Friday, March 21, 2014

Tufanye kazi, Watanzania wana matarajio makubwa na gesi –Muhongo


 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo wakati wa kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makampuni washirika ya StatOil, BG Tanzania, Exxon Mobil na Orphir Energy. Katikati ni Rais na Meneja Mkuu wa Kampuni ya BG Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Derek Hudson. 
 Rais  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Exxon Mobil Bw. Rolf Michael de Jong   kwa niaba ya washirika  wa  makampuni  yanayofanya maandalizi ya utekelezaji wa Mradi huo wa gesi iliyosindikwa (LNG) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wakati wa kikao hicho.
 Mkuu wa Mashauriano wa Kampuni ya StatOil Tanzania Bw. Ole- Johan Lydersen wa kwanza mwishoni akiongea jambo wakati wa kikao hicho.
Afisa Mipango Miji Bw. Daniel Nguno kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiongea jambo wakati wa kikao hicho cha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa LNG.

 ========  ======  =======

Tufanyekazi, Watanzania wana matarajio makubwa na gesi –Muhongo

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, Watanzania wana matarajio makubwa kutokana na kugunduliwa kwa hazina kubwa ya gesi katika maeneo ya kina kirefu cha bahari.

Profesa Muhongo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makampuni washirika ya Statoil, BG Tanzania, Exxon mobil na Orphir Energy yanayofanya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa   gesi  iliyosindikwa (LNG).

Ameongeza kuwa, Serikali inayo nia ya dhati katika kutekeleza mradi huo ili kuhakikisha kwamba uchumi wa gesi unakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote. Hivyo, wenye jukumu la utekelezaji wametakiwa kutekeleza mipango mikakati yao kwa kuzingatia muda husika, wakati huo huo wakifanyakazi kwa ushirikiano na mamlaka husika na kwa uwazi.

“Wananchi wana matarajio makubwa na gesi, msiiangushe Tanzania katika hili, hatutaki kuonekana waongo, mkichelewa mnatupa wakati mgumu. Sisi sote tunatakiwa kuongea lugha moja kwa wananchi. Tumejipanga vizuri tunachotaka ni kutekeleza mipango yetu”. Amesema Profesa Muhongo.

Katika hatua nyingine, Waziri Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi, wamesisitiza kuwa makampuni hayo,  yanapaswa kuhakikisha kwamba mipango yao  ya utekelezaji wa mradi huo  inapaswa kwenda sambamba na matakwa   ya Sera ya  Gesi Asilia.

Katika kikao hicho, makampuni hayo washirika yamewasilisha  taarifa ya hatua waliyofikia katika  maandalizi ya utekelezaji wa mpango kazi wa mradi huo  na kueleza hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa na zinazotakiwa kuchukuliwa ili utekelezaji wa mradi  ufanyike kama ulivyopangwa.

Aidha, katika taarifa hiyo wameainisha hatua mbalimbali ambazo watatekeleza katika maeneo ambayo gesi imegunduliwa vikiwemo vyanzo vya Zafarani, Lavani na Tangawizi katika kitalu namba 2 kilichopo mashariki mwa Mkoa wa Lindi.

maandalizi ya tamasha la pasaka yakamilika,rebecca malope kutumbuiza jijini mwanza.



MKurugenzi wa Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha la krismass na Pasaka,Bwa.Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar mnamo April,20 mwaka huu yamekamilika.

Aakizungumza na Waandishi wa habari jijini dar leo katika viwanja vya Karimjee,Msama amebainisha kuwa kila kitu kimekwishakamilika,wakiwemo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza siku hiyo,aidha amesema kuwa pamoja na wanamuziki wa nyumbani kushiriki tamasha hilo,pia kutakuwepo na wanamuziki wengine kutoka nje ya nchi.

Msama amesema kuwa katika kuhakikisha washabiki na watazamaji wanalifurahia tamasha hilo lenye kujaa nyimbo za kumsifu na kumuabudu Mungu,kutakuwepo na wanamuziki nyota kutoka nchini Afrika kusini,ambao watalipamba vyema tamasha hilo.

