ni moja ya kiumbe muhimu kwa sababu moja kubwa ya kuwa hapatikani katika sehemu yoyote duniani isipokuwa katika Bonde la kihansi Nchini tanzania  pekee..
Huyu ni Chura pekee katika jamii ya vyura wengi ambao mnawafahamu na waliopo duniani kwa sababu moja muhimu sana kuwa , chura huyu hutaga mayai na kukaa nayo katika kimfuko kilichopo ndani ya chura mwenyewe  hadi muda wa kuanguliwa unapotimia na ndipo huanguliwa na kutoa kiumbe kilicho hai. 
kwa Lugha nyepesi ni kwamba chura huyu huzaa kwa sababu  mayai anayotaga hayaonekani hubaki tumboni kwake hadi anapo zaa ndio watoto wanatoka nje.
Tabia hii muhimu ya vyura hawa kuzaa ndiyo ambayo inawafanya waendelee kuwa ni wapekee kabisa Duniani, tofauti na vyura wengine ambao wao hutaga na kuhifadhi mayai yao katika maji na mwishoe kuanguliwa. 
Chura huyu pekee ni kiumbe ambaye ameingia katika mkayaba wa  wanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka, chura huyu hawezi kufanyiwa biashara yoyote.
Zaidi ya hapo Bonde hili la pekee la Kihansi lina ukubwa wa kilometa nne kwa urefu na nusu kilometa kwa upana, na Bonde hili linapatikana katika mto wa Kihansi unaoanzia wilaya ya Mufindi na kililo  mkoani Iringa na kupeleka maji yake  kilombero mkoani Morogoro. 
Mwisho katika mafanikio yote yanayopatikana katika bonde hili la pekee la Kihansi hayatokani na mtu mmoja , wala kundi flani bali ni kwa taifa letu na kwa jamii kwa ujumla.

MOTO WATEKETEZA YUMBA 10 PEMBA

MOTO WATEKETEZA YUMBA PEMBA MICHEWENI

MOTO UKITEKETEZA NYUMBA PEMBA


Moto wateketeza nyumba zaidi ya kumi huko  pemba micheweni moto huo ambao ulianza majira ya mchana na chanzo chake mpaka sasa hakijafaamika bado moto huo umesababisha hasara kubwa ya mali ambazo babo hakuyafanyika tathimini lakini ni madhara makubwa sana moto huo umeleta licha ya kwamba hakuna mtu aliyejeluhiwa kwenye tukio hilo.

BANGI YALUHUSIWA MAREKANI

BANGI YALUHUSIWA MAREKANI ,TAZAMA SASA FOLENI YA WANUNUZI WA KILEVI HICHO.



Hawa hapo juu ni baadhi ya wateja ambao wanaishi marekani(colorado)wakijinunulia bangi zao wenyewe toka ipitishwe kisheria kufutika katika jiji la collorado Marekani.


bangi 9
\

Huko colorado nchini marekani wameruhusu uvutaji wa bangi lakini kwa wale tu wanaoanzia na miaka 21 na kuendelea ndio wanaoluhusiwa kuvuta bangi
Mduka mengi ya kuuza bangi hizo huwa kuna walinzi ambao ukienda ni lazima uonyeshe kitambulisho kuwa wewe uko na miaka 21 au zaidi,
upekuzi wetu bantanyau umebaini kuwa toka bangi iluhusiwe kuvutwa colorado duka moja linaweza kuhudumia wateja hadi mia saba kwa siku na wenye maduka wanasema wanayo bangi ya kutosha kabisa.


Foleni ya kununua bangi mazee

Foleni kwenye duka la kuuzia marijuana(bangi)



Denver prepares for marijuana legalization

Hapo juu ni bango ambalo linaonyesha matangazo wapi bangi ina patikana hasa kwa wale watalii ambao wanatembelea colorado



New Year Celebration

bangi 7

bangi 6

bangi 4

Maduka yaliyo na kibali cha kuuza marijuana(bangi)

bangi 3
bangi 2
bangi 11
bangi 14
bangi 13

CHADEMA WAFANYA KIKAO CHA KAMATI KUU

CHADEMA WAFANYA KIKAO CHA KAMATI KUU LEO JIJINI DAR.


