Saturday, October 3, 2015

Breaking News: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari

ChristopherMtikila
Taarifa zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (pichani) amepata ajali na kufariki dunia alfajiri ya leo eneo la Msolwa-Chalinze.
inaungana na wanachama wa DP pamoja na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Mchungaji Mtikila Amen.
mtikila
Pichani ni gari iliyopinduka na kumuua Mchungaji Mtikila.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama cha DP, Abdul Mluya