"Katika tamasha hilo kutakuwepo na wanamuziki kutoka Afrika kusini,akiwemo Rebecca Malope  mbaye atatumbuiza kwenye hitimisho la tamasha hilo jijini Mwanza,pamoja na Mwanamuziki Kekeletso Phoofolo ambaye atatumbuiza hapa jijini Dar,wakiwemo na wanamuziki wengine wengi wa hapa nyumbani kama vile Rose Muhando,Upendo Nkone,Bon Mwaitege,John Lisssu,Upendo Kilahilo na wengineo wengi" alisema Msama.
Msama amesema kuwa Tamasha hilo litazunguka mikoa isiyopungua tisa,ameongeza kuwa pia katika kuisadia jamii,Kamati ya maandalizi ya tamasha la pasaka itaandaa fungu Maalum kwa ajili ya kuwapa Mayatima na watoto waishio katika mazingira magumu.

Sisi kama Msama Promotions tutaandaa fungu rasmi kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima,lengo likiwa ni kuwapa fungu maalum kwa ajili ya kujitegemea,mfano kuwaanzishia biashara ambayo itakuwa endelevu na yenye kuwasaidia badala ya kupewa vitu vya kupita tu kila wakati"alisema Msama.

Amesema kuwa watatoa fungu maalum kwa kila kituo kwa kuwapa kiasi cha shilingi Milioni tano kwa kila kituo ili kujiendeleza zaidi,na tunalitoa kutokana na mapato ya Pasaka,na mapato mengine yatatumika kuendeleza ujenzi wa kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu ,Kituo cha Watoto kiitwacho Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa wasiojiweza.

SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE


 Timu ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General Tyre jijini Arusha
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyeusi) akioneshwa moja ya mashine zilizokuwa zinatumika kutengenezea matairi katika kiwanda cha General Tyre kilichopo katika jiji la Arusha na Mwangalizi wa Kiwanda hich, Bw. Leonald Mgoyo. Serikali ina mpango wa kukifufua kiwanda hicho baada ya kusimama uzalishaji tangu mwaka 2007.
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyusi) akiagana na Mwangalizi wa Kiwanda hicho, Bw Leonald Mgoyo baada ya 

ukaguzi wa kiwanda hicho. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la

 Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Gideon Nasari na kushoto kwake ni Naibu Katibu 
Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uzalishaji, Bw Maduka 
 Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakifurahia jambo wakati wa ukaguzi huo.

Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango 

wakitazama bidhaa zilizokuwa zikitengenezwa na kiwanda cha matairi 

cha General Tyre. Serikali ina mpango wa kufufua kiwanda hicho ambacho 

kilisimama uzalishaji tangu mwaka 2007.

KUTOKA DODOMA,HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA KATIBA

NI SAA 9 NA DAKIKA 50 VIONGOZI WA KITAIFA WAMEANZA KUINGIA
BUNGE LA KATIBA
Viongozi wa Serikali wanaingia,Rais Mstaafu wa Zanzibar Mh:KARUME 
SASA ANAINGIA RAIS MSTAAFU ALLY HASAAN MWINYI..
Anaingia Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mh:Makungu
Anaingia Jaji Mkuu wa Tanzania Chande Othuman,.
Anaingia Rais wa Zanzibar Mh:Ally Mohamed Shein
Anaingia Makamu wa Rais Mh;Bilal