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed wakati wa Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu.…

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed wakati wa Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Thursday, January 2, 2014

BREAKING NEWS!!!

 
Taarifa ambazo zimetufikia kupitia kituo cha WAPO Radio FM zinaeleza kwamba kuna bomu limelipuliwa kwenye kanisa katoliki la Mtakatifu Karoli, Ruanga huko USA River jijini Arusha, ambapo wanakwaya takriban 6 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo zimetufikia, zinaeleza kwamba watuhumiwa ni jeshi la Polisi, na kwamba walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu - lililojeruhi 6, ambapo 4 kati yao wameruhusiwa baada ya matibabu kwenye hospitali ya Mission na ya Wilaya ya Arumeru.

Majira ya saa sita na nusu, waumini walidai kuona gari la polisi likipita kwa kasi, na lilipowakaribia walistuka mlipuko ukiwarusha pembeni, ambapo walijikuta na majeraha na usoni, mapajani na maeneo mbalimbali ya mwili. Kisha baada ya hapo gari ilisogea mbele na kuanza kurusha mabomu kwa watu wowote iliokutana nao.

Hadi sasa inaelezwa kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika, huku Kamanda Liberatus Sabas akikataa kuzungumzia zaidi suala hilo. Alipotafutwa na WAPO Radio FM, hakueleza kwa kina, lakini akasema kuwa sio suala la kwaya kama ambavyo imeelezwa, bali ni wakinadada wawili na kwamba hawezi kuzungumza zaidi, bali kesho (Ijumaa) atatoa taarifa rasmi na iliyo kamili kwa vyombo vya habari.


Alipoulizwa kuwa kama ni kweli jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika, alisema kuwa atazungumza kesho kuhusiana na tukio hilo. Tukio hili limetokea ikiwa ni siku mbili zimepita tokea kuapishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Ernest Mangu ambaye amechukua nafasi ya IJP Said Mwema aliyestaafu.

Wednesday, January 1, 2014

Ndugu wazazi, walezi na wanafunzi

Ndugu wazazi, walezi na wanafunzi.

Mnataarifiwa ya kuwa majina ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2013 ambao wamefaulu na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari (kidato cha kwanza) mwaka 2014 yanapatikana katika mbao za matangazo katika shule za Msingi waliposoma wanafunzi husika na katika mbao za matangazo kwenye Ofisi za Kata zilizo jirani.

Mkenya apigwa KO usiku wa Mwaka Mpya

MABONDIA WATIFUANA USIKU WA KUINGIA MWAKA MPYA

Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo Picha na @http://mabantanyau.blogspot.com
Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo Picha na @http://mabantanyau.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana kakonde na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao wa raundi sita kwa ajili ya kufunga mwaka king class mawe alishinda kwa point Picha na @http://mabantanyau.blogspot.com
Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point Picha na @http://mabantanyau.blogspot.com

Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point Picha na @http://mabantanyau.blogspot.com
USHINDI RAHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AKINULIWA MKONO JUU BAADA YA KUMDUNDA MUSTAFA DOTTO WAKATI WA KUSHEREKEA USIKU WA MWAKA MPYA ZAIDI TEMBELEA @http://mabantanyau.blogspot.com
Bondia Kalama Nyilawila kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makone na Ibrahimu Maokola wakati wa mpambano wao ulifanyika kwa ajili ya kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya Kalama  alishonda kwa k,o ya raundi ya pili
 @
http://mabantanyau.blogspot.com
Bondia Iddy Mnyeke  kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao wa kuuwaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya mpambano huo ulito droo  picha na
@
http://mabantanyau.blogspot.com

Cosmas Cheka na Iddy Mnyeke wakipambana


MABONDIA WAKISUBILI MATOKEO AMBAYO YALIKUWA NI DROO

JACK AJUTA KUBEBA MADAWA YA KULEVYA


JACK PATRICK MATESO SAA 48, DADA YAKE AMLILIA, ASEMA ALIMUONYA



Stori:  Jelard Lucas
HABARI ya kufungia mwaka 2013 na kufungua pazia la mwaka mpya wa 2014 ni madai ya mwanamitindo kiwango Bongo, Jacqueline Patrick kukamatwa katika  Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akiwa na mzigo wa madawa ya kulevya aina ya heroin lakini Risasi Mchanganyiko linaangaza mapya zaidi juu ya sakata hilo.

