Wednesday, July 22, 2015

AWASHUKURU WATANZANIA BAADA YA KUPATA TUZO DIAMOND

Diamond akisikiliza masali kutoka kwa waandishi wa habari.
… Akijibu maswali.
…Bab Tale akiwakaribisha waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mmoja wa mameneja wa Diamond, Said Fella (Mkubwa na wanawe) akieleza jambo kwa waandishi wa habari.
Mwakilishi kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, Hamza Dalla akifuatilia kwa makini kikao hicho.
….Akiwa ameshikilia tuzo yake baada ya kumalizika kwa kikao na waandishi wa habari.
Akiwa katika pozi ya la kufurahia tuzo hiyo.
Mwandishi wa habari wa Global Publishers, Brighton Masalu (kushoto) akiwa ameshikilia tuzo ya Diamond.
Diamond (katikati) akiingia ukumbini humo akiwa na mmoja wa mameneja wake, Bab Tale (mwenye shati jekundu).
Baadhi wa waadishi wa habari wakimfuatilia kwa umakini mkubwa.
SIKU chache baada ya kurejea nchini akiwa na tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa kiume (Best Live Act), mfalme wa muziki wa Bongo fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewashukuru Watanzania kwa moyo wa upendo waliouonesha kwa kumpigia kura na kumuwezesha kutwa tuzo hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ndani ya Hoteli ya Ntansoma jijini Dar, pia  msanii huyo aliitaka serikali na makampuni binafsi kuwaunga mkono wasanii wachanga wanaotamani kuutangaza muziki wetu katika anga la kimataifa kutokana na kile alichokiita ugumu na changamoto nyingi.

Friday, May 29, 2015

JOKATE: ALI KIBA NDIO KIBOKO YANGU

Na Mabantanyau Family
MREMBO :mchakarikaji Bongo,  Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, juzikati aliamua kuvunja ukimya na kusema kuwa mwanamuziki Ali Kiba kwa sasa ndiye kila kitu katika mambo yake mengi ya kimaisha.
Mrembo mchakarikaji Bongo,  Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Akizungumza na Mabantanyau Jokate alisema, watu wanaongea sana kuhusiana na ukaribu wao bila kujua kuwa Kiba ni mtu wake kitambo na sasa ndiye kila kitu kwake kwani ana projekti naye kibao ambazo zinakuja na wasioelewa, ipo siku wataelewa.
Mwanamuziki Ali Kiba.  (DK)
“Yaani watu wangu wajue Kiba ni kila kitu kwangu ila siyo ishu ya mapenzi, tuna projekti kibao, nawaomba watu wavute subi--ra watajionea kila kinachoendelea kati yetu.Kuanzia sasa Kiba atakuwa akipeperusha ‘brand’ za Kidoti kwa kila atakachofanya ikiwa ni pamoja na mavazi,” alisema Jokate.

Sunday, April 12, 2015

AJALI KUBWA YATOKEA YA BASI LA ABIRIA NA LORI LA FUSO LEO

Basi la abiria la NGANGA lililogongana na fuso na kuwaka moto
Basi hilo la Nganga likiteketea kwa moto
Gari la kubebea mizigo aina ya fuso likiwa linateketea kwa moto
Habari zilizotufikia punde zinasema watu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto maeneo ya milimani kilomita kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. Pichani ni basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara zitapopatikana.

.YANGA YAITANDIKA MBEYA CITY 3 - 1 TAIFA


Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiwatoka Mabeki wa Timu ya Mbeya City wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa hivi sasa.Yanga imeishia Bao 3 - 1.
Kiungo Mchezeshaji wa timu ya Yanga, Haroun Niyonzima akiangalia kwa kupeleka mpira wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa hivi sasa.Yanga imeishia Bao 3 - 1.
Kipa wa Mbeya City, Hanington Kalyesubula akiangalia mpira wavuni huku washabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakisangilia ushindi ushindi na washabiki wao.
Kipa wa yanga akiwa kazini tayari kabisa kujiandaa kuzuia mpira.