HIVI SASA NI SAA 10:000 KWA SAA ZA HAPA TANZANIA MH:RAIS WA JMT KIKWETE ANAINGIA AKIWA AMEONGOZANA NA MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA MH:SAMWEL SITTA.
 Saa 10:01 Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mh:Samwel Sitta anaomba Dua Maalumu ya Bunge.
 Saa 10:03 Mwenyekiti wa Bunge Maalumu anasoma Itifaki ya Kutambulisha Viongozi Wakuu wa Serikali
Wazee Mh:Samweli Malecela na Pius Msekwa.
Watu Mashuhuri yupo Mama Maria Nyerere(Mke wa Muasisi wa Nchi hii Hayati Julius Kambarage Nyerere).
Pia Wanawake wa Viongozi takribani wote wa Viongozi wa serikali wapo wakiongozwa na Mama Salma Kikwete.
Wakuu wa Usalama,Meya wa  Manispaa ya Dodoma na Mabalozi mbalimbali.
SAA 10:07 MWENYEKITI WA BUNGE MAAALUMU ANAMSIMAMISHA RAIS WA JMT AHUTUBIE BUNGE MAALUMU LA KATIBA.
Saa 10:08 Rais anaanza Kusoma hotuba yake kwa Kusoma Itifaki ya Viongozi ndani ya Bunge.
HINTS ZA HOTUBA YA RAIS MUDA MUDA HUU DODOMA.
>Nawapongezeni kwa Kuwa sehemu ya Kuandika historia Mpya kwa Taifa la Tanzania,Mkitunga Katiba Bora Majina yenu yataandikwa kwa Wino wa Dhahabu.
>Naombeni Mtunge Katiba Itakayo Dumisha Umoja wetu,Asili zetu,Katiba ambayo haitatutenganisha kirangi,Kisiasa au Kiimani. 
 >Kihistoria hii ni Mara ya 3 Katiba ya Tanzania Inatungwa Upya,Tofauti na Vipindi Vingine.Kipindi hiki Utungaji wa Katiba Umeshirikisha Wananchi wengi zaidi. 
Msukumo Mkubwa sana wa Kudai Katiba Mpya Ulianza baada ya Mfumo wa Vyama Vingi,Wengi walizani kuwa Kudai kudai Katiba Mpya kutawasaidia Kushinda chaguzi dhidi ya CCM.La hasha!!! 
>Desemba Mwaka 2012 nilitangaza Kuanza Mchakato wa Kutunga Katiba Mpya,Kazi hii ilipewa Tume ya Kukusanya Maoni ya Watanzania..
Mchakato Mzima wa Katiba Utahitimishwa na Wananachi kwa Kuipigia Kura ya Maoni kama wanaikubali Katiba au La!!! 
Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Mpya Tar.18/03/2014 hapa Bungeni,Ilikuwa ndio Mwisho wa Kazi ya Tume ya Warioba kazi iliyobakia ni Kwenu Wabunge. 
>Naishukuru sana Tume ya Warioba Rasimu walioitunga inaleta Mambo mengi kwenye Katiba Mpya ya Tanzania,Ni Rasimu Nzuri.
Rasimu inamambo mengi sana .
Naombeni sana Msome Rasimu ya Katiba Yote kwa Makini,Sio unafundishwa cha Kusema,Unafundishwa Uzungumze nini.Akili za Kuambiwa Chnganya naza kwako.
Kama Kuna Jambo halifai kwenye Rasimu Wajumbe Msisite kulifuta.

Tungeni Katiba ambayo Watanzania wataipenda,Sio Mtunge katiba baada ya Muda Mfupi manataka kurekebisha,Msitunge Katiba Mpya isiyoweza Kutekelezeka.
 #‎kikwete‬ Kuna sehemu Rasimu Inamapungufu sana.,Ibara ya Pili inaacha Maziwa na Mito kuwa ni Sehemu ya Tanzania.
MUUNDO WA SERIKALI TATU.
Kuna Mambo yanayopendekezwa na Tume Mf.Viwanda,Afya n.k yapo kwenye Serikali ya Nchi za Ushirika.
Serikali ya Muungano inahusisha,Katiba,Usalama (Baadae bado) 
Mambo mengi yanatekelezeka Kupitia Serikali ya Muungano tuliyo nayo sasa,Rasimu ya Serikali tatu inawaweka wapi watumishi?Naomba Msome sana Rasimu yote. 
 #KIKWETE Ibara ya 128 inayoleta dhana ya Kupoteza Ubunge kutokana na Kutofanya kazzi za Kibunge kwa Tatizo la Maradhi au kiuzini kwa Muda wa Miezi 6.Someni kwa Makini kipendele hiki,Jambo hili liwekwe Vizuri.
Yaani Mbunge augue Miezi sita Mfululizo eti afukuzwe,Huu ni Ukatili Usiotakiwa kwenye Katiba Mpya.