Macho na masikio ya Wabongo wengi kwa sasa ni juu ya mwenendo wa madai hayo, wakati gazeti hili likiendelea kupekenyua limenasa mpya kuwa, Jack yupo kwenye mateso makali kutoka kwa askari wapelelezi nchini humo wanaotaka kujua mtandao unaomuunganisha katika mchezo huo.

SAUTI KUTOKA CHINA
Chanzo chetu makini kilichopo China ambacho kinapiga kitabu kilieleza kuwa, katika kufuatilia ishu hiyo, juzi Jumatatu, Desemba 30, 2013, alikutana na kizingiti cha kushindwa kuonana na Jack katika mahabusu aliyowekwa kwa maelezo kwamba, uchunguzi bado unaendelea.

Raia huyo wa Tanzania aliyedai ana ukaribu na Jack, kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini, alisema mengi kuhusiana na mateso anayopata mrembo huyo hivi sasa.
“Ni kweli Jack amekamatwa hapa Macau. Hilo halina ubishi kabisa. Sheria za huku zinatofautiana kati ya jimbo na jimbo. Nilifika mahabusu aliko kwa lengo la kutaka kumwona lakini nilikataliwa. Nimeambiwa hawezi kuonana na mtu yeyote hadi Machi, mwakani (mwaka huu). Bado wanaendelea na uchunguzi kwanza.

“Unajua wanajaribu kufichaficha mambo ili polisi waweze kufanya upelelezi wao vizuri lakini nimepenyezewa taarifa kuwa ataingizwa chumba cha mateso ili abanwe na kutaja mtandao wake. Wanajua yeye wameshamkamata, lakini wanataka kufahamu mzigo alitumwa na nani, ameutoa nchi gani na unakwenda nchi gani?

“Lengo la kufanya hivyo ni kukomesha mtandao mzima wa madawa ya kulevya. Si ajabu akawa kwenye mateso kwa kipindi chote hicho kama hatakuwa mkweli lakini kwa sasa ataingizwa kwenye kikosi cha kwanza.

“Hapo atakalishwa kwenye chumba cha mateso kwa siku mbili mfululizo (akimaanisha saa 48). Ni mateso makali sana. Wataalam wanajua wanafanyaje ili mtuhumiwa aweze kuzungumza ukweli kwa muda mfupi. Sasa hapo ikishindikana ndipo anaweza kuhamishiwa kwenye kikosi kingine,” alipasha mtoa habari wetu na kuongeza:

“Ni kama huko Bongo tu. Unaposikia chumba cha mateso ya wapelelezi maana yake shughuli yake siyo ndogo. Mimi namuonea huruma sana Jack, lakini najiuliza, hivi ni kwa nini huwa hawajifunzi kupitia wenzao?

“Si juzi tu wengine (Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa Edward) wamekamatwa kwa madawa hayohayo na walisota kwa muda mrefu? Kwa nini hawasikii jamani? Namuhurumia sana kwakweli.”

KUMBE DADA YAKE ALIMUONYA
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na dada wa Jack zinasema kuwa, wakati akitaka kusafiri akitokea Bongo, alimweleza dada yake juu ya mpango wake huo, akamuonya lakini modo huyo alikataa.

“Alimfuata dada yake na kumweleza mchongo mzima kuwa alitaka kwenda na mzigo China, dada yake akamwambia aachane na hizo biashara, akakataa. Jack alifikia hatua akamwambia dada yake kuwa hana mtoto, hana mume wala ndugu anayemtegea kwa hiyo yupo tayari kwa lolote kwani hakuwa na cha kupoteza.

“Kama angemsikiliza dada yake (jina linahifadhiwa) haya yote yasingemkuta na asingeingia kwenye mateso ya namna hii,” alisema mtoa habari wetu huku akiendelea kusisitiza jina lake lisionekane mahali popote kwenye ukurasa huu.