Friday, April 10, 2015

MGOMO WA MADEREVA WATIKISA NCHI

Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.
Wakina mama hawa wakiwa wamemshikilia Mgonjwa wao waliekuwa wakimsafirisha kwente mkoani, wakiondoka stendi ya kuu ya Mabasi Ubungo baada kukosa usafiri kutokana na mgomo wa vyombo hiyo leo.
Huku Ubungo mambo yako namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.
Mijadala ikiendelea kwa wadau mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar.
Mara lori likazuiliwa na watu hawa, wakidai kuwa amepakia abiria hivyo anatakuwa kuwashusha kama anataka kuendelea na safari yake.
Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama barabarani.
Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.
Uongozi wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni, kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka

Wednesday, March 11, 2015

AJALI YAUWA WATU ZAIDI YA 50 LEO MAFINGA

                                          





                                                                                               BREAKING NEWS:



 Ajali imetokea changalawe Mafinga basi la Majinja lilikuwa linatokea Mbeya kwenda Dar limeangukiwa na kontena muda huu na watu wengi wanakadiriwa kufariki na hali ni mbaya sana
Watu wapatao 50 wanahofiwa kufa papo hapo baada ya basi hilo la Majinja Express kugongana na lori na kuangukiwa na kontena

Tuesday, March 10, 2015

MATUMLA JR. KUMVAA MKOREA MACHI 27 MWAKA HUU

Bondia mkongwe nchini Rashid Matumla, kutoka kushoto, Mohamed Matumla, Japhet Kaseba na Rais wa (TPBO), Yassin Abdallah 'Ustaadh' katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).(P.T)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Rais wa TPBO, Yassin Abdallah 'Ustaadh'.
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Mohamed Matumla Jr ambaye ni mtoto wa gwiji wa zamani wa mchezo huo, Rashid Matumla ‘Snake Boy’ anatarajia kupanda ulingoni Machi 27, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kugombania nafasi ya kwenda kushindania ubingwa WBF dhidi ya Mkorea, Wang Xi Hua.
Licha ya hivyo, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustaadh’, amewataja mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, kuwa ni Japhet Kaseba atakayegombania ubingwa wa UBO Afrika dhidi ya Mada Maugo huku Thomas Mashali akitarajia kuwania ubingwa UBO  Afrika kilo 76 dhidi ya Karama Nyilawila

ARSENAL YAITOA KOMBE LA FA MAN UTD

WELBECK
Timu ya Arsenal usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA baada ya kuwalaza mahasimu wao Manchester United kwa jumla ya mabao 2 -1.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Danny Welbeck aliyerejea Old Trafford akiwa na Arsenal ndiye aliyepigilia msumari wa moto kwenye kidonda baada ya kupachicha goli la pili lililoipeleka moja kwa moja Arsenal kwenye hatua ya nusu fainali.

Friday, March 6, 2015

ALBINO WAZICHAPA KAVUKAVU IKULU DAR ES SALAAM




Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), wamepigana ngumi na mateke wakigombea kuingia kumwona Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam. Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ambapo lilianzia kwenye eneo la mapokezi Ikulu mara baada ya walemavu hao kukaguliwa na kuwekwa kwenye chumba maalumu cha kupumzikia wageni. Baada ya muda, ofisa wa Ikulu alifika kwenye chumba walipokuwa walemavu hao akiwa na karatasi yenye orodha ya watu 15, ambao ndio waliopaswa kumwona Rais. Kila ofisa huyo alipokuwa akisoma jina, mhusika alitoka nje ya chumba hicho tayari kwa kwenda kumwona Rais. Baada ya ofisa huyo kumaliza kusoma majina hayo, alisema: “Hawa ndio wanaokwenda kuwawakilisha kwa sababu hamuwezi kuingia kundi lote hili.”Wale wengine walioachwa hawakukubaliana na hali hiyo basi vurugu ndio likaanzia hapo!

Thursday, January 22, 2015

Dogo Aslay Ndani ya Penzi Zito na Naima

Jamani Mahaba Kitu Kingine , Mwanzo tulijua Nuhu Mziwanda pekeake ndio mwenye ujasiri huu wa kujichora tattoo ya mpenzi wake ..lakini sasa list imeongezeka , Mrembo Naima nae avunja Ukimya , Ajichora Tattoo ya mpenzi wake Dogo Aslay .
Naima ni yule binti aliyekuwaga kwenye beef na Wema Sepetu wakimgombania CK.

Jack Patrick Amepitwa na wakati sasa ni Vanessa Mdee Penzi motomoto Asema JUX

Jux na Vanessa Mdee hawataki tena kuficha uhusiano wao. Tangu mwaka mpya uanze, waimbaji hao wameuachia ulimwengu ufahamu kuwa ni wapenzi na wanapenda baada ya kipindi kirefu cha tetesi za uhusiano wao ambazo walikuwa wakizikanusha.

Uhusiano huo umepelekea hadi Jux amtumie Vee Money kama mpenzi wake kwenye video ya ‘Sisikii’ na kama umeitazama utakuwa umegundua chemistry ya kuvutia kati yao.