Pia kuhusu Mbunge kuwa Bungeni kwa Vipindi Vitatu,Sasa Kama Mtu ameingia akiwa na Miaka 25 anamaliza akiwa na Miaka 40.Hii si sawa,Ni kunyimana Fursa.Hatuwezi Kupata Viongozi wa Kutengenezwa kwa Namna hii,Viongozi watatoka wapi wakati kila anapofikia hatua ya Kukomaa Ukomo wake umefika.

 #KIKWETE MUUNDO WA SERIKALI,Hii ndio Ajenda Mama,Ombi langu Kwenu Kwanza Muwe watulivu mnapojadili Swala hili,Mkilijadili kwa Jazba wenye hasira hawa Jengi,Wenye hasira hawatengenezi jambo Vizuri.Uamuzi usio kuwa sahihi kwenye Jambo hili Unahasara Kubwa,Tanzania inaweza kuwa Nchi iliyojaa Migogoro yenye Matatizo ambayo hatujawahi kuwa nayo.
Kudai Serikali tatu sio Jambo Jipya,Ulikuwepo wakati Wa Kuunganisha Nchi zetu Mbili,Wakaamua Serikali mbili.
Imependekezwa Mara Nyingi lakini Halikukubarika,Bora Mzungumze kama linakubaliwa likubaliwe,kama Linakataliwa Likataliwe.
Waasisi wa TAIFA LETU Waliamua Kuchagua Muundo wa Serikali Mbili.
1.Ni muundo Usio Imeza Zanzibar.
2.Ni Muundo Inayomuepushia tanganyika Kubeba Muundo wa Muungano n.k.
Ni vigumu sana Kuacha Kujadili Figa za Wazee wetu hawa,Wao ndio Wakwanza kutuletea Mfumo huu.
Zungumzeni hoja zao,Zungumzeni muone hoja zao.
Mfanye Maamuni "Informed Decision" .Wapeni Heshima ya Kujadili Mawazo yao,Yanani ni Bora kuliko ya hawa Wazeee??

TUME IMETOA SABABU MBIL ZA SERIKALI TATU.
1.Ni maombi ya Watanzania wengi
2.Muundo wa Serikali tatu unatoa Majibu sahihi ya Changamoto za Muungano wa sasa.
WAPO WANAOKUBALIANA NA TUME NA WAPO WASIOKUBALIANA NA TUME

TAZAMA PICHA ZINGINE 8 JINSI AJALI YA LORI LILILOGONGA MAGARI 5 UBUNGO MCHANA LEO


 Basi la UDA likiwa limebebwa kwa juu katika eneo la tukio
 
 
 
 
 
Ajari mbaya iliyo husisha magari takribani 5 imetokea maeneo ya ubungo mkabala na stendi ya mabasi ya mikoani ikihusisha magari ya abiria uda na gari zingine ndogo mpaka sasa haijajulikana idadi sahihi ya watu walio poteza maisha

AJALI MBAYA YATOKEA KITUO CHA MABASI UBUNGO LEO









Ajali mbaya imetokea muda mfupi uliopita kituo cha Ubungo lango kuu la kuingilia mabasi yatokayo mikoani. Ajali imehusisha magari 6 likiwemo UDA. Lori lafeli break na kusababisha uharibifu Mkubwa wa Magari na watu kuumia vibaya sana kituo cha Mabasi Ubungo. Magari kibao yafinyangwa. Mpaka sasa haijajulikana idadi ya watu waliopoteza maisha.

