Basi la abiria la NGANGA lililogongana na fuso na kuwaka moto
Basi hilo la Nganga likiteketea kwa moto
Gari la kubebea mizigo aina ya fuso likiwa linateketea kwa moto
Habari zilizotufikia punde zinasema watu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto maeneo ya milimani kilomita kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. Pichani ni basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara zitapopatikana.