Weekend hii wawili hao wakiwa pamoja na Navy Kenzo, walikuwa na show visiwani Zanzibar ambapo Jux pamoja na kutumbuiza nyimbo zake, alipanda jukwaani kumpa kampani mpenzi wake huyo kwa kuchukua nafasi ya Barnaba wakati alipokuwa akitumbuiza wimbo ‘Siri’.

Baada ya show hiyo wapenzi hao walijumuika pamoja kula upepo kwenye beach za Zanzibar na mashabiki wao wanafurahia tu kuwaona pamoja.

Jack Patrick Kabla hajakamatwa na Madawa ya Kulevya Maccau Ndio alikuwa Mpenzi wa Jux , Akitoka Jala Atakuta Jux si wake Tena

Monday, December 29, 2014

TIMU MASHABIKIIIII NI MSEMO SAHIHI KABISA

Shabiki huyu alikuwa kivutio kikubwa kwenye mechi baina ya Mbeya city na Ndanda fc
Shabiki huyu katoka Mtwara kuishabikia timu yake ya Ndanda.

NYALANDU ATAKA KUWANIA URAIS 2015

Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM",

Sunday, December 7, 2014

IDRISS SULTAN ASHINDA SHINDANO LA BIGBROTHER....

1_7ebc0.jpg
IMG-20141207-WA0091_f9182.jpg
Idriss Sultan Mtanzania aliyetikisa Bigbrother leo ameibuka mshindi wa shindano hilo na kuwabwaga washiriki kutoka mataifa mbalimbali yaliyoshiriki katika shindano hilo akiibuka na kitita cha shilingi milioni 500 za Kitanzania katika shindano hilo lililokuwa likiendelea kwa miezi mitatu nchini Afrika Kusini Idriss ni Mtanzania wa tatu kushinda shindano hilo akitanguliwa na Mwisho Mwampamba na Richard wote wakiwakilisha vizuri taifa la Tanzania katika shindano hilo, Mabantanyau blog inampa hongera sana Idriss kwa ushindi huo na inamtakia kila mafanikio katika maisha yake

Saturday, September 13, 2014

MAYWEATHER ASHINDA PAMBANO LAKE DHIDI YA MADINA LEO ALFAJILI



Mayweather v/s Maidana

Mayweathet ashinda pambano lake la ubingwa wa WBC/WBA welterweight championship ambao umemalizika Alfajili ya kuamkia jumapili Sept 14 2014 leo.Mayweather ameshinda pambano lake hilo kwa point dhidi ya mpinzane wake Maidina japo pambano lilikuwa kali sana na kusisimua.Lilikuwa na laundi kumi na na mbili na zimeisha zote bila matatizo ingiwa katika raundi kama ya tisa hivi Madina alikatwa point  baada ya kumpiga kwa kiwiko na kumsukuma mayweather na kudondoka chini na refa wa mchezo huo kuamuru Madina kukatwa point kwa kosa hilo.
MWANDISHI:MABANTANYAU FAMILY

Wednesday, September 10, 2014

MIFUPA YA DINOSARIA YAPATIKANA HUKO MKOANI RUKWA TANZANIA

mifupa db4e2
Aina mpya ya dinosaria imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania. Mabaki hayo ya dinosaria yaliyopewa jina la - Rukwatitan Bisepultus - yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi mwa nchi hiyo. Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka mia moja iliyopita, na alikuwa na uzito sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita mbili. Mnyama huyo ni aina ya titanosaurus -- ambao ni wakubwa, na wanaokula nyasi. Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chaki iliumbika) takriban miaka milioni mia moja na arobaini iliyopita

NYANGUMI ALIYEKUFA AIBUKIA PWANI YA MTWARA

Mzoga wa samaki aina ya nyangumi ukiwa katika pwani ya Bahari ya Hindi mkoani Mtwara baada ya kuvutwa ukielea majini na wavuvi wa Kata ya Msangamkuu. Mzoga huo una urefu wa futi 48 na uzito unaokadiriwa kuwa zaidi ya tani 30.
Wananchi kutoka katika Kata ya Msangamkuu, Mtwara wakishuhudia mzoga huo.GPL(P.T)
Wakazi wa Mtwara wakiukata mzoga huo

PROFESA JAY (NIGGA J) KUZINDUA VIDEO ZA KIPI SIJASIKIA NA 3 CHAFU J'MOSI HII

Wednesday, September 3, 2014

CONTINHO NA JAJA KUONYESHA VITU VYAO UWANJA WA TAIFA LEO JIONI DAR

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgDGb-LS-MhaBAUcuGu2GZshDaGa5ays7COLjD15RfAOBp4T-nlnUsdwm65R5GaUPQ2zlYi2PqF_7M1zbHG7bXmFti_-HyjDD2cVdm4TPOfwkPx_7QK8H-94-jbqD2yZ4BGgaP1V3XZ8gz8/s1600/COUTINHO+NA+JAJA.jpg