Kuhusu kuonekana Australia kwa vipande vya ndege ya Malaysia iliyopotea.


Screen Shot 2014-03-21 at 3.36.25 PM
March 20 2014 Waziri mkuu wa Australia alitangaza bungeni kwamba nchi yake kupitia picha za satellite imeona vipande kwenye bahari ya hindi ambavyo vinaaminika kuwa mabaki ya ndege ya Malaysia iliyopotea ikiwa na abiria 239 March 8 2014.
Saa kadhaa baada ya
hizo taarifa kutoka, ilitangazwa kwamba vikosi vya uokoaji vimeshindwa kufika kwenye eneo hilo la tukio baharini kutokana na hali mbaya ya hewa iliyochangiwa na mvua.
Leo March 21 2014, taarifa kutoka vyombo vikubwa mbalimbali vya habari duniani, imefahamika hakuna kilichoonekana eneo la tukio kwenye bahari ya hindi ambako ‘ilisemekana’ vipande vya ndege hiyo iliyopotea vimeonekana hivyo vikosi vya uokoaji vimeondoka eneo hilo.

PICHA ZA MOTO ULIOTEKETEZA SEHEMU YA HOTELI YA PICOLO BEACH

Pichani juu ni taswira za sehemu ya Hoteli ya Pecolo Beach iliyopo Kawe jijini Dar iliyoteketea kwa moto leo mchana. Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyoanzia kwenye nguzo iliyopo jirani na hoteli hiyo

PISTORIUS KUUZA NYUMBA YAKE YA KIFAHAR

Nyumba ya kifahari ya Oscar Pistorius
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorious atauza nyumba yake ili aweze kumudu gharama ya kesi ya mauaji inayomkabili.
Hii ni kwa mujibu wa wakili wake Brian Webber ambaye amenukuliwa na Shirika la Wanahabari La Afrika Kusini (SAPA) akisema kesi hiyo itaendelea kwa zaidi ya wiki tatu zilizotarajiwa kwa kesi hiyo kukamilika.
Oscar hajaweza kurejea katika nyumba yake hata baada ya maafisa wa uslama kumruhusu arejee huko zaidi ya mwaka mmoja uliopita huku uamuzi ukitolewa wa nyumba ile kusalia ikiwa imefungwa hadi pale kesi hiyo itakapo kamilka.
Kwa Mujibu wa SAPA, hati za kortini zilizoandikishwa mwaka jana wakati mwanariadha huyo alipokuwa akiwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana zaonyesha kuwa nyumba hiyo iliyo katika mtaa wa Silverwoods ina thamani ya Randi millioni 5 ambazo ni sawia na dola za marekani 457 000.
Oscar anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake mnamo tarehe 14 mwezi wa Februari mwaka jana huku akisema kuwa alimpiga risasi kimakosa.
Kesi ya mauaji dhidi yake ambayo kwa sasa iko katika wiki ya tatu, imehairishwa hadi siku ya jumatatu ambapo mashahidi wengine watano wa upande wa mashitaka wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kabla ya yeye kupewa fursa ya kujitetea.
Upande wa mashitaka unadai kuwa Pistorious alimpiga risasi Bi Steenkamp, aliyekuwa mwana mitindo, mtangazaji maarufu wa runinga na mwana sheria baada ya kinachodahniwa kuwa ugomvi wa nyumbani.
Huku kwa upande wake, Pistorious akisema kuwa aliamini kuwa mpenzi wake alikuwa amelala na akidhani kuwa palikuwa na mwizi nyumbani kwake alifyatua risasi kuelekea chooni asubuhi mapema mnamo tarehe 14 februari mwaka 2013.
Iwapo mwanariadha huyu mwenye umri wa miaka 27 atapatikana na hatia , huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha

Wednesday, March 12, 2014

Picha nne za tukio la Ajali ya Basi la Hood

Basi la Kampuni ya Hood likiwa limepinduka na watu kuumia vibaya Same,Kilimanjaro chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.


