Saturday, January 9, 2016

MKAPA KUFANYA KAZI NA RAISI MAGUFULI

Rais Dk John Magufuli akizungumza na Rais
Rais Dk John Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar leo. Picha na Ikulu  
By Mabantanyau family
Dar es Salaam. Rais mstaafu Benjamin Mkapa amesema yuko tayari kufanya kazi yoyote na kutoa ushirikiano wake kwa serikali ya Rais John Magufuli endapo atahitajika.
Mkapa aliyeambatana na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba ametoa kauli hiyo leo punde baada ya kukutana na Rais John Magufuli Ikulu, Dar es Salaam.
“Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo,” taarifa iliyotolewa na Ikulu leo mchana imeeleza.
Kwa mujibu wa Ikulu, malengo ya mkuu huyo wa zamani wa nchi kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na Watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba amempongeza katika juhudi zake katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Jaji Warioba amewataka Watanzania wote kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi anazofanya ikiwemo kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.
"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachia, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini Watanzania wote tushughulike na matatizo hayo," amesisitiza Jaji Warioba.

Saturday, October 3, 2015

Breaking News: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari

ChristopherMtikila
Taarifa zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (pichani) amepata ajali na kufariki dunia alfajiri ya leo eneo la Msolwa-Chalinze.
inaungana na wanachama wa DP pamoja na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Mchungaji Mtikila Amen.
mtikila
Pichani ni gari iliyopinduka na kumuua Mchungaji Mtikila.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama cha DP, Abdul Mluya

Sunday, September 13, 2015

JANA WAFANYIKA UZINDUZI WA CHEZA KWA MADOIDO NDANI YA DAR LIVE

1.
3.
Yamoto Band wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Wasanii wa Yamoto Band, Enock Bella (wa kwanza kushoto) akifanya yake na Aslay (kulia).(P.T)
4.Msanii Ruby akiwa stejini kufanya yake.
Msanii wa Bongo Fleva, Hellen George 'Ruby' akifanya yake stejini.
9.
...Ruby akiimba wimbo wake 'Na Yule'.
5.Shetta akitoa burudani kwa mashabiki wake.
Msanii wa Bongo Fleva,  Shetta akitoa burudani kwa mashabiki wake.
6.Shetta akikonga nyoyo za mashabiki wake.
Shetta akiendelea kuwapa burudani mashabiki zake.
7.Chegge na Temba mzuka ukiwa umewapanda stejini.
Chegge na Temba wakikamua stejini.
7
...Chege akiendeleza makamuzi.
10.Queen Dar leen akitoa burudani katika mashabiki wake.
Queen Darleen akitoa burudani kwa mashabiki wake.
8.
Makamuzi yakiendelea ndani ya Ukumbi wa Dar Live.
11.Mwimbaji wa Taarabu kutoka Bendi mpya ya Moyo Medern Taarab akiimba.
Mwimbaji wa Moyo Modern Taarab akiimba jukwaani.
12.Bebdi ya Moyo Modern Taarab ikitoa burudani.
13
14
15
Bendi ya Moyo Modern Taarab ikitoa burudani.
16.Mpiga kinanda wa Moyo Modern Taarab akifanya yake.
Mpiga kinanda  wa Moyo Modern Taarab akifanya yake.
17.Bonge la Nyau akionesha manjonjo.
18.
19
20.
Madansa wakifanya yao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana usiku.
VIJANA wanaounda Bendi ya Yamoto, usiku wa kuamkia leo wameangusha burudani ya aina yake katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar wakati vijana hao wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido.
Kabla ya uzinduzi wa Cheza kwa Madoido, wasanii mbalimbali walipanda jukwaani kutoa burudani ikiwemo bendi mpya ya Taarab iitwayo  Moyo Modern Taarab inayomilikiwa na kiongozi wa Yamoto Band, Said Fela.
Wasanii mbalimbali wa chipukizi nao walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwa kuimba nyimbo mbalimbali ambapo wapenzi wa burudani waliburudika vya kutosha.
Katika listi ya wasani waliotumbuiza jukwaani ni pamoja na Ruby, Dulla Yeyo, Izeman huku Moyo Modern Taarab wakipagawisha na nyimbo zao kali zinazojulikana kama Haijalishi, Dongo la Gizani na Zetu Duwa.
Wengine waliokamua jukwaani ni Chegge, Temba, Queen Darleen, Shetta, Ditto na wengine kibao kisha uzinduzi wa Cheza kwa Madoido kufanyika katika ‘skrini’ kubwa kisha Yamoto Band kutumbuiza shoo kali

Wednesday, July 22, 2015

AWASHUKURU WATANZANIA BAADA YA KUPATA TUZO DIAMOND

Diamond akisikiliza masali kutoka kwa waandishi wa habari.
… Akijibu maswali.
…Bab Tale akiwakaribisha waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mmoja wa mameneja wa Diamond, Said Fella (Mkubwa na wanawe) akieleza jambo kwa waandishi wa habari.
Mwakilishi kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, Hamza Dalla akifuatilia kwa makini kikao hicho.
….Akiwa ameshikilia tuzo yake baada ya kumalizika kwa kikao na waandishi wa habari.
Akiwa katika pozi ya la kufurahia tuzo hiyo.
Mwandishi wa habari wa Global Publishers, Brighton Masalu (kushoto) akiwa ameshikilia tuzo ya Diamond.
Diamond (katikati) akiingia ukumbini humo akiwa na mmoja wa mameneja wake, Bab Tale (mwenye shati jekundu).
Baadhi wa waadishi wa habari wakimfuatilia kwa umakini mkubwa.
SIKU chache baada ya kurejea nchini akiwa na tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa kiume (Best Live Act), mfalme wa muziki wa Bongo fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewashukuru Watanzania kwa moyo wa upendo waliouonesha kwa kumpigia kura na kumuwezesha kutwa tuzo hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ndani ya Hoteli ya Ntansoma jijini Dar, pia  msanii huyo aliitaka serikali na makampuni binafsi kuwaunga mkono wasanii wachanga wanaotamani kuutangaza muziki wetu katika anga la kimataifa kutokana na kile alichokiita ugumu na changamoto nyingi.