Na MABANTANYAU FAMILY
Timu ya soka ya Yanga siku ya leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Thika United ya nchini Kenya,kwenye mchezo wa kujipima ubavu.
Mchezo huo ni maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara, ambayo inatarajia kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu. Maandalizi ya mchezo huo tayari yamekwisha kamilika,huku timu hizo zikitarajiwa kutoa burudani kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania.
Kumekuwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili,zikijinasibu kushinda mchezo huo.Huu ni mchezo wa nne wa kocha Marcio Maximo tangu achukuwe mikoba ililoachwa wazi na kocha Hans Der Plujim ambae alifungashiwa virago.Kwenye michezo mitatu ya mwanzo timu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi kwenye michezo yote .
Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.Continho,jaja kuonyesha vitu uwanja wa taifa leo
Timu ya soka ya Yanga siku ya leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Thika United ya nchini Kenya,kwenye mchezo wa kujipima ubavu.
Mchezo huo ni maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara, ambayo inatarajia kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu. Maandalizi ya mchezo huo tayari yamekwisha kamilika,huku timu hizo zikitarajiwa kutoa burudani kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania.
Kumekuwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili,zikijinasibu kushinda mchezo huo.Huu ni mchezo wa nne wa kocha Marcio Maximo tangu achukuwe mikoba ililoachwa wazi na kocha Hans Der Plujim ambae alifungashiwa virago.Kwenye michezo mitatu ya mwanzo timu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi kwenye michezo yote .
Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.Continho,jaja kuonyesha vitu uwanja wa taifa leo
Timu ya soka ya Yanga siku ya leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Thika United ya nchini Kenya,kwenye mchezo wa kujipima ubavu.
Mchezo huo ni maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara, ambayo inatarajia kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu. Maandalizi ya mchezo huo tayari yamekwisha kamilika,huku timu hizo zikitarajiwa kutoa burudani kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania.
Kumekuwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili,zikijinasibu kushinda mchezo huo.Huu ni mchezo wa nne wa kocha Marcio Maximo tangu achukuwe mikoba ililoachwa wazi na kocha Hans Der Plujim ambae alifungashiwa virago.Kwenye michezo mitatu ya mwanzo timu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi kwenye michezo yote .
Ushindi huo ukichagizwa na ujio wa wachezaji wa kibrazil, Continho na Jaja ambao wamekuwa kivutio kwa wapenzi wa soka, tayari wapenzi wa soka wa visiwani wamepata fursa ya kuwaona wachezaji hao.Sasa ni zamu ya wapenzi wa soka wa Tanzania bara.

GARI LA RAIS WA KENYA LAPATIKANA UGANDA BAADA YA KUIBIWA



Msemaji wa Rais alikana kuwa gari hilo lilikuwa limeibwa
Maafisa wakuu kutoka shirika la polisi wa kimataifa, Interpol amethibitisha kuwa gari la ulinzi wa rais Uhuru Kenyatta lililoibwa mjini Nairobi wiki jana limepatikana nchini Uganda.
Kwa sasa gari hilo limepelekwa mjini Kampala.
Gari hilo aina ya BMW liliibwa siku ya Jumatano usiku mjini Nairobi. Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na wizi huo.
Mkurugenzi wa polisi wa kimataifa Interpol nchini Uganda Assab Kasingye aliambia BBC kuwa gari hilo litarudishwa Nairobi.
Gari hilo liliibwa na watu waliokuwa wamejihami Jumatano wiki jana.
Hata hivyo msemaji wa serikali Manoah Esipisu alikanusha habari hizo akisema kuwa gari lililoibwa halikuwa na ulinzi wa Rais Kenyatta bali lilikuwa gari kuu kuu la polisi.
Lakini lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi aliyeripoti kuwa gari hilo ni mmoja ya magari ya ulinzi wa Rais.Afisa huyo wa polisi pia alisemekana kuwa mmoja wa maafisa wa polisi wa ulinzi wa Rais.
Tukio la wizi wa gari hilo, lilisababisha taharuki miongoni mwa maafisa wa ulinzi kwa sababu magari ya ulinzi wa Rais yenyewe yanapaswa kuwa na ulinzi mkali.
Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa visa vitatu vya wizi wa magari huripotiwa mjini Nairobi kila siku.
Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi vya wizi wa magari ambapo mtu yeyote anaweza kuathirika.