Wednesday, March 11, 2015

AJALI YAUWA WATU ZAIDI YA 50 LEO MAFINGA

                                          





                                                                                               BREAKING NEWS:



 Ajali imetokea changalawe Mafinga basi la Majinja lilikuwa linatokea Mbeya kwenda Dar limeangukiwa na kontena muda huu na watu wengi wanakadiriwa kufariki na hali ni mbaya sana
Watu wapatao 50 wanahofiwa kufa papo hapo baada ya basi hilo la Majinja Express kugongana na lori na kuangukiwa na kontena

Tuesday, March 10, 2015

MATUMLA JR. KUMVAA MKOREA MACHI 27 MWAKA HUU

Bondia mkongwe nchini Rashid Matumla, kutoka kushoto, Mohamed Matumla, Japhet Kaseba na Rais wa (TPBO), Yassin Abdallah 'Ustaadh' katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).(P.T)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Rais wa TPBO, Yassin Abdallah 'Ustaadh'.
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Mohamed Matumla Jr ambaye ni mtoto wa gwiji wa zamani wa mchezo huo, Rashid Matumla ‘Snake Boy’ anatarajia kupanda ulingoni Machi 27, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kugombania nafasi ya kwenda kushindania ubingwa WBF dhidi ya Mkorea, Wang Xi Hua.
Licha ya hivyo, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustaadh’, amewataja mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, kuwa ni Japhet Kaseba atakayegombania ubingwa wa UBO Afrika dhidi ya Mada Maugo huku Thomas Mashali akitarajia kuwania ubingwa UBO  Afrika kilo 76 dhidi ya Karama Nyilawila

ARSENAL YAITOA KOMBE LA FA MAN UTD

WELBECK
Timu ya Arsenal usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA baada ya kuwalaza mahasimu wao Manchester United kwa jumla ya mabao 2 -1.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Danny Welbeck aliyerejea Old Trafford akiwa na Arsenal ndiye aliyepigilia msumari wa moto kwenye kidonda baada ya kupachicha goli la pili lililoipeleka moja kwa moja Arsenal kwenye hatua ya nusu fainali.

Friday, March 6, 2015

ALBINO WAZICHAPA KAVUKAVU IKULU DAR ES SALAAM




Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), wamepigana ngumi na mateke wakigombea kuingia kumwona Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam. Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ambapo lilianzia kwenye eneo la mapokezi Ikulu mara baada ya walemavu hao kukaguliwa na kuwekwa kwenye chumba maalumu cha kupumzikia wageni. Baada ya muda, ofisa wa Ikulu alifika kwenye chumba walipokuwa walemavu hao akiwa na karatasi yenye orodha ya watu 15, ambao ndio waliopaswa kumwona Rais. Kila ofisa huyo alipokuwa akisoma jina, mhusika alitoka nje ya chumba hicho tayari kwa kwenda kumwona Rais. Baada ya ofisa huyo kumaliza kusoma majina hayo, alisema: “Hawa ndio wanaokwenda kuwawakilisha kwa sababu hamuwezi kuingia kundi lote hili.”Wale wengine walioachwa hawakukubaliana na hali hiyo basi vurugu ndio likaanzia hapo!