Kuhusu kesi ya Mramba na Yona,hiki ndicho kilichoamuliwa na Mahakama leo.


BASIL YONA
Leo March 11 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi  Mawaziri Waandamizi wa zamani ambao ni Basil Mramba na Daniel Yona wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
Matumizi hayo mabaya ya madaraka yanadaiwa  kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7  kwa kutoa msamaha wa kodi.
Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji John Utamwa baada ya washtakiwa hao kuwasilisha maombi ya kwenda kutibiwa nje ya nchi ambapo Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na maombi hayo.
Baada ya kusikiliza ombi hilo Jaji Utamwa alisema
mahakama inawaruhusu washtakiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kutibiwa na kwamba pamoja na ruhusa hiyo amewataka Mramba na Yona kuwepo mahakamani siku ya kusikiliza kesi hiyo Aprili 22 mwaka huu.
Katika kesi hiyo inayowakabili Mramba na Yona piamshtakiwa mwingine ni Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha Gray Mgonja,Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Aprili 22 hadi 25, mwaka huu.
Katika kesi ya msingi washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.
Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation  waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
YONA+CHRGE+2
YONA+CHRGE

Matokeo ya UEFA Usiku wa leo Jumanne na Waliofunga hawa hapa

Mapya na Mazito kuhusu Kesi ya Babu Seya na Wanaye haya hapa,Duhhh hatari

WAKILI maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando amesema mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake watatu walimbambikiwa kesi.


Mabere Nyaucho Marando akiongea na waandishi 
Akizungumza na waandishi wa habari wa Global Publishers katika ofisi zao zilizopo Mwenge Bamaga mwishoni mwa wiki iliyopita, Marando alisema alipitia jalada la kesi hiyo lenye kurasa 1,362 na kugundua kuwa hakuna hata sehemu moja inayomhusisha kigogo mmoja wa nchi, lakini kesi walikuwa wamebambikiwa.
Hakutaja waliombambikia. Baadhi ya mahojiano ya Marando na waandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Wewe uliwatetea Babu Seya na watoto wake, unaweza kutueleza ilikuwaje ukatafutwa wewe kuwatetea?
Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
Marando: Kuna rafiki yangu alikuja kuniomba nifanye kazi ile, nilikataa hasa kwa kuwa nami nina watoto wa kike. Baadaye nilikubali kwanza kusoma jalada la kesi lenye kurasa 1,362 nikaona hawakufanya makosa waliyoshitakiwa, walibambikiwa nikaamua kuwatetea katika ngazi ya rufaa, niliwatetea bure kabisa.
Mwandishi: Kama hivyo ndivyo, ina maana makosa walibambikiwa?
Marando: Ndiyo, naamini makosa yale walibambikiwa lakini siyo na kigogo yeyote wa serikali katika nchi hii. Lakini Mahakama ya Rufaa haina makosa, Babu Seya na wanawe walikuwa wamehukumiwa na magazeti. Nyinyi waandishi mlimhukumu kwa hii fabricated case (kesi ya kutunga) na sababu zipo.
Mwandishi: Je, kuna njia yoyote iliyobaki ya kumtoa Babu Seya na mwanaye?
Marando: Mimi kama wakili, hapo ndiyo mwisho wangu, nimenyoosha mikono. Nimeshindwa nusu, nimeshinda nusu (Kwa kuwatoa jela Mbangu na mdogo wake Francis Nguza na kubaki jela Nguza na Papii.)
Mwandishi: Umekuwa Chadema na kuna habari kuwa uliondolewa kuwa mwanasheria wa chama akapewa Tundu Lissu,pia kuna habari kuwa umekosana na mwenyekiti wako, Freeman Mbowe, Je,  kuna ukweli wowote juu ya hayo?
Marando: Sijawahi kuwa mwanasheria wa Chadema isipokuwa wanapokuwa na tatizo la kisheria huwa nawapa ushauri wakihitaji. Mheshimiwa Mbowe sijakosana naye isipokuwa katika vikao tunaweza kutofautiana na hivyo ndivyo chama makini kilivyo. Wote hamuwezi kuwa na wazo moja katika hoja, baadaye inapigwa kura, upande unaoshinda na unaoshindwa huwa kitu kimoja. Hakuna ugomvi hapo, mimi ni Makamu  Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu.
Mwandishi: Lipo suala kuwa wewe ni usalama wa taifa na ulihusika na mauaji ya Komandoo Tamim, Je, hilo unaweza kulifafanua?
Marando: Mimi nilijiunga na usalama wa taifa na nilikuwa kitengo cha mambo ya nje hasa kuhusu vyama vya ukombozi enzi hizo. Niliacha kazi hiyo kwa kukabidhi barua kwa aliyekuwa mkurugenzi wake, Dk. Hansy Kitime baada ya kulazimishwa kujiunga na TANU kwani sikuwa mwanachama. Kuhusu Tamim aliuawa mwaka 1983 wakati huo mimi nilikuwa nimeshaacha kazi.
Hili la kuua walikuwa wakinipakazia watu wa usalama wa taifa bila shaka kwa sababu niliacha kazi kijeuri nikawa jobless (sina kazi).
Baadaye nikaajiriwa Shirika la Sheria Tanzania kabla ya kuanzisha kampuni yangu ya uwakili mwaka 1984. Nimefafanua hili mara nyingi sana, nadhani leo mmenielewa na Watanzania watanielewa

Breaking news ya Radio One kuhusu waliokamatwa kituo cha mabasi Ubungo.


Screen Shot 2014-03-12 at 1.51.39 AM
Screen Shot 2014-03-11 at 11.35.01 PM

Huu ndio Mkoko Wa Samwel Etto ambao Kwa Wachezaji yeye Pekee anamiliki,Ni Balaa


Screen Shot 2014-03-12 at 2.55.30 AM 
Hili ni moja ya magari ambayo tumezoea kuyaona kwenye video za muziki za gharama kubwa lakini pia hata kwenye baadhi ya movie za Hollywood.
Unaambiwa hili ni moja ya magari ya kifahari anayomiliki staa wa soka Samuel Eto’o ambae anaichezea Chelsea sasa hivi huku akitajwa kuwa staa wa soka anaeshika namba 3 kwa utajiri duniani akiwa nyuma ya Ronaldo anaeshika namba 1, na Lionel Messi anaeshika namba 2.
Hizi ni baadhi tu ya pichaz kutoka kwenye video yenyewe hapojuu ambayo ndio unaweza kulitazama hili gari vizuri hata kumuona yeye mwenyewe akiliendesha.
Screen Shot 2014-03-12 at 2.55.44 AM
Screen Shot 2014-03-12 at 2.56.15 AM
Screen Shot 2014-03-12 at 2.57.03 AM

JK ATANGAZA KULA SAHANI MOJA NA MAJANGILI

Wawakilishi wa Chama cha Uhifadhi wa Wanyama cha Frankfurt (FZS), wakikabidhi magari zaidi ya 11 kwa Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusaidia vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori katika hifadhi na mbuga za taifa.Picha na Ikulu
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imenuia kumaliza kabisa ujangili nchini, ikiwa ni hatua ya kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.
Hakusita kusisitiza kwamba, nia ya dhati ya Serikali ni kuhakikisha mkakati huo unakamilika, japokuwa kumekuwa na changamoto zinazotokana na ukubwa wa hifadhi hizo na uhaba wa vitendea kazi pamoja na askari wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa kupokea magari 11 ya kisasa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili kutoka kwa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la Ujerumani, Kikwete alisema tatizo hilo limekuwa la muda mrefu, lakini juhudi za kulikomesha zinafanyika.
Alisema, pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna tatizo la uhaba mkubwa wa wafanyakazi wanaotakiwa kudhibiti majangili, ambapo kwa sasa kuna wafanyakazi 1,155 sawa na asilimia 24 tu ya mahitaji halisi ya wafanyakazi 4,000 wanaohitajika.
"Mwaka uliopita, Serikali ilisimamia ajira ya wafanyakazi 449 na sasa kuna ajira ya wafanyakazi 500.
Kwa maana hiyo tutafikisha wafanyakazi wapya 949 na kufanya mahitaji ya wafanyakazi wapya kuwa 4,000 zaidi ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu kwa viwango vya kimataifa," alisema.
Kwa mujibu wa viwango vilivyopo sasa, mfanyakazi mmoja anasimamia eneo la kilometa za mraba 169 ikilinganishwa na viwango vya kimataifa vya kilometa za mraba 25 kwa kila mfanyakazi mmoja.
Rais Kikwete alisema kwa sasa Serikali itaendelea kuajiri idadi hiyo ya wafanyakazi kila mwaka kwa miaka mitatu ijayo ili kuhakikisha pengo lililopo linazibwa.
Alisisitiza kuwa, kampeni dhidi ya ujangili ni suala la kimataifa na Tanzania au nchi zilizoathirika hazitaweza kulikabili bila ushirikiano wa kimataifa.
Alisema upo ulazima wa kuteketeza mitandao yote ya ujangili na kuwawajibisha ipasavyo watakaonaswa, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kulinda urithi huo wa dunia.
Ukosefu wa vifaa
Akifafanua, Rais Kikwete alisema kuongeza idadi hiyo ya wafanyakazi pekee haitakuwa na maana iwapo hawatakuwa na vifaa maalumu vya kisasa vitakavyowawezesha kukabiliana ipasavyo na tishio la ujangili.
Katika mkakati wa maboresho hayo, Kikwete alisema wanafanya jitihada za kuongeza idadi ya magari, kuongeza vifaa vya kisasa kwa ajili ya doria na vifaa vya mawasiliano, ambavyo vinahitaji uwezo mkubwa wa kifedha ambao utaweza kutekelezwa na serikali kwa kipindi kirefu iwapo haitapata msaada wa uwezeshaji kutoka kwa wadau.
Msimamo wa Wizara
Akizungumzia msimamo na mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Waziri Lazaro Nyalandu alisema kutokana na ukubwa wa tatizo, wanahitaji vifaa vya kisasa zaidi, ikiwamo helikopta na ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kufanya doria kwenye maeneo yote ya mbuga na hifadhi za taifa.
Aliwatahadharisha wafugaji wanaopenda kuingiza mifugo yao kwenye maeneo ya hifadhi, akiwataka kuondoa mifugo yao mapema kwa kuwa katika operesheni hiyo hakuna atakayeachwa.
"Katika operesheni hii, hakuna jangili wala mfugaji atakayeachwa iwapo atakutwa kwenye maeneo ya hifadhi," alisema.
Alifafanua kwamba, msaada huo wa magari utapelekwa maeneo tofauti, matano kanda nane za Selous, mengine matano Hifadhi ya Serengeti na moja Hifadhi ya Maswa.
Mwaliko wa vyombo vya habari
Nyalandu alisema Wizara yake imevialika vyombo vyote vya habari vya kimataifa kwa ajili ya kuja kupata taarifa sahihi kuhusu kampeni dhidi ya ujangili zinavyotekelezwa ili kuepuka ripoti za upande mmoja kwa ajili ya kuweka usawa.
Alisema hatua hiyo ilichukuliwa na wizara yake walipokwenda kwenye mkutano maalumu na Rais Kikwete ulioandaliwa na mtoto wa Mfalme wa Uingereza, Prince Charles kwa ajili ya kuangalia namna ya kulinda wanyama walio hatarini kutoweka duniani, wakiwemo tembo na faru