ABEBESHWA MZIGO, ALIPWA MALIPO YA AWALI
Ilizidi kusemekana kuwa, alipokaribia kuondoka Bongo, Jack alimwambia dada yake kwamba anakwenda kambini (kituo cha kuingiza mzigo tumboni) ambapo aliporejea kwa dada’ake alimuonesha dola za Kimarekani 21,000 (zaidi ya shilingi milioni 33) ambazo ni malipo ya awali huku akimwambia alishabebeshwa nusu ya mzigo.

Hata hivyo, habari zinasema Jack alimwambia dada yake huyo kuwa hakuwa akijisikia kusafiri lakini kwa kuwa anatafuta maisha aliamua kuondoka baada ya mzigo kukamilika wote siku iliyofuata.

INA MAANISHA NINI?
Kwa mujibu wa maelezo hayo, Jack aliondoka na unga hapahapa Bongo kwenda Thailand kupitia Nairobi, Kenya na baadaye Macau, China ambako alinaswa.

MASTAA WAFUNGUKA
Watu wamekuwa na mitazamo tofauti kulingana na ishu hiyo lakini Risasi Mchanganyiko lilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao wameeleza maoni yao kuhusiana na sakata hilo la Jack.

Katika mahojiano na waandishi wetu, tulitaka kusikia kutoka kwao namna wanavyolinganisha tabia ya kujihusisha na biashara za kusafirisha madawa ya kulevya na vitendo vya umalaya ambapo wametoa maoni tofauti.

JACQUELINE WOLPER:
“Mh! Mwenzangu, bora uwe na mabuzi (wanaume wenye mkwanja) 40 kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba mastaa wenzangu wasikubali kubebeshwa madawa kwa kudanganywa eti na dola 30,000, kamwe haiwezi kubadili mfumo wa maisha yako.” 

REHEMA CHALAMILA ‘RAY C’:
 “Madawa ya kulevya hayakubaliki, yalinitenda sana haya madude! Kabisa tulinde vizazi vijavyo kwa kupiga vita madawa ya kulevya. Fanya yote lakini siyo madawa ya kulevya.”

SHAMSA FORD:
 “Nasema hivi, bora umalaya japo pia si mzuri kuliko kudili na biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba waachane na vitu hivyo kwani vinatumaliza kisanii... lakini nasisitiza kutulia na bwana mmoja ni vizuri sana kuliko kurukaruka.”

JOKATE MWEGELO:
 “Hakuna aliye mkamilifu lakini kama kitu ni kiovu ni kiovu tu hata kama mimi na wewe tunakifanya, kimsingi hakuna bora na anayesema kuna ubora basi hajitambui. Vyote vinadhalilisha utu na thamani ya mwanamke. Mwili si wa kuchezewa.”

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’:
“Tukitumia majina yetu vizuri, hakuna atakayejihusisha na yote hayo... tujitume kufanya kazi, umalaya unaweza kuwa bora kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya kama utabanwa kuchagua maovu hayo. Maisha ya Ughaibuni yatatumaliza kwani tunaiga kwa kukurupuka bila kuelewa.”

TUMETOKEA HAPA
Jack anatuhumiwa kukamatwa na madawa ya kulevya Desemba 19, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea jijini Bangkok, Thailand akiwa safarini kwenda Guangzhou nchini China.
Ilielezwa kuwa unga aliokutwa nao una uzito wa kilo 1.1  ndani ya kete 57 huku thamani yake ikitajwa kuwa ni  zaidi ya shilingi milioni 223.
Bado yupo mikononi mwa polisi wa China wakati upelelezi wa awali ukiendelea ambao utafikia tamati Machi, mwaka huu kabla ya kuingia hatua nyingine.

WACHINA WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO BANDALINI DAR ESA SALAAM


WACHINA WAKAMATWA NA SHEHENA YA MENO YA TEMBO BANDARINI DAR.



Wakuu,

Japo naiweka kama tetesi ila napenda ifahamike kuwa ukweli wake utajidhihiri muda si mrefu.

Tetesi yenyewe ni kuwa Kuna Wachina wamekamatwa na Shehena Kubwa ya Meno ya tembo Bandarini Dar na sasa wamechukuliwa kisiri na "watu flani" ambao hawataki habari hii ijulikane.

Napenda kuviarifu vyombo vyetu vya dola kuwa makini na "watu hawa flani" kwani wananchi hatutakaa kimya endapo hili litanyamaziwa.

Namna yoyote ya kuzima huu ujangili italeta balaa kubwa si kwa vyombo vya dola tu bali hata kuitia doa serikali kwa ujumla. Msifiche, waanike ili waueleze umma nani yupo nyuma yao!

Happy New Year 2014!

========
UPDATE:

Ili wajue tumeshajua na si siri na kiasi cha "mzigo" tunajua, naongeza data:

Ilikuwa ni meli ya kijeshi ya China ambayo ilikuwa imeegesha gati namba 3 baada ya kuwa nchini katika shughuli za kawaida za ushirikiano katika kudhibiti maharamia (Pirates). Katika kuuficha mzigo kwa kudai magari yamebeba chakula ndipo wakashtukiwa.

Chanzo chetu kinatufahamisha kuwa Wametiwa pingu na wanajeshi wa JWTZ na TISS na wamepelekwa Ukonga na msafara wa magari mawili yakiongozwa na pikipiki za Polisi.

Hata walipo tuna chanzo chetu ambacho kitaendelea kutujuza kinachojiri.

Taarifa ya Ikulu kuhusu kifo cha Waziri wa fedha William Mgimwa


Taarifa ya Ikulu kuhusu kifo cha Waziri wa fedha William Mgimwa.

mgimwa 12

Rais Jakaya Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri huyu wa fedha William Mgimwa na kwamba taifa limempoteza katika kipindi ambacho linamuhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa.
Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue ambae ndio ametangaza kifo cha Waziri huyu kwa niaba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amesema Mgimwa amefariki saa tano na dakika 20 asubuhi hospitalini Afrika Kusini.
Maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Marehemu yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia na kwamba taarifa zaidi zitazidi kutolewa kadri zitakavyopatikana

KALAPINA ULINGONI



Jana ndio ilikua siku ya Kalapina kupigana ulingoni, unajua nini kilitokea?

DSC_0033

Yaweza kuwa ni nafasi ya wasanii wa Tanzania kujaribu upande wa pili wa maisha yao kwenye utafutaji pesa manake msanii Kalapina toka block41 Kinondoni Kikosi cha Mizinga ameamua kuangalia upande wa pili ambao ni masumbwi a.k.a ngumi za kulipwa.


DSC_0038

December 31 mkesha wa kuukaribisha mwaka 2014 umeingia kwenye headlines upande wa Kalapina baada ya mpinzani aliyekuwa apigane nae usiku huo kutotokea kwenye pambano hilo na kufanya millardayo.com kufanya interview na Kalapina baada ya kushuka jukwaani ili kujua imekuaje.


DSC_0053

Kalapina anasema ‘mpinzani wangu alikuwepo na alipima siku ile lakini nafikiri jina limemtisha na historia yangu ya mtaa imemtisha ameogopa na kweli leo ningefanya mambo makubwa kwenye ulimwengu wa ngumi, ningeacha historia nilijiandaa huyu mtu aondoke na machela’


DSC_0050

‘kama nilivyotangaza pale mapromota mi nipo tayari sasa hivi nipo tayari kufa nipo tayari kupambana mi nimeingia kwenye ngumi rasmi sasa hivi, kupigana ni sehemu ya maisha yangu na bondia atakayejitokeza kupigana na mimi nitampigia saluti’ – Kalapina


DSC_0045

‘Taarifa ya kutokuwepo mpinzani wangu kwenye mpambano sikuwa nayo mapema hadi napanda pale jukwaani nilikuwa na uhakika mpinzani wangu yupo na tunapigana, mimi sibipiwi ukinibipu nakupigia…… taarifa hii imfikie’ – Kalapina


DSC_0036

‘Kwa sasa hivi namtaka Japhet Kaseba namtaka na Mchumia Tumbo maana wanaongeaongea sana hawa, kama Mchumia Tumbo anajifanya hana. mpinzani wakati wapinzani tupo’.


Kwenye hili pambano la Kalapina alitakiwa kuzichapa na Bahati Mwafiyale ambae aliitwa mara kumi na hakutokea jukwaani hivyo Kalapina akapewa ushindi aisee.