Wednesday, July 22, 2015

AWASHUKURU WATANZANIA BAADA YA KUPATA TUZO DIAMOND

Diamond akisikiliza masali kutoka kwa waandishi wa habari.
… Akijibu maswali.
…Bab Tale akiwakaribisha waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mmoja wa mameneja wa Diamond, Said Fella (Mkubwa na wanawe) akieleza jambo kwa waandishi wa habari.
Mwakilishi kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, Hamza Dalla akifuatilia kwa makini kikao hicho.
….Akiwa ameshikilia tuzo yake baada ya kumalizika kwa kikao na waandishi wa habari.
Akiwa katika pozi ya la kufurahia tuzo hiyo.
Mwandishi wa habari wa Global Publishers, Brighton Masalu (kushoto) akiwa ameshikilia tuzo ya Diamond.
Diamond (katikati) akiingia ukumbini humo akiwa na mmoja wa mameneja wake, Bab Tale (mwenye shati jekundu).
Baadhi wa waadishi wa habari wakimfuatilia kwa umakini mkubwa.
SIKU chache baada ya kurejea nchini akiwa na tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa kiume (Best Live Act), mfalme wa muziki wa Bongo fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewashukuru Watanzania kwa moyo wa upendo waliouonesha kwa kumpigia kura na kumuwezesha kutwa tuzo hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ndani ya Hoteli ya Ntansoma jijini Dar, pia  msanii huyo aliitaka serikali na makampuni binafsi kuwaunga mkono wasanii wachanga wanaotamani kuutangaza muziki wetu katika anga la kimataifa kutokana na kile alichokiita ugumu na changamoto